Hold on a minute!!.... Lengo la Mkutano wa Jangwani lilikuwa nini... lilifikiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hold on a minute!!.... Lengo la Mkutano wa Jangwani lilikuwa nini... lilifikiwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 28, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya CDM.. ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa CDM Jangwani siku ya Jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

  a. Kuanzia M4C kitaifa (ni marudi ya lile la Arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
  b. Kuwaambia wananchi kuhusu Katiba Mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
  c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
  d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
  e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini? zinachangia CDM taifa au CDM mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
  f. x,y


  Kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. maana baada ya Jumamosi kupita leo Jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a M4C?

  Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la Jumatano la gazeti..
   
 2. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Kimsingi malengo yalifikiwa, japo si 100% yamesemwa sana kuwa Cdm ni ya kikabila, ni ya kikanda yaani kaskazini hususa wachaga. Na walisema haikubaliki pwani, Dsm na kusini, sasa waliwadhihirishia wabaya wao kuwa Cdm ni ya Watanzania wote, bila ya kujali kabila, dini, ukanda wala jinsia, na iko tayari kushika dola 2015. Mungu ibariki CHADEMA.
   
 3. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji mimi nakukubali sana you have something in your mind.Isitoshe unamsimamo wa kile unachokiamini that is nice to see.Napenda watu wa design yako sio watu waoga kuuliza wasichokielewa.Pamoja sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. d

  dada jane JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwangu binafsi naona malengo yao yametia kwa kiasi kikubwa hasa kuvunja rekodi na kuanzisha cdm square.
   
 5. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Yawezekani lengo lilifanikiwa kwa 40% ila tusiishie hapo sote kwa pamoja twatakiwa tuwe wachezaji na sio washabiki ili tuweze kuikomboa nchi yetu. Je? Huu muungano wa bara na zanzibar unafaida gani kwa wabara? Naomba ziletwe kura za maoni tuuvunje muungano tuache kunyanyaswa kila siku na hako kamkoa kajiitacho nchi.
   
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  mwanakijiji you have brain, i was asking ma self the same qns but in different sentences.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  Hili haliwezi kuwa lengo kwani uchaguzi wa 2010 ulishalithibitisha hilo na wapiga kura wa Tanzania walishakataa hoja hizo za ukanda na ukabila; au CDM wamesahau kuwa wamepata wabunge na madiwani kuanzia Kusini hadi Kaskazini, Mashariki hadi Magharibi? Mbozi, Maswa, Kiwira, Songea,? Wanataka kuthibitisha nini? So hili haliwezekani kuwa lengo kwani ni redundant.
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Malengo yametimia sana tu we subiri effect zake mwka 2015!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Lengo gani lilifikiwa kwa asilimia 40?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  May 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Yapi hasa yaliyofikiwa?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  May 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  What? lengo lilikuwa kuanzisha CDM Square? Nachukulia kwamba unatania tu this Monday morning
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  May 28, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  kama yeye ni rare!! kweli tatizo lake au uzuri wake ni lugha nzuri na ushawishi. Mimi binafsi nina misimamo yangu, tatizo langu ni lugha yangu mbaya.....huwa naona kama wafuata mkumbo, wasiofikiria na wasiokuwa na uwezo wa 'ku-question why this why that' wana matatizo ya akili, huwa naona kama retarded fulani na siwezi kuchukuliana nao! huyu bwana MKJJ ni zaidi ya kardinali!
   
 13. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mkuu yalifikiwa kwa 90%ni changamoto ndogo za kurekebisha kama swala mabadiliko ya katiba na uchumi na hali ya kisiasa ya nchi vipewe mda mwingi zaidi kwani hapo ndipo wanahitaji kusikia na kuhamasika zaidi, halafu swala uchangishaji fedha linahitaji utulivu kwani watu walihamasika lakini mh.mwenyekiti mbowe alichanganya changanya kidogo kama ulitazama vizuri watu wanahitaji changia fedha kwa wakusanya fedha wakati huo huo wanaendelea na zoezi la kujivua gamba hali hii ili fanya wakusanya fedha kutofkia watu wote,kwani walikua wamekaa kwa mara ya kwanza lakini mbowe aliposema watu wasimame utratibu wa ukusanyaji haukuwa mzuri sana.

  So nawashauri wakati wa kukusanya fedha wahamasishe watu wakae chini ili watu wanao pitisha fedha wachangie vizuri, na mwisho swala kubana matumizi ya mda ni mhimu sana,kuna mambo yana umuhimu kidogo wasiyape kipaumbele sana kama kila anayetambulishwa si lazima aongee, watu wanahitji zaidi kuwasikia mwenyekiti na katibu na zaidi tundu lisu akizungumzia katiba na swala la muungano, nitarudi baadae kidogo................................!
   
 14. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  la mkutano wa jangwani dar. Pamoja na kupata vijana za idi ya 3000 walio juvua gamba na kuvaa gwanda,pia nilitarajia wakina mama na wazee wa dar ambao hukaa magogoni na kushabikia hotuba za kikwete, nao pia wangelivua gamba na kuvaa gwanda kwa mkutano wa jangwani, pia hoja ya katiba mpya haijafanikiwa kwa 100% nilichokimaanisha 40% nikutokana na msemo wa waswahili, kubeba mimba si kazi , kazi ni kulea mwana. Chadema bado twahitajika kutia bidii zaidi.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  May 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  Mmoja amesema kuwa yamefikiwa kwa asilimia 40! sasa sijui mnazungumzia malengo hayo hayo au tofauti? Wewe unaposema yamefikiwa kwa asilimia 90 ni yapi haya?
   
