Hoja za Wapinga Muungano hazijibiwi kwa risasi, virungu au mikwara! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja za Wapinga Muungano hazijibiwi kwa risasi, virungu au mikwara!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 2, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tawala zote duniani ambazo zimeshindwa kuwajibu wakosoaji wake mara zote zimegeukia kutumia nguvu kuzima hoja dhidi yao. Hili ni kweli na tumeliona Syria, kama tulivyoliona Misri; tumeliona Georgia kama ilivyo Russia; tumeliona Libya kama tulivyoliona Uchina. Mara nyingi watawala wanaposhindwa hoja wao hutumia risasi kama siyo virungu na pingu.

  Hoja za wapinga Muungano zimekuwa wazi kwa muda mrefu;hakuna jambo linalosemwa leo ambalo kwa mtu yeyote anayefuatilia siasa za Tanzania anaweza kushangazwa kwamba ni ngeni. Siyo hoja ya mafuta wala siyo hoja ya Utanganyika, siyo hoja ya kunyanyaswa wala hoja ya kubanwa zote hizi ni hoja zilizodumu kwa takribani miongo mitano sasa. Hakuna jipya.

  Bahati mbaya sana, wakati wa Mwalimu hoja hizi zilijibiwa kwa kutumia nguvu ya hoja. Kwa kuzichukua hoja zinazotolewa na kuzikata vipande vipande na kuzifunua kwa kuonesha udhaifu wake. Na hii ndio sababu ya mwalimu Nyerere kuamua mara mbili kujibu hoja za wapinga Muungano bila kulazimika kuitisha matumizi ya nguvu. Ukisoma kitabu cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania utaona jinsi hoja za Muungano zilivyojibiwa; na ukirejea ile hotuba ya Juni 14, 1995 Kilimanjaro hoteli utaona kuwa Nyerere aliweza kuzichambua hoja zote hizi kwa kutumia mantiki na hadi leo hakuna mtu ambaye ameweza kujitokeza kuonesha udhaifu wa hoja hizo - isipokuwa mashambulizi binafsi (ad hominem) dhidi ya nafsi ya Nyerere.

  Leo hii tunashuhudia viongozi walioshindwa - bara na visiwani - wakitumia nguvu ya risasi, pingu na vurungu kujaribu kupangua hoja za wapinga MUungano. Bahati mbaya sana hakuna risasi, kirungu au pingu iliyowahi kujibu hoja! Kwa kushindwa kusimama na kuzijibu hoja hizi moja baada ya nyingine watawala hawa wanawapa na niseme wamewapa nguvu wapinga Muungano.

  Kwa muda mrefu baadhi yetu tumekuwa tukiutetea Muungano kwa kuonesha udhaifu wa hoja za wapinga Muungano lakini sasa na sisi wengine tumefikia kikomo. Kwanini sisi tusio viongozi na watawala tusimame kuutetea Muungano wakati mamia ya wabunge walioapa kuulinda Muungano huu wakila kuku na kujipepea huku wakinywa vinywaji vikali? Kwanini, sisi watu wa kawaida ambao hatulipwi hata senti moja ya Muungano kusimama na kutetea Muungano wakati wapo watu ambao walipita huku wengine wakipiga magoti kuomba uongozi wa JMT?


  Inawezekana vipi leo watu wanatukuzwa ati ni "viongozi vijana" na kuwa "wamesoma" lakini wameshindwa kusimama na kujenga hoja za kuutetea Muungano huku wakipinga hoja dhaifu zinazotolewa dhidi ya Muungano? Ukweli ni kuwa Muungano ulipofika sasa hauwezi kuteteeka na hauna mtetezi. Kikwete hawezi kujenga hoja ya kuutetea wala Shein - kama alivyozungumza juzi- hana ujasiri wala uwezo wa kuutetea Muungano. Vuai hawezi wala Seif hawezi kuutetea; siyo Makinda wala Pinda na siyo Kificho wala Mkuchika wanaoweza kuutetea Muungano. Hakuna mbunge hata mmoja ambaye anaweza kusimama na kujenga hoja ya kuutetea Muungano au kuwajibu wengine zaidi ya wabunge nao kuchochea tu hoja za kwanini huu Muungano hauteteeki!

  Je wakati umefika wa kuanza kusema:

  Farewell Zanzibar, Goodbye Muungano?
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kuvunjika kwa muungano si salama kwa Tanganyika na Zanzibar.
   
 3. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Mkuu MMJ,

  Hoja ikiwasilishwa kwa hoja itajibiwa kwa hoja.Lakini hoja ikiwasilishwa kwa uvunjifu wa amani itajibiwa kwa mkono wa chuma.
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  MKJJ,

  Thanks for bringing this again, maana si mara ya kwanza kuandika haya.

  Kwa kweli ukiangalia zile you tube video za uamsho utama Ia kucheka tu! Kwani Wana uamsho wanatumia tu mwanya wa habari kutowafikia wazanzibari wengi kwa sababu nyingi TU zilizo ndani na nje ya uwezo wao ku Aini uhalisia wa maisha ya sasa! Lakini uamsho wamejua na wanatumia udhaifu na om we la uongozi katika serikali zetu kueneza propaganda zao. Hakika wapinga muungano wote ukiwaleta mezani kwa kujadili hoja kwa hoja, mwisho wa siku utagundua hawana hoja, zaidi ya kero zilizopo kwa miongo kumi ya taifa.

  Sijui ni "incompetency" ndani ya serikali, kwangu Mimi Binafsi sielewi ni kwa nini CCM inazuia kujadiliwa kwa muungano kwa uwazi, labda imi ni mmoja wa Watu misi jua yalifanyika ndani yamuungano. Naungan mkono na ninasema kama tumeshindwa kujadili aina ya muungano na modality, we should let them go, of course baada ya makubaliano kulinda yaliyotokana ndani ya miaka 47 ya muungano!
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sasa kama mwenyekiti hoja amegundua kwa makusudi hutaki kumsikiliza?
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, kweli umetetea Muungano na kuteta kuhusu Muungano kwa muda mrefu.
  Nini kimekufanya ukate tamaa mida hii?

  Kwa nini hutoi rai ya kuwa Muungano ujadiliwe kwa uwazi na kwa upana wake. Sijaona mada yako yenye kutoa uzito wa kuwa na mjadala wa Muungano kwa uwazi na kwa upana wake.

  Nakushauri uandike mada moja yenye kutaka mjadala wa Muungano uingizwe kwenye kazi ya Tume ya kukusanya maoni juu ya Katiba mpya kuliko kuandika hizi mada za kutaka Muungano uvunjike. Mada zako za hivi karibuni zinaonesha unakurupuka zaidi kuliko kufuatilia matukio, kujiridhisha na ukweli wa uyasikiayo na kuyafanyia udadisi.

  Halafu kuna mdau ametoa rai katika uzi huu https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/270856-hati-za-muungano-ndio-hizi-2.html#post3971657. Rai hii kama itatekelezwa unafikiri haiwezi kuokoa "tunu " yetu. Muungano wa aina ya kipekee duniani?

  It is not yet time to say " Farewell Zanzibar, Good bye Muungano"

  Bado tuna muda kama tuna nia njema kuukarabati Muungano, lulu yetu ili utoe mvuto na faida kwa pande zote za jamhuri ya muungano. Kero zinatatulika, kinachokosekana ni "viongozi" wa kutatua kero za Muungano. Hili linafanya kuwepo/kuzindua mjadala wa wazi na mpana juu ya Muungano kwa wananchi kuwa na maana zaidi kuliko wakati wowote ule.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Tanganyika itakuwa salama tu hili halina shaka; swali ni je Zanzibar itakuwa salama?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Ngoja niseme hivi; mimi binafsi nimeukataa mchakato huu wa Katiba Mpya na kwa kweli nilisema siwezi kuushiriki kwa sababu umepoka madaraka ya wananchi. Wenye kazi ni wale ambao tayari wamekubali kuwa ni halali halafu wanalalamika ati kwa nini muungano na mambo mengine yamekatazwa kujadiliwa!
   
 9. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tanganyika haitakuwa salama kwa sababu:
  1. Wazanzibar wanataka kugawana jehsi la Tanzania nusu kwa nusu (sio wanajeshi bali mali na vifaa vya kijeshi). Jeshi tulilonalo kulicut down into 1/2 si salama kwa Taifa letu.
  2. Wazanzibar wanataka kugawana hazina ya BoT nusu kwa nusu. Katika kipindi kigumu cha kifedha tulichonacho kucut down hazina 1/2 si salama kwa Taifa letu.
  3. Wazanzibar wanataka all immovable assets of the Union Government zithaminishwe na kugwanywa nusu. Net payment ifanyike kwa yule aliye nazo chache. Mfano, nyumba ya spika imejengwa hivi karibuni kwa thamani ya sh. bil 1.5, hapa wanataka tuwalipe milion 750. Sasa the same ifanyike katika mali zote including barabara!
  Hii formular italeta mgogoro mkubwa sana na Muungano utavunjika katika mazingira ya kinyongo, hasahasa kwa upande wa Zanzibar kuwa wamedhurumiwa na wa bara. Hii itasababisha tuwe na jirani mwenye chuki na sisi na jeshi lenye nguvu. Hii si salama kwa Taifa letu.
  4. Viongozi wa juu wa Tanzania wanajua siri ZOTE za Tanganyika lakini kuna siri za Zanzibar ambazo watanganyika hawazijui. Viongozi hao wanaweza kuamua kuisubotage Tanganyika, jambo ambalo si salama kwa Tanganyika.

  List ni ndefu, ila ngoja niishie hapa kwa kusema kuwa kuvunja Muungano kutaleta keri kubwa zaidi kuliko kero zilizopo za Muungano. Ni vyema tukatumia jitihada zaidi kuuboresha Muungano kuliko kufikiria kuuvunja na kuziweka Tanganyika na Zanzibar katika hali isiyo salama.
   
 10. B

  Bull JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muamsho na beyond kuvunja Muungano


  Kumekuwa na mipango ya makusudi liliyoandaliwa na Makanisa wakishirikana na Viongozi mafisadi kujaza Makanisa Zanzibar na kuhodhi ardhi ya Wazanzibari,

  Makanisa hayo yamejazana kama uyoga yakfuatiwa na Migahawa ya nyama ya Kiti moto, baa na umalay uliokithiri mitaani

  Zaidi ya 98% ya WaZanzibari ni Waislam, ukuwaji wa makanisa hauwiani kabisa na idadi ya wakiristo wahamiaji waliopandikizwa kwa ajili ya kuaribu mila na dasturi za Wazanzibar

  Kama Wazanzibari hamtokuwa makini, basi mtakuwa kama Wapalestina walivyo porwa ardhi yao na Waizraili
   
 11. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hao (Wazanzibari) watajiju!

  Mimi wamenikera sana. Wameharibia watu ratiba na mipango yao. Huku bara wanafanya mambo yao kwa raha mustarehe lakini Wabara huko Zanzibar hawana amani. Kariakoo wamejaa kibao wanafanya biashara na hakuna anayewabugudhi.

  Muungano na ufe na usalama wao watajiju wao wenyewe. I've just had it with them. Matukio ya wiki iliyopita kwangu were the final straw!!!!
   
Loading...