Hoja za US na EU zitutafakarishe, zituimarishe na kutusongesha mbele imara zaidi kama taifa

Niseme mwanzo mwanzoni kuwa siandiki hapa katika namna ya kujibu, kutetea au kuunga mkono hoja zilizotolewa na Marekani (US) na Umoja wa Ulaya(EU) kuhusu mambo kadha wa kadha yanayodaiwa kufanyika hapa nchini. Hoja kubwa mbili za Marekani na Umoja wa Ulaya ni masuala ya demokrasia na haki za binaadamu.

Inajulikana kuwa Tanzania kama nchi yetu pendwa si nchi iliyojitenga. Tangu kupata uhuru, Tanzania imekuwa ikishirikiana na nchi nyinginezo za Afrika, Ulaya, Asia na Amerika katika Nyanja mbalimbali. Ndiyo maana Tanzania imekuwa kwenye Jumuiya mbalimbali za kimataifa kama Jumuiya ya Afrika Mashariki, SADC, Umoja wa Afrika (AU) na hata Umoja wa Mataifa (UN).

Pamoja na hilo, katika muktadha huo huo wa kushirikiana na nchi nyinginezo, Tanzania imeridhia na kutia saini mikataba mbalimbali ya kimataifa kuhusiana na mambo mbalimbali yakiwemo ya kidemokrasia na haki za binaadamu. Hivyo, kwa uelewa wangu wa mambo ya kimikataba, Tanzania ina wajibu wa kulinda na kutekeleza mikataba hiyo.

Nasema tena kuwa hoja zilizobebwa ba matamko ya Marekani na Umoja wa Ulaya zinapaswa kututafakarisha, kutuimariha na kutosongesha mbele tukiwa imara Zaidi kama Taifa. Kwakuwa Tanzania imekuwa ni kisiwa cha amani, utulivu, mshikamano na majibu ya busara kwa hoja zozote, hoja za Marekani na Umoja wa Ulaya hatupaswi kupelekeshwa nazo wala kuzipuuza.

Tanzania imejaliwa wabobezi wa kila sekta. Katika uga wa kidiplomasia, tunao wanadiplomasia waliobobea wakiongozwa na Balozi Augustine Mahiga ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje. Kama nchi, naamini, tuna maslahi, haki, wajibu na utamaduni wetu. Tuko makini katika kulinda, kutekeleza na kuendeleza mambo hayo ambayo ndiyo yanayoweka msingi wa taifa letu.

Nasisitiza, hoja za Marekani na Umoja wa Ulaya, kama washirika wetu wa maendeleo na mambo mengineyo, zitupe muda wa kutafakari na kuchukua hatua stahiki.
Pamoja na andiko zuri, umesahau kuwa andiko leo meandaliwa na mwanasheria wa kitanzania! Wewe ni Mwansheria nadhani ukirudia kusoma utang’amua. Kwa hali hii tlhatuwezi Katu kuwa kitu kimoja. Aidha unaona hapa JF walio wengi ni hater wa JPM hivyo mbaya wake ndiye rafiki mkubwa wao
 
Nasema tena kuwa hoja zilizobebwa ba matamko ya Marekani na Umoja wa Ulaya zinapaswa kututafakarisha, kutuimariha na kutosongesha mbele tukiwa imara Zaidi kama Taifa. Kwakuwa Tanzania imekuwa ni kisiwa cha amani, utulivu, mshikamano na majibu ya busara kwa hoja zozote, hoja za Marekani na Umoja wa Ulaya hatupaswi kupelekeshwa nazo wala kuzipuuza.


Kisiwa cha Amani! Hivi muda mwingine mnapoandika haya maneno kunakuwa na ushawi wa aina fulani ya Kilevi?.
Au mie nina taabu ya uelewa wa neno Amani?
Wangapi wameokotwa koko kwenye viroba?
Wangapi wanahofiwa kupotea huko pwani?
Je akilina alipata ajali ya Gari?
Je lissu ni majambazi?
Au Amani ina maana nyingine zaidi ya kutokupotea kwa uhai wa mtu au kumwagika wa Damu ?
 
Back
Top Bottom