Hoja za Mawakili wa Serikali dhidi ya Adamoo

Adamo ndio kamtaja Mzee Mbowe kumtumia ktk Ugaidi.
ndio maana anapapatua ili maelezo yake yasipokelewe, ila kazidisha uongo hadi unanuka!!
eti anadai hajala siku 10!! hiyo ni dalili ya mtu muongo! na mzushi!

IMG_20210930_170832_807.jpg
 
Ungekuwa na akili ungekuwa umetambua huu uzi unazungumzia hoja za Adamoo zinazobishaniwa. Utetezi upande mmoja na mashtaka upande mwingine.

Halipo neno Chadema au hata Dr. Slaa kwenye uzi huu.

Yote yaliyo hapa anayo Jaji na kayasikia yeyote aliyefuatilia.

Wapi nimekosea, kupunguza, kuongeza au hata kutia chumvi? Onyesha nitarekebisha.

Hoja ni humo. Kama huna hoja funga mdomo wako.

Huku siyo Telegram!
Usitumime nguvu kubwa kumwelimisha mpbavu ndugu it's a waste of effort, this guys are plain fools
 
Mawakili wa Serikali wanadai Adamoo alikamatwa kwa mujibu wa sheria na tena akatoa maelezo kwa kina Kingai kwa mujibu wa sheria na bila shinikizo. Hivyo wanaitaka mahakama kuyapokea maelezo hayo kama ushahidi wa kuaminika dhidi ya watuhumiwa kwenye shauri la msingi.

Adamoo kaeleza mwenyewe namna alivyokamatwa. Yaliyotokea Moshi, alivyojikuta Tazara, hadi polisi Mbweni.

Shahidi #2 wa utetezi kaeleza mazingira ya ukamatwaji. Kilichotokea Moshi, alivyojikuta Tazara hadi Mbweni.

Shahidi wa pili alimwona Adamoo akipelekwa kwenye kinyumba cha mateso Moshi. Alimsikia sauti ya zege akilia. Alimwona akikokotwa kurejeshwa mahabusu. Kama alivyohisi zamu yake ya mateso na vipigo ilifuata baada tu ya Adamoo kurejeshwa mahabusu.

Shahidi wa pili aliambiwa na mmoja wa watesi wao kuwa kipigo cha Adamoo kilikuwa kikali zaidi kuwa bahati yake yeye alipata mwokozi.

Aliporudishwa rumande kwake alisema na Adamoo ambapo Adamoo alijibu - Mikazo (code ya kijeshi kuwa kateswa sana).

Kabla ya safari ya Dar shahidi #2 alimwona Adamoo akikokotwa kuletwa kwenye gari.

Tazara, shahidi wa pili alimsikia akilia na kumwona na kujiridhisha kuwa alikuwa ni luteni Urio ambaye alikuwa naye akiteswa.

Njiani kwenda Mbweni Shahidi wa pili akigongwa gongwa kichwani kwa bastola aliambiwa na Inspekta Mahita kuwa asipokubaliana na yao watamtupa pia kama walivyomtupa Moses Lijenje.

Mbweni Shahidi #2 anasema yeye na bila shaka Adamoo hawakupata chakula chochote rasmi kwa siku 10.

Adamoo na Shahidi wa 2, kote Tazara na Mbweni waliandikishwa kwa majina tofauti na yao. Johnson John alikuwa Commando Ling'wenya shahidi #2.

Mashahidi wote hawa wanasema waliletewa maelezo wakatakiwa kuyasaini wakiwa kwenye vitisho.

Shahidi #3 wa utetezi mke wa Adamoo anasema nyumbani kulisachiwa akiwa hayupo na baadhi ya vitu vikachukuliwa. Yeye na wenzake walifika vituo kadhaa vya polisi kuwatafuta wenza wao kwa utambulisho wa majina yao bila mafanikio.

Mama Ling'wenya angejua vipi mumewe ni Johnson John kama ile chanjo ya yetu pendwa ya J&J?

Segerea, shahidi wa tatu alisikia askari magereza wakisema mumewe yaani Adamoo ni yule mtu kwenye kabati.

Alipokuja Adamoo alikuwa kadhoofu, macho yamemdumbukia, akichechemea, akiwa na makovu mapya mikononi.

Adamoo alimwambia shahidi wa tatu kuwa alikuwa kateswa na kupigwa sana Moshi.

Mashahidi wa serikali wameshindwa kuieleza mahakama ni kwa nini washitakiwa walipelekwa Mbweni Polