Hoja zimeisha, Watu wataisha, Tutajadili nini tena?

Pope

Senior Member
Dec 3, 2007
117
0
Ilinichukua Muda mrefu sana kuamua kujiunga nilikuwa nasita nikiona jinsi watu wanavyokata hoja kwa NGUVU ZA HOJA na kujibu hoja kwa hoja, na ndivyo nilivyopokelewa nilipotupa karata yangu ya kwanza tuu.

Nikitoka kwenye mishe mishe nitaangalia Jambo Forum kwanza ndio niangalie kwingine, magazeti nk.

Lakini kwa kipindi cha siku za karibuni naona hoja za msingi zinakwisha na ilobaki tumejitenga kiitikadi na kiimani zaidi.
Siasa za majimbo!!! Watu wana Copy kutoka kwenye magazeti na ku Paste hapa wakati wa kwenye magazeti ndio walikuwa wana Copy hapa na kupaste kule!!

Sio nia yangu kuyasema haya lakini unajisikiaje unapofungua ukurasa na kuangalia Topic na kukuta huoni ambayo inahitaji mchango wako kama MTANZANIA ila zipo nyingi zinazohitaji mchango wako kama Mwanachama, either kutetea CCM au CAHDEMA nk, au utetee UKRISTU au UISLAM!!

Hatari ya hii ni kuwa unajikuta unawajibuka KUTETEA UJINGA HATA KAMA UNAJUA HUU NI UJINGA kwa kuwa ni suala la imani ambapo kila mmoja ana amini upande wake unastahili zaidi ya mwenzie.

Sasa kama hoja zimeisha (SIAMINI NA SITAKI KUKUBALI KAMA ZIMEISHA) na tumehamia kumu attack Mtu mmoja mmoja (Individuals) naimani hawa wanaweza kuisha.... Tutajadili nini?

Wabillah Tawfiq
 
Ije hoja za kitaifa si kibinafsi!!

hata wewe waweza leta si lazima ziletwe na wengine. sote ni wanachama wa jamvi hili na sote tuna haki ilio sawa ya kusoma kuchangia na kuanzisha mijadala mipya kwa mujibu wa tuonavyo
 
Back
Top Bottom