Hoja za Tanzania na Burundi kuhusu Corona ni za kuigwa

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,152
10,862
Kwa upande wa Tanzania raisi wa nchi hiyo Makufuli alipokuwa akizindua shamba la miti kwao Chato alisema tuendelee kuchukua tahadhari ya ugonjwa lakini hakuna haja ya kujawa na hofu na kwamba watu wajifukize na hata akataja dawa zilizothibitishwa na mkemia mkuu kuua virusi na bakteria wote.Akaongeza kuwa tusikubali kuwa sehemu ya biashara za wengine.

Na kule Burundi waziri wa afya Thaddee Ndikumana amesema nchi yake haijaona umuhimu wa kuagizia chanjo za corona hasa kwa vile asilimia ya kupona kwa wale wanaopata ugonjwa huo ni zaidi ya 97.

Lazima mantiki hizo ziwatoe watu kwenye shida na msongo unaoleta maradhi mengine miilini.Si tunaona kasi ya kila mtengeneza chanjo anavyojitangaza mataifa mengine akitaka kuwahi soko.Na wako tayari mkupuo wa mwanzo kutoa sadaka ili kujichimbia sokoni.

Na kama watu wengi wamepata huo ugonjwa wakapona kirahisi na wengi bila kutumia dawa rasmi kutakuwa na umuhimu gani kupiga chanjo ambazo kwanza hazijajaribiwa vya kutosha na zipo fununu baadhi ya chanjo zina ajenda za siri katika miili ya watu.
 
Hizo chanjo wapeleke rwanda kenya na kwingine ila nchi zinazojitambua kama yetu hatuchezei miili yetu.
Sio kila siku iwe ni sisi tu kupokea.Safari hii kama wakileta zao kwanza tuziingize maabara na tuzifanyie majaribio upya tukiridhika basi tubadilishane na covidol zetu alizozizundua raisi karibuni kwenye hotuba yake. Hapana kutoa pesa.
 
Sio kila siku iwe ni sisi tu kupokea.Safari hii kama wakileta zao kwanza tuziingize maabara na tuzifanyie majaribio upya tukiridhika basi tubadilishane na covidol zetu alizozizundua raisi karibuni kwenye hotuba yake.Hapana kutoa pesa.
Kweli kabisa
 
Malaria inaua watu wengi saana kusini mwa jagwa la sahara na kuna dawa zipo ambazo zikipuliziwa malaria itakuwa historia Africa lkn WHO wanakatalia hiyo dawa isitumike hasa kwa sisi nchi maskini ukitumia unanyimwa msaada.

sasa hoja ya JPM ipo hapo why wanakatalia kutokomeza maralia kama wanatupenda kweli.
Sio sawa ,kila mtu ana haki ya kuishi kwa mujibu wa katiba.
 
Wanaokufa bila corona ni wengi kuliko asilimia hiyo,mbona hatuwezi kuwazuia wasife,

Mkuu tunazungumzia corona vs kinga ,swali lilikuwa kwamba hakuna umuhimu wa kuleta kinga kwa7bu wanaopona ni 97% ,mimi ndio nikauliza kwahiyo tuwaache tu hao 3% wafe?
 
Malaria inaua watu wengi saana kusini mwa jagwa la sahara na kuna dawa zipo ambazo zikipuliziwa malaria itakuwa historia Africa lkn WHO wanakatalia hiyo dawa isitumike hasa kwa sisi nchi maskini ukitumia unanyimwa msaada

sasa hoja ya JPM ipo hapo why wanakatalia kutokomeza maralia kama wanatupenda kweli

Unasikiliza Story za wanasiasa? Nani alikwambia kwamba Dawa ya kupuliza kutokomeza malaria Africa wamezuia? Weka link tusome!!
 
Si unaona basi.Haraka za nini kutafuta chanjo ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha na zina matokeo mchanganyiko kwa waliokwishakuzitumia.
Kuna watu humu JF siasa zime waharibu,wao kila kitu wapo pinga hata pasipo pingika.

Hizi chanjo hasa za UK na US zinapigiwa promo na kampuni zinazo zitengeneza na hamna chombo huru ambacho hakiegamii upande wowote,kilicho zipima hizi chanjo ili kujua ubora wake.

Yaani kwa kifupi chanjo za Corona zimekuwa kama mchezo wa kamari,kama msipokuwa makini kama taifa basi mtabet mpaka kwenye afya za raia,bila kujua effect zitakuwaje huko mbele.

Mimi sizani kama kuna haraka kwenye hizi chanjo,kama taifa na sisi tuchukue chanjo zote (za Uswizi,Canada,Iran,China,Russia,UK,US,Germany) tuzipime tujilizishe ubora wake ndio tuzitumie.Lkn hizi oya oya za kuigaiga zitatugharimu huko mbele.
 
Inajulikana hii covid ni aina ya mafua na ugonjwa huu haukuanza leo.Zipo kinga nyingi na rahisi katika vyakula na mimea ambavyo mtu akitumia anajikinga na maradhi mengi ya mafua.Hao wazungu wanajua hicho lakini kwanini wanaanza na kuhimiza watu kununua chanjo zao.Na kwanini na sisi waafrika hatuna juhudi za kujitetea kwa kutengeneza na kutangaza tiba zetu.Mpaka lini tutakuwa sehemu ya majaribio ya madawa na soko la makampuni ya dawa.
 
Ni mpaka pale wataalam wetu watapo amua kujikita kwenye taaluma zao, na kuachana na siasa.

Una kuta jitu ni professa wa masuala ya Nuclear lakini anandoto za kua mbunge na kuitekeleza taaluma yake.

Nb : Wasomi jikiteni kwenye taaluma zenu, achaneni na siasa.

Siamini mpaka leo Tanzania inaagiza vijiti vya kuchokonolea meno kutoka China?
Acheni hizo jamaa (wasomi)
 
Wataalamu na wasomi wetu hawana kitu zaidi ya maneno mengi Kama wamebobea ktk jambo fulani,,utawasikia maneno kama""

-- actually.
--my opinion
--of course.
--in the matter refact.
--by the way.

-- you know.
-- straight to the point.

Lakini ni zero kabisa...

Watu hata kibatari hawawezi kutengeneza..

Elimu ya kukariri maneno walioandika wazungu,,kwenye vitabu..

Ukiwakuta wanafafanuwa jambo ni kama wataalam kweli .

Kumbe bure kabisa.
 
Malaria inaua watu wengi saana kusini mwa jagwa la sahara na kuna dawa zipo ambazo zikipuliziwa malaria itakuwa historia Africa lkn WHO wanakatalia hiyo dawa isitumike hasa kwa sisi nchi maskini ukitumia unanyimwa msaada.

sasa hoja ya JPM ipo hapo why wanakatalia kutokomeza maralia kama wanatupenda kweli.
Dawa gani hio?

Naona kuna chanjo ya Malaria

Inajulikana hii covid ni aina ya mafua na ugonjwa huu haukuanza leo.Zipo kinga nyingi na rahisi katika vyakula na mimea ambavyo mtu akitumia anajikinga na maradhi mengi ya mafua.Hao wazungu wanajua hicho lakini kwanini wanaanza na kuhimiza watu kununua chanjo zao.Na kwanini na sisi waafrika hatuna juhudi za kujitetea kwa kutengeneza na kutangaza tiba zetu.Mpaka lini tutakuwa sehemu ya majaribio ya madawa na soko la makampuni ya dawa.
Hizo ni story tu kuwa eti covid ni mafua tu. Hayo mafua na hizo homa ni introduction tu. Mafua ya kawaida ata usipotumia dawa wala miti shamba yanaondoka. Hii covid inakwenda kuchokonoa mapafu na ikianza hio shughuli ya uchokonaji ndio shida inapoanza.

Nina jamaa yangu UK ameekwa ventilator miezi mitatu straight mpaka aliingia kwenya coma, walipoona anepata afueni wakaitoa kwa ajili ya mtu mwengine, hapo hapo wakamuona hawezi kupumua wakamrudishia. Madaktari wakamfanyia uchunguzi na kugundua kuwa hatoweza tena kupata pumzi hata moja kwa mapafu yake ilibidi wamkatishe mashine na amezikwa tayari.

Huu ugonjwa ukianza dalili ya mwanzo tu uanze kujitibu mapema ukiuachia bwerere ndio utaelewa kama huelewi. Unaambiwa ukifikia stage ya kuekewa ventilator na ukapona, basi mapafu yako tayari yashatoboka toboka na hio shida utakuwa nayo milele
 
Back
Top Bottom