#COVID19 Hoja za baadhi ya Watanzania kuhusu kukataa chanjo bado ni dhaifu sana

Kijiwe cha kahawa pale Temeke nusra wazichape.

Wa kwanza: Aisee juzi mh.Samia amechomwa hadharani chanjo ya CORONA

Wa pili : Uongo mtupu ,yule kachomwa maji matupu

Wa tatu: Acha ujinga ukichomwa maji unavimba ta..o ndio maana mkeo(akimjibu wa pili) ta toka alazwe AMEKUWA NA WOWOWO

Wa nne : Ndugu yangu tuheshimiane usifike huko....ninasemaje ,mh.Rais kachomwa chanjo ya PEPOPUNDA

Wa tano : Nyinyi mac...ko mtakuwa mas...uger kuendekeza chanjo za mabeberu.

Ustadhi mmoja akainuka na kumkwida huyo jamaa wa 5 akimtahadharisha kauli zake.

HAWA NDIO BAADHI YA WATANZANIA 🤣🤣

#TukitokezeniKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#KaziIendelee
 
Mtu anayemsikiliza na kumwamini Gwajima ujue lazima atakuwa msukule wa kanisa lake au muumini wa imani ya yote yaliyosemwa na mwendazake...
Ana uliza kama chanjo ni ya kweli mbona watu waliochanjwa wanakufa?

Nami namuuliza

Kama kanisa lako ni la ufufuo na uzima kwanini waumini wako wanakufa?

Kwanini hukumfufua mwajiri wako alipokufa?

Akijibu hayo maswali kwa tafsiri yeyote itayoonesha ufufuo wake ni wa kweli, inabidi afungwe sello akanyee makasha kwa kosa la kumuacha mwendazake aende zake ili hali alikua na uwezo wa kum ressurect
 
ETI Katika hoja wanazotumia wanasema eti chanjo gani ambayo serikali imejitoa kabisa kwamba litakalokupata wao hawawajibiki kwa lolote ?

Watanzania wamesahau kwamba hata ukienda hospitali una haki ya kukataa kutibiwa,una haki ya kukataa sawa,una haki ya kumkataa daktari usiyemtaka asikutibu.

Endapo ukikubali kutibiwa kwa ridhaa yako na katika tiba hiyo ukapata madhara basi hakuna daktari atakayewajibika eti ahukumiwe kwa jambo hilo.

Hata ukienda kufanya upasuaji lazima ukubali kusaini,usaini ukaenda ukafa kwenye upasuaji ujue hakuna utakayemlaumu kwa sababu ulikubali mwemyewe.

Hivyo sio kwenye korona tu hata kwenye tiba zingine wanaohusika na jambo hilo wanajivua endapo ukikubali kufanyiwa jambo hilo litakalo kupata lakwako wewe.

Hivyo serikali ipo sahihi kujitoa lwenye lawama kwa sababu mtu atachoma chanjo akiumwa kichwa tu atataka aiwajibishe serikali kwamba chanjo inamdhuru,katika hili serikali imefanya vyema.
Daktari akiwa mzembe atahukumiwa tu, sio kwakua umesign basi daktari anakua hana hatia na baya litakalokupata.

Nadhani uliisikia ile skendo ya mtu wa kichwa kutibiwa mguu na wa mguu kutibiwa kichwa, kwa hapo utasema eti sijui umesaini daktari hana kosa?

Vivyo hivyo kwa serikali vipi kama hiyo chanjo ina madhara na watu wakafa kama kuku, itaacha tu kisa wamejitoa? Na wewe unaona ni sahihi kabisa serikali kujitoa kwenye kitu ilicholeta yenyewe, inakipigia debe, matangazo kibao afu wanajitoa kwenye hatia kwa chochote kitachotokea, yani ile kitu ya wao kujitoa ndio imetia mashaka wengi sana.

Ni sawa na mtu akupe kitu usichojua uhatari wake na ajitoe endapo litakupata baya lolote basi usimhusishe.
 
Wewe mwenyewe huna hoja.

Kama chanjo ni salama 100% kwa nini serikali ikujazishe indemnity form?

Anyway, kila mtu ana mwili wake, anaetaka kuchanjwa achanjwe na asietaka hivyo hivyo.

Anaetaka kuchanjwa asilazimishe mwingine kisa yeye anataka achanjwe na asietaka hivyo hivyo.

Kila mtu ana haki na matumizi ya mwili wake
 
Daktari akiwa mzembe atahukumiwa tu
Umeshasema akiwa mzembe yeye na sio dawa,hpja kubwa ni dawa na huduma anayotoa,sidhani kama hukuelewa mantiki ya hoja yangu.
sio kwakua umesign basi daktari anakua hana hatia na baya litakalokupata.
Ndivyo ilivyo,akikutibu sehemu sahihi kwa dawa sahihi kwa mujibu wa muongozo husika litakalotokea yeye hawajibishwi.

Sasa kama muongozo unasema afanye upasuaji wa kichwa wewe ukafanya wa mguu manake ikuwa nje ya muongozo.

Ukifanya upasuaji wa kichwa mgonjwa akafa kwa kukosea baadhi ya procedures haitosemwa uzembe na huna pakumshitaki popote.

Au nesi anasafisha vidonda bahat mbaya vikapata infection kutokana na dressing mbaya ya nesi,huna pa kumpeleka kwamba eti kakusababishia infection.

Au umewekewa catheter (kipira cha mkojo)ukapata infection kwenye kibofu alafu ukataka kushtaki kwamba eti ooh wamekusababishia infection,hiyo utajua mwenyewe mkuu kwa sababu ulishakubali na umefanyiwa kwa mujibu wa muongozo.
kwa hapo utasema eti sijui umesaini daktari hana kosa??
Sasa kama muongozo unasema kichwa wewe unaenda kwenye mguu manake umekeuka muongozo husika.

Tibu kwa muongozo hata mgonjwa akipata shida hakuna wa kukushtaki.
Vivyo hivyo kwa serikali vipi kama hiyo chanjo ina madhara na watu wakafa kama kuku,
Tolea mifano halisi,usitoe mifano ya kutisha ili univutie kwenye hoja yako wakati kimsingi unatoa mifano ambayo haijawahi kutokea hapa nchini kwa chanjo zote ambazo serikali imezithibitisha.

Watu watakufa kwa ugonjwa tu lakini hawatokufa kwa sababu eti ya chanjo waliyodungwa.
itaacha tu kisa wamejitoa
Toa mifano halisi.

Usitoe mifano ya kufikirika ili kupinga jambo halisi.
Na wewe unaona ni sahihi kabisa serikali kujitoa kwenye kitu ilicholeta yenyewe,
Naam ni sahihi hiyo haina maana kwamba ukichoma chanjo ukapata homa eti ukienda spitali hautibiwi wala kusikilizwa hapana,ukipata complication yoyote ile ukienda hospitali za serikali utasikilizwa na kupatiwa huduma pale inapowezekana.

Lakini suala la kusema kwamba eti serikali ndio imekukusudia ikutie maradhi hayo hilo jambo serikali imejitoa kwa sababu haukulazimishwa.
kujitoa kwenye kitu ilicholeta yenyewe, inakipigia debe, matangazo kibao afu wanajitoa kwenye hatia kwa chochote kitachotokea
Serikali inajenga barabara kibao na kuzipigia debe hizi barabara za lami lakini bodaboda kila siku wanakufa utailaumu serikali kwa sababu ndo imejenga ?

Madhara ya chanjo kama barabara tu,kuna watakaosalimika na watakaopata madhara wasimlaumu aliyeweka yeye kazi yake ni kujiridhisha na kuleta.
kujitoa kwenye kitu ilicholeta yenyewe, inakipigia debe, matangazo kibao afu wanajitoa kwenye hatia kwa chochote kitachotokea
Lakini pia serikali inapiga debe utumiaji wa ARV kwa watu wenye HIV,lakini ukiangalia madhara ya ya ARV kwa muda mrefu inapelekea chronic disease hatari sana
Kama vile cancer na hata kufeli kwa figo inaweza kusababisha

Kwa madhara ya ARV kama una afya ya akili huwezi kusema unailaumu serikali kwa kuleta ARV .
yani ile kitu ya wao kujitoa ndio imetia mashaka wengi sana
Kwa sababu watanzania wengi ni wajinga tunakubali hoja za kitoto ambazo hazina maana.

Kwa hivyo kama ambavyo sisi watz wengi ni wajinga ndio maana hilo limewatia wengi mashaka,
 
Ana uliza kama chanjo ni ya kweli mbona watu waliochanjwa wanakufa?

Nami namuuliza

Kama kanisa lako ni la ufufuo na uzima kwanini waumini wako wanakufa?

Kwanini hukumfufua mwajiri wako alipokufa?

Akijibu hayo maswali kwa tafsiri yeyote itayoonesha ufufuo wake ni wa kweli, inabidi afungwe sello akanyee makasha kwa kosa la kumuacha mwendazake aende zake ili hali alikua na uwezo wa kum ressurect
Alishindwa kumfufua mama yake atawezaje kumfufua mwajiri? Anafufua misukule yake inayomwabudu kwa mtindo wa Bongo movie...
 
Umepigia mbuzi gitaa, sina hakika kama duniani kuna watu wajinga na mbumbumbu kama Tanzania
 
Chanjjo mabayo ni salama 100% inakuwa na sifa gani ?

Jambo gani ambalo limetimia kwa 100% lisilohitaji ridhaa ya mgonjwa hasa katika mambo ya kitiba ?
Unaposema 100% safe maana yake there is no any side effects whatsoever. 100% is 100% safe.

Serikali inasema it is 99.99% safe, lakini inakujazija indemnity form kwamba ukipata matatizo usii hold accountable, wtf.

Nimechoma sindano ya Hipatitis B sikujaza Indemnity form. Nimechanjwa chanjo nyingi huko nyuma nikiwa mdogo wazazi wangu hawakujazishwa indemnity form.

Leo hii unasema chanjo is safe 100% halafu nijaze indemnity form, huhitaji elimu ya form four kujua kua kuna jambo sio zuri linafichwa.
 
Serikali inajenga barabara kibao na kuzipigia debe hizi barabara za lami lakini bodaboda kila siku wanakufa utailaumu serikali kwa sababu ndo imejenga ?

Madhara ya chanjo kama barabara tu,kuna watakaosalimika na watakaopata madhara wasimlaumu aliyeweka yeye kazi yake ni kujiridhisha na kuleta.
Unanituhumu kwa kutoa mifano isiyo halisi, sasa wewe huu mfano wa ujenzi wa barabara sijui umekujaje hapa. Chanjo ni tofauti na huo mfano wako wa barabara, sio wote wataitumia kwa matumizi sawa hiyo barabara lakini chanjo nyote mnaochanjwa ni sawa nadhani kwa kila kitu.

Naam ni sahihi hiyo haina maana kwamba ukichoma chanjo ukapata homa eti ukienda spitali hautibiwi wala kusikilizwa hapana,ukipata complication yoyote ile ukienda hospitali za serikali utasikilizwa na kupatiwa huduma pale inapowezekana.

Lakini suala la kusema kwamba eti serikali ndio imekukusudia ikutie maradhi hayo hilo jambo serikali imejitoa kwa sababu haukulazimishwa.
Daah sio kua watu walikua hawaumwi kabla ya chanjo, hapana na wala sio kua wakichanjwa wataacha kuumwa, pia hapana. Wasiwasi wa sisi wananchi hadi kutoiamini serikali kwenye hili suala ni hiyo misimamo yake inayotia mashaka. Walikua hawazitaki izo chanjo kabisa na kashfa kibao tena mpaka viongozi wa kwenye kada ya afya, leo hii wanaleta chanjo na kusema usign kabisaa kua ukipata side effects wao hawahusiki, chanjo sio upasuaji. We ushawahi kwenda hospitali ukatibiwa na kusain form kama ile?? Kwa mimi sijawahi , we amini tu uaminivyo ndgu yangu kikubwa ni hiari kuchanjwa.

Lakini pia serikali inapiga debe utumiaji wa ARV kwa watu wenye HIV,lakini ukiangalia madhara ya ya ARV kwa muda mrefu inapelekea chronic disease hatari sana
Kama vile cancer na hata kufeli kwa figo inaweza kusababisha

Kwa madhara ya ARV kama una afya ya akili huwezi kusema unailaumu serikali kwa kuleta ARV .
Sitakupinga kama jinsi ARV zilivokuja ndivyo hizi chanjo za corona zilivyokuja. Zimekaa kisiasa mnoo. Serikali nzima inazipigia debe wakati mwaka jana hao wote walikua wakizikandia 😂😂 siasa mpaka kwenye maisha ya watu.

Kwa sababu watanzania wengi ni wajinga tunakubali hoja za kitoto ambazo hazina maana.

Kwa hivyo kama ambavyo sisi watz wengi ni wajinga ndio maana hilo limewatia wengi
Hoja za kikubwa ndio zipi hizo, yaani mtu ajiridhishe chanjo kua 90+% iko sawa, afu aseme ukichanjwa usaini lilikukuta jambo mie simo. Ni akili ya kawaida tu kujua kua haziko sawa kwa asilimia hizo ama lah kuna kundi linaathirika nazo kwa namna moja ama nyingine.
 
Huko zinakotoka Chanjo America kuna watu wamegoma kupata chanjo ya Corona. Watu waliochanjwa America ni million 168 wakata America Idadi ya watu million 300 .
Watu waliogoma America watakuwa na hoja dhaifu ?
wakati wao Madaktari wanaotengeneza hizo Chanjo wanaishi nao , wanakula nao wanapata taarifa zaidi kuliko hata wewe Mtanzania
 
Watu waliogoma America watakuwa na hoja dhaifu ?
Waamerica kama wanatoa hoja kama hizi za watanzania basi nao watakuwa wajinga.

Au wazungu wanatoa hoja kwamba na wao wanataka kuangamizwa na wazungu wenzao kama ambavyo wafrika tunavtodanganyana ?
 
Unaposema 100% safe maana yake there is no any side effects whatsoever. 100% is 100% safe
Hii tafsiri ya kwwmba 100% safe maana yake haina any side effects umeitoa wapi ?


Nimechoma sindano ya Hipatitis B sikujaza Indemnity form. Nimechanjwa chanjo nyingi huko nyuma nikiwa mdogo wazazi wangu hawakujazishwa indemnity form.
Hiyo chanjo ya hepatitis uliyochoma ni wapi serikali imesema itahusika na side effects ambazo utazipata kwa kuchoma chanjo hiyo ?


Mana pengine ukawa unapinga maandishi wakati mfumo ni ule ule.

Leo hii unasema chanjo is safe 100% halafu nijaze indemnity form
Kwani unapojaza consent form katika matibabu mengine ina maana hakuna side effects zinazoweza kutokea katika matibabu hayo ?

Unapokubali kuchomwa sindano maana yake hakuna side effects za sindano ?
Nimechanjwa chanjo nyingi huko nyuma nikiwa mdogo wazazi wangu hawakujazishwa indemnity form
Lengo la hiyo fomu ni ridhaa yako.

Kama wazazi wako waliridhia uchomwe chanjo maana yake hiyo form kazi yaange ingelikuwa kuhifadhi kumbukumbu ya ridhaa yao.

Hivyo hapa unakataa lugha lakini maana ni ile ile.
 
Huko zinakotoka Chanjo America kuna watu wamegoma kupata chanjo ya Corona. Watu waliochanjwa America ni million 168 wakata America Idadi ya watu million 300 .
Watu waliogoma America watakuwa na hoja dhaifu ?
wakati wao Madaktari wanaotengeneza hizo Chanjo wanaishi nao , wanakula nao wanapata taarifa zaidi kuliko hata wewe Mtanzania
Huto muamerika anakataa chanjo kwa sababu wazungu ni watu wabaya ?

Huyo muamerika anakataa chanjo kwa sababu hawawapendi waafirica ?

Huyo mzungu anakataa chanjo kwa sababu eti kuna chip ndogo kwenye chanjo watapandikizwa ?
 
Unanituhumu kwa kutoa mifano isiyo halisi, sasa wewe huu mfano wa ujenzi wa barabara sijui umekujaje hapa
Umekuja hapa kwa sababu ni mfano halisi.
Chanjo ni tofauti na huo mfano wako wa barabara
Hiyo ni mifano hai kwa sababu

Kwanza barabara zipo halisi na ajali zipo halisi zinatokea,fuatilia takwimu za ajali za barabarani utaona kwamba hizo ajali zinahusisha watu ambao wapo na zinahusisha barabara ambazo zipo na zinajengwa na serikali.

Hivyo mifano yangu ni halisi kwa sababu vitu vyote vipo vinatokea.

Wewe mifano uliyotoaa sio halisi kwa sababu hakuna chanjo mabayo ilokuja watu wakachomwa wakafa kama unavyodai.

Na huko ndio kutoa mifano ambayo haijawahi kutokea(mifano feki a.k.a mifano ambayo sio halisi)

Kwa hiyo maana ya uhalisia hapa ni kwamba iww kweli kitu kipo na kimewahi kutokea.


sio wote wataitumia kwa matumizi sawa hiyo barabara lakini chanjo nyote mnaochanjwa ni sawa nadhani kwa kila kitu
Kila anayepata ajali barabarani lazima awe anatumia barabara kwa lengo moja tu la kutoka sehemu moja kwenda nyingine ama kwa lugha nyepesi kusafiri.

Sio rahisi wewe kutuambia kwamba wanaopata ajali wanatumia barabara kwa matumizi tofauti,sio kweli.

Wanaopata ajali wote wanatumia barabara kwa lengo moja tu la kutoka sehemu moja kwenda nyingine,labda utuambie kila mtu analifikia lengo hilo kwa njia tofauti.

Na kitu kuwa na njia tofauti haina maana na lengo tofauti,unaweza kuwa na njia ishirini lakini lengo ni moja tu.

Hivyo point hii pia naomba kuiwakilisha kwako kwamba watumiaji wa barabara wanaopata ajali wote hutumia kwa lengo moja tu la kutoka sehemu moja kwenda ingine(au kusafiri)
chanjo nyote mnaochanjwa ni sawa nadhani kwa kila kitu
Sio kweli.

Kuna watu miili yao wana allergic reaction(aleji) wakiitumia baadhi ya dawa,na wengine hawana.
Kwa mfano huo tu watumiaji wa chanjo hawako sawa kwa kila kitu.
Wasiwasi wa sisi wananchi hadi kutoiamini serikali kwenye hili suala ni hiyo misimamo yake inayotia mashaka
Tatizo sio serikali bali tatizo ni nyie wananchi mumetiwa mashaka.
Walikua hawazitaki izo chanjo kabisa na kashfa kibao tena mpaka viongozi wa kwenye kada ya afya,
Hii sio hoja ya kukataa chanjo kwa sababu mfano tu wakati wa magufuli watu walikuwa wanasifia sana serikali bila kukosoa.

Lakini watu wale wale baadhi yao sasa hivi wanakosoa serikali.

Kama kweli wanayokosoa ni ya kweli tunayachukua,hatuwezi kukataa wanayoyakosoa kwa kigezo cha kuwa eti mwanzo walisema tofauti.

Hivyo kipimo sio kigeugeu bali kipimo ni nini anasema huyo mtu.wewe mwache ageuke geuke awe na ndimi mbili lakini hoja ya msingi tuangalie anasema nini.
leo hii wanaleta chanjo na kusema usign kabisaa kua ukipata side effects wao hawahusiki
Nakuuliza tena ni matibabu gani katika afya ambayo serikali ilisema kwamba itahusika na side effects ambazo mgonjwa atazipata baada ya kutibiwa ?

Lete ushahidi wa hayo matibabu,pengine ukawa unakataa jina tu lakini maana ni ile ile.
chanjo sio upasuaji.
Yote ni taratibu za kimatibabu.
We ushawahi kwenda hospitali ukatibiwa na kusain form kama ile??
Wanaoenda kufanyiwa upasuaji lazima wajaze fomu ya kuhifadhi kumbukumbu ya ridhaa zao kwamba wamekubali wenyewe.

Jambo hili ni maarufu sana hata kama sijawahi kufanya upasuaji lakini lipo wazi.

Au wale wanaofanyiwa amputation(kukatwa viungo) lazima watoe ridhaa wenyewe kwanza then ndo wafanyiwe.
 
Back
Top Bottom