Hoja za msingi za kwanini Tanzania inahitaji Sheria ya Ulinzi wa Data

Status
Not open for further replies.

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1582627733782.png

Ingawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kupitia Ibara ya 16 imeweka bayana umuhimu na Haki ya Faragha, mpaka sasa Tanzania haina Sheria inayosimamia haki hiyo. Hoja zifuatazo zinatumiwa na wadau kuelezea umuhimu wa sheria hiyo

1582625725658.png

Sheria hii itahakikisha Haki ya Faragha inasimamiwa na kutekelezwa kwa vitengo kama ilivyoandikwa kwenye #Katiba ya Tanzania.

Maendeleo la Teknolojia yanaweza kuathiri ulinzi wa Data Binafsi za Watu hivyo Sheria hii itawalinda watu dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza.

Sheria itatoa muongozo na majibu kuhusu ufuatiliwaji wa mawasiliano ya watu ambao uko kinyume cha taratibu, sheria na usio halali.

Uwepo wa Sheria hii utarahisisha usimamizi wa maamuzi yanayotolewa kuhusu Data za Watu pamoja na matumizi ya taarifa za watu kwenye matangazo.

Sheria itasaidia kuundwa kwa Kanuni za #UlinziWaData


======

The right to protection of personal data is derived from the individual right to privacy. Tanzania has had a difficult history in the protection of the right to privacy; from evading its inclusion in the Bill of Rights after her independence to unsuccessful enactment of the right to privacy and data protection in the draft Freedom of Information Bill in 2006.

In 2013, Tanzania decided to reform her framework for the protection of personal data and individual privacy. This chapter explores the background to the protection of privacy in Tanzania and the recent reforms.

The chapter also takes a look at social attitude to privacy and the legal framework that supports the individual claims and protection to one’s privacy in Tanzania. This overview provides for the background upon which the present Draft Personal Data Protection Bill emanates.

This is followed by a textual analysis of the Draft Bill which describes the weaknesses of the Draft Bills from simply omitting one condition for the processing and adding a condition to Commissioner’s duties which are not usually found in data protection codes.
 
Mawazo yako mkuu ni konki sana na kwa kuwa Katiba inatambua hili nadhani Sheria haina namna ni lazima ije tu.

Ila swali langu ni kwamba what do we do ili Sheria hii ipatikane? Tunaanzaje hapa?
 
Sheria ya ulinzi wa data inahitajika sana hasa katika kipindi hiki ambacho matumizi ya kimtandao yamekuwa makubwa sana.

Hivyo ni bora Serikali ikaona kuwa ni muhimu sana na kuwahisha sheria hii ili kuweza kuweka uhuru wa faragha ya mtu kuzingatiwa bila kuingiliwa na mtu au mamlaka Fulani.
 
Mkuu hongera kwa uzi murua kabisa. Kwakweli haki ya falagha ni jambo la msingi sana kwa Watanzania wote.

Haki hii imekuwa haiongelewi sana na wadau wengi kwa sababu watu hawana ufahamu wa kutosha juu ya umuhimu wa falagha na kuzuia mawasiliano yao kuingiliwa na watu wengine.

Jambo la kusikitisha kutokana na ukosefu wa haki hii hata baadhi ya viongozi fulani walijikuta wanaingiliwa falagha zao za kimawasiliano waziwazi na wakashindwa cha kufanya.

Nadhani wanaharakati wa haki za kimtandao wanapaswa kutumia nguvu ya ziada kuhakikisha Watanzania wengi wanajua umuhimu wa haki hii ya msingi, huenda ikawasaidia kuanza kuidai na kuipigania au hata kutumia mbinuza kiteknolojia kulinda data zao.
 
Kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa sekta ya sayansi na teknolojia, Serikali nayo inatakiwa kuandaa Sheria ambazo zitatoa muongozo kwa wananchi kutumia vyema teknolojia pasipo kuvunja taratibu za nchi.

Bila uwepo wa Sheria hii watu wataendelea kutumia Mtandao watakavyo hata kama wanamkandamiza au kumuumiza mwingine.

Sheria hii ni muhimu
 
Ni muhimu kwa sheria kama hii lakini neno Data na Faragha, ipewe tafsiri pana ili kusiwe na escape route
 
Sheria zinahitaji kusasishwa ili kuendana na wakati ambao unabadilika kila siku kutokana na ukuaji wa teknolojia. Tangu mtandao uliposhika hatamu, watu wamekuwa waki-sharei zaidi habari zao za kibinafsi mtandaoni. Katika nchi nyingi, sheria za faragha zipo na zinabaki muhimu kusaidia kulinda habari za watu na haki za binadamu, lakini hazibadilishwa ili kuendana na changamoto za ulimwengu wa leo.

Kwa hapa fasi ya Bongo sheria ya Ulinzi wa Data ni muhimu sana kwa sababu ya matumizi makubwa ya mtandao. Katiba ya Jamhuri imeweka wazi kuhusu Haki ya Faragha hivyo sheria ikiwepo kabisa ambayo ni rafiki kwa nchi na isiyokinzana na matakwa ya kikatiba itakuwa ni hatua kubwa sana kwa nchi ili kulinda haki za raia.

Ugumu unakuja kwa namna ya kusukuma ili Serikali ione umuhimu wa jambo hili, binafsi naona kuna makusudi kabisa ya kuchelewesha jambo hili.
 
Mimi sina uelewa sana juu ya hili, hivyo ninajiuliza hivi:

Endapo Sheria ya Faragha ikitungwa, bado itaweza kuzuia mamlaka nyeti za Serikali kama vile TISS kuingilia faragha ya mtu? Na vipi kama ambaye faragha yake inaingiliwa, mamlaka hizo zina uhakika au zitaamua tu kum-label (hawashindwi) kama potential suspect kwenye suala zito linalodhaniwa kuhatarisha usalama wa taifa?

Does the Right to Privacy outweigh National Security?
Does National Security outweigh the Right to Privacy?
Do the two “weigh equally”?
 
Intanet, barua pepe na simu za mkononi ni njia kubwa za kuwasiliana kwa dunia ya sasa na mawasiliano haya yanatakiwa kuwepo bila ya mipaka. Pamoja na hayo intaneti huwezesha pia upelelezi usio na kikomo katika mawasiliano ya watu hasa kutoka kwa Serikali na mashirika ya simu

Kuna haja ya kuwa na sheria ya ulinzi wa data kwasababu siku hizi everyone who is using internet has something to lose pale itakapotokea compromise ya aina yoyote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom