Hoja za wabunge wazalendo zitakuwa zipi?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,982
45,900
Wakati tukiwa karibu kabisa kuanza kwa vikao vya bunge, katika awamu ya Tano ya Uongozi wa Taifa hili.

Tutegemee hoja zipi mpya ukiachana na zile za kila siku tulizozizoea za escrow, richmond na nyingine kama hizo.

Nafikiri kwa mtazamo wangu ni vyema tukaanza kusikia hoja zinazomgusa mwananchi wa chini moja kwa moja, kama umuhimu wa afya bora maji safi na salama, elimu bora na ya uhakika, vile vile tukasikia na kuona hoja za kuhakikisha kua mikataba yote nyeti inayogusa rasilimali za taita hili ikipitiwa upya na kujadiliwa ili hatimae kuona kwamba taifa linanufaika nazo.

Ni wakati wa kuwa wabunifu na kuacha kudandia hoja zilizokwisha vuma na kuibua hoja zenye maslahi mapana ya wananchi wanyonge.
 
Mi nadhani takukuru kuvunjwa kisha kuundwa taasisi mpya,imepoteza imani kwa wananchi. Haiwezekani watu wanalipwa pesa nyingi bila tija kwa taifa.mimi si mchunguzi lakini rushwa halmashauri ni waziwazi,askar barabarani,mahakamani,kwenye mabenki mikopo mpaka umtoe afsa mikopo nk. Hii taasisi haiji na mipango yyte kuzuia rushwa Kama kusisitiza uwazi katika matumizi ya fedha za serikali. Ruzuku ya serikali mashuleni ilitakiwa waje na mkakati kuhakikisha wanazuia matumizi mabaya lakini wao waapi. Wananchi hatupeleki taarifa zetu kwao sababu hawana makali yoyote watu wanaina bora kuzituma kwa mawaziri sasa Huu ni utendaji gani
 
Ukaguzi wa mapato na matumizi ya vyama vya kisiasa kipindi cha uchaguzi mkuu uliofanyika october 2015
 
Napenda hoja zinazogusa jamii,mfano,bomoabomoa,ahadi ya serikali ya kuongeza pension ya mwez wastaafu na mifuko ya hifadhi ya jamii kushindwa kuwalipa wastaafu pension zao za mwez,ufisadi nhc,escrow,wakwepa kodi bandarin ni akina nani!n.k
 
Napenda nisikie hoja ya mwenda kwa miguu kwenye barabara zetu analindwaje. Barabara zetu zimekuwa si salama nyingi zimejaa bodaboda na zinapita kila sehemu,zimejengwa pasipo kufikiria pedestrians utakuta sehemu ya kutembea kuna mitaro iliyomikubwa isiyofunikwa, njia za service road kuna mama lishe wauza maua,wachoma mahindi yaani ni shaghalabaghala tuu. Health,environment and safety kwa pedestrians ni zero. Tunahitaji mamlaka husika kuona hili tatizo serikali za mitaa,Halmashauri na Tanroads. Kuna kona zimejazwa vibao vya matangazo mpaka hazionekani. Hii si sawa
 
Back
Top Bottom