Hoja za Profesa Palamagamba Kabudi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja za Profesa Palamagamba Kabudi...

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Ntambaswala, Jul 26, 2010.

 1. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wiki kama mbili zilizopita nilikuwa naangalia kipindi cha Simbeye pale TBC1, mmojawapo wa wazungumzaji alikuwa ni huyu Profesa. Kwa kweli nirifarijika sana jinsi huyu bwana alivokuwa akitetea maslahi ya watanzania (nchi) katika mchakato wa EAC na jinsi anavyoona mambo yanavyoharakishwa bila kutoa nafasi ya kudurusu kila hatua tunayomaliza. Hapa nampa heko Profesa ingawa tulitofautiana katika suala la mgombea binafsi(labda pia ni kutokana na ufahamu wangu mdogo kuhusu sheria)

  Huyu profesa ameonyesha kuwa yeye ni msomi yupo tayari kutetea kile anachokiamnini kwa kutumia hoja yakinifu na zenye mantiki. Nilifurahi zaidi kwa vile yeye ni mojawapo wa wawakilishi wa Tz katika majadiliano ya EAC.

  Katika kipindi hicho pia alikuwepo Dr Kamala, duu jamaa alishindwa kabisa kujenga hoja, kama huyu ndiye anakaa na akina Wetangula katika majadiliano basi Tz tujue hatuna mtu. Hoja zake siku zote ni dhaifu, hana sauti ya mamlaka, kiingereza chake ni finyu n.k. Hata ukilinganisha hoja zake na za profesa Kabudi ungedhani ni mtu wa mwenye shahada ya kwanza anajadiliana na Profesa wake....

  Kama nchi lazima tuwe tunateua mawaziri ambao wanaweza kujenga hoja za kueleweka, na pia ambao wanaweza kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza kwa ufasaha zaidi. yawezekana Kamala ana strenghths zake nyingi tu lakini katika hili la EAC anapwaya sana ni kama yeye ni mtu wa kuburuzwa na Wakenya na Waganda na yeye anafurahia sana hii intergration-sijui kwa maslahi gani. Angejua Watz wengi tuko skeptical na hii move asingekuwa anajenga hizo hoja anazojenga sasa kuwa EAC ina faida nyingi sana.
   
 2. bona

  bona JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  viongozi wa kitanzania wanadhan ni kushikilia au kutoa msimamo kwa kitu wengi wasichokitaka ili wapate umaarufu, na wanaigana kinachosikitisha zaidi, ntatoa mifano michache kwa ili, shamsa mwangunga aliongea kwa jeuri kusisitiza barabara ya makuyuni musoma kupitia serengeti lazima ijengwe kwani ni kati ya ahadi zao kwa watanzania eti ni ilani ya ccm, cha kujiuliza ahadi ngapi wamehaidi hawajetekelza? kwa nini wasianza na vile rahisi kama mahakama ya kadhi nk, benard membe ameshikilia suala la dual citizenship kana kwamba ndio muarobaini pekee wa matatizo yetu watanzania, suala la viongozi kushikilia vitu vinavyopingwa na wengi linashangaza sana! naona ni fashion hasa wenye uelewa mdogo kama huyu kamala, membe, mwangunga na wengineo
   
 3. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni pamoja na kijeba Mwapachu, wote akili nusu. Hawajui nchi jirani zina hila dhidi ya nchi hii.
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Prof. Kabudi ni msomi wa kweli, hilo halina ubishi, tatizolangu kwake, ni kama la Prof. Mwakiembe, ni makada wa chama cha Mapinduzi hawa, hivyo kwenye jambo lolote lenye maslahi ya CCM, wataweka kwanza maslahi ya CCM yakifuatiwa na maslahi ya Serikali ya CCM mbele ndipo yaje maslahi ya watu/haki ya kweli.

  Hoja zake kwenye suala la mgombea binafsi, zilinimaliza kabisa imani yangu kwake, ila heshima yangu kwake kama msomi wa sheria aliyebobea, inabaki pale pale.

  Niliwahi kumshauri Simbeye na Prespective yake, wakimaliza kurekodi hicho kipindi cha Kiingereza ambacho ni kwa maslahi ya wageni na the elite group, warekodi kingine cha Kiswahili kwa maslahi ya Wanzania wa kawaida kina sisi.
   
 5. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  True that mimi naamini ya kuwa watanzania wengi hawataweza kuelimishwa ikiwa mambo yanayowahusu ,yakizungumzwa kwa kingereza,TBC wangekirekodi then wakiedit ikiwezekana kiekewe subtitle ya kiswahili ili wadau wasome. na kuelewa.
   
 6. n

  newazz JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Mkuu alisema nini Prof. Kabudi cha kutetea kutoingia kwenye Jumuia na hoja yake ikakukuna?