 16. T

  Thesi JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  MMK c kweli. Uchaguzi wa 2010 unaonyesha kwamba watu waliikataa CDM mikoa ya pwani na hata Dar ambako kuna wakaazi wengi waislamu, waliambulia wabunge wawili Dar, mji mkuu ambao ungetakiwa kuwa mfano kuchagua upinzani kuwa chachu ya mabadiliko. Sehemu inakofanya kazi propaganda za ukanda na udini ni Zanzibar na pwani. Lengo lilikuwa kuanza kuhamasisha watu wa pwani dhidi ya dhana hiyo ambayo wanaanza sasa kupiga kambi kwenye mikoa hiyo kuondoa dhana hiyo potofu.
  Pili ni vizuri kuelezea Watanzania kuhusu misimamo yao juu ya uundwaji wa katiba. Hii aliiongelea hasa Lisu. Hii nayo atasema walishatuambia huko nyuma lakini anajua ni wangapi wanajua hilo?
   
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji kuna mahali pana shida au jambo ambalo halijajulikana sidhani kama CDM inahitaji kuita watu jangwani ili wavue gamba na kuvaa gwanda, pia sidhani kama wanaweza kuita watu jangwani ili kufanya harambee ya chama, pia siamini kama kwa muda ule wangeweza kuelimisha juu ya muungano au hata uundwaji wa katiba mpya.

  Kwangu mimi nafikir malengo yao yalipaswa kuwa juu zaid ya hapo, unless kama wanayafanya siri ila kwa uelewa wangu mdogo CDM inatakiwa iuze sera zake mbele za watu ionyeshe japo ina M4C lakin wao wana sera gapi ambaazo zinamtetea mtanzania, na mpaka sasa katika sera hizo kwa kuwa ni chama kikubwa cha upinzani wamefanya nini.

  Nahofia kuwa yawezekana kabisa kuna ambayo wao waliyatoa kama sehem ya hotuba zao za kuhamasisha lakni yatatumiwa na CCM kama ilani yao au moja ya sera ake kwa wakati ujao.

  Namshauri Mbowe kaka yangu aangalie kwa makini watanzania wanataka nini na watueleze wa mikakati gani ya kutupa yale tunayoyataka. hili nafikir liwe ndio lengo kubwa la kampeni hii ya M4C. tena wawe makini sana manake kama vijana wa kiume ndio waliokuwa wengi pale, wakifuatiwa na vijana wa makamu basi ajue hapo pana mob psychology tu ambayo after certain period yaweza kuhamishiwa kwingine. Watu wanahitaji kujua sera za chama, na mbinu au njia gani zitatumika kutimiza sera hizo tena elim hii baada ya kuambiwa basi wapewe na vikabrasha vitakavyo elezea haya kwa umakini.
  jamani naomba tu msinishambulie
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Thesi kwani ni kwasababu ya kupata wabunge wawili tu ndio wamesukumwa kufanya mkutano huu? haya nisiuzungumzie ukanda wala udini lakin je unafikir kwa kufanya haya tu CDM ndo itapata wanachama wengi? Je umewah kufikiri kama CDM ingekuwa inapita kunaadi sera zake na mbinu zitakao tumika kumeet wanayoyasema kisha wakapendelea kusikiliza ushauri wa watanzania kwenye kutimiza hayo Cdm ingevuna wanachama wangapi?


  binafsi siyo mpenzi wa maneno yenye kuoopesha kwa maana ya maneno makali lakin pia yakitumiwa katka kuelezea sera ni afadhali zaid kuliko yakitumiwa katika kuelezea mapungufu ya mtu mwingine
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Afadhali umeniwakilisha ktk hili. Nami pia nilikuwa najiuliza vivyo hivyo. Lakini pia ningependa kutoa ushauri kwa CDM kwamba sisi watz wa vijijini ambao ni wengi tunahitaji sana elimu ya uraia ili tujitambue (sijui kwa mijini ingawa picha ya mkutano wa jumamosi imeonesha kwamba tuko kwenye 'mtumbwi' mmoja). Vinginevyo, pamoja na kuvuna wanachama wengi, haitakuwa na maana iwapo tutavua magamba ya mwili tu lakini fikra zetu bado ni zilezile za 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Tunahitaji kufunguliwa na kuaminishwa kwamba tunahitaji mabadiliko na ni mabadiliko ya namna gani na kwamba sisi wenyewe ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko. Picha niliyoipata jumamosi haitofautiani na iliyoko vijiji vya huku kwetu, kwamba mabadiliko yataletwa na viongozi. Tunashangilia kwa nguvu zote mikutanoni lakini baada ya hapo tunayaacha hapohapo na kama tunaondoka na kitu basi ni kuelezana namna mlivyokuwa mkitiririsha vina jukwaani. Uchaguzi ukifika mnajua kinachotokea. Ni kwa sababu imani ya wananchi kwa CDM haikulelewa. Niliona jumamosi walalahoi wenzangu wanashangilia lakini kwenye mambo ya msingi wa ukombozi wao walikaa kimya, ilinionesha hawakuelewa. Kwa hiyo kazi bado ni kubwa. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ila naamini ktk mabadiliko. Natamani kuendelea lakini simu ya mchina inanitesa.
   
 20. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  inamaana Mwanakijiji huoni if there is something gained by CDM from the meeting? Do you mean CHADEMA's Popularity in Dar is just the same as it was before the meeting?

  Do you mean the 'fear' that CCM has on CDM is just the same as it was before the meeting?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...