  Ninavyojua mimi, kuingia kwenye jumuia ya afrika mashariki ni mchakato ambao serikali zote wameshaafiki.

  Tofauti ni namna ya kutekeleza makubaliano.

  Hilo litakuwa gumu sana , kwani Tanzania tuna tatizo kubwa sana la haki za kiraia , zinazotokana na kuchezewa katiba ya Tanzania.
   
 7. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Palamagamba Kabudi ni msomi wa siku nyingi.Tunaomfahamu twajua kuwa kile ni kichwa kilichinolewa kwa usomi na fikra.
  Si ajabu kwamba ni Profesa.
  "Dr" Kamala ni kati ya wale jamaa ambao wamepitia mlango wanaoufahamu wenyewe kuingia kwenye "usomi".
  Matokeo yake tunayaona , tunapata wasomi wanasiasa ambao hata kujieleza kile wanachotakiwa kukifahamu , hawajui.
  Achlia mbali kiingereza cha kuunga unga.
  Pole mama yangu Tanzania
   
 8. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Well well well. No doubt kuwa Kabudi ni kichwa lakini ananiacha hoi sana anpoamua kuwa mmoja kati ya wale maprofesa ambao kwa makusudi kabisa wameamua kukiss ass na kuuza utu wao kwa kusifia na kusuport wasiyotakiwa kufanya hivyo.
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Huh!
  No Comment sir
   
 10. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kuna thread moja kule kwenye jukwaa la Siasa ilitoa sababu ya prof. Kabudi kung'ang'ania mambo ya CCM. Ilitajwa kwamba ni mtu aliyeajiliwa na usalama wa Taifa tangu miaka ya 70.

  Wengi ktk hao usalama bado wanadhani kazi yao ni kuilinda CCM.
   
 11. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Udaktari wake nae ameupatia HAPA?
   
 12. Companero

  Companero Platinum Member

  #12
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huyu si ndiye yule Rafiki wa Korti/Mahakama ambaye hoja zake zilitumiwa kuzima Ugombea Binafsi?
   
 13. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa, hivi tukikutaka wewe ujenge hoja tofauti za Prof. Palamagamba kuhusu mgombea binafsi unaweza kutuambiaje kiufasaha hasa? Kama msomi amabye upo tayari kutetea kile anachokiamnini kwa kutumia hoja yakinifu na zenye mantiki. Kwanza tupe concept wewe unavyoelewa, kisheria maana ya mgombea binafsi then Tafadhali weka jamvini mengine....
   
 14. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wakuu wangu tusifike mahali tunamlaumu kila mtu (kama Prof. K). mwisho wa siku tutaanza kulaumiana wenyewe na hatutafika popote. Prof. alitoa hoja kulingana na mwelekeo wa fikra zake tuziheshimu na tutoe fikra zetu. sioni mantiki ya ku link kila kitu na au CCM au UPINZANI
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Baada ya kumaliza High School pale Milambo Secondary School na HGL mwishoni mwa miaka ya sabini (nadhani 1978 au 79), Paramagamba aliajiliwa kama mwandishi wa habari nadhani wa Daily News kwa miaka kama miwili au mitatu hivi kabla hajaenda kusomea LLB hapo UDSM ambapo alipata division ya juu yenye GPA zaidi ya 3.8 out of 5 akaajiriwa kama TA katika kitivo cha sheria (wakati huo), kazi ambayo ameifanya kuanzia katikati na mwishoni mwa miaka ya themanini hadi leo. Kwa hiyo ni vigumu sana kuniamanisha kuwa anatumikia usalama wa taifa hasa ukizingatia kuwa kipindi alichomaliza chuo kikuu kulikuwa na mabadiliko ya uongozi kati ya Nyerere na Mwinyi ambapo usalama wa taifa walioajiriwa na Opiyo waliondolowa wote na kujazwa wengine wapya chini ya Lupia.

  Mahakimu wale pamoja na yeye walitumia kifungu hafifu sana cha katiba ambacho kinapingana na Katiba yenyewe. Kuna kifungu fulani katika katiba kichoinyang'anya mahakama mamlaka ya kuamua kesi zinazohusu mambo ya aina hiyo. Kilichotakiwa na mahakama ni kusema vifungu vyote viwili siyo constitutional kwa sababu vinapingana na lengo kubwa na katiba yenywewe.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
   
 17. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Udaktari wa kama Kamala na wenzake unapatikana kwa USD 180 tu hapa www.instantdegrees.com
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Lol!

  Hata mimi niliangalia hiki kipindi cha TBC1. Huyu Prof. ni mahiri kweli wa kujieleza na kutetea maslahi ya Tz ktk EAC!

  Inafaa awe waziri ktk Wizara hii ya EAC achukue nafasi ya Kamara!

  Call a spade a spade na siyo a big spoon!
   
 19. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Jul 28, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
   
Loading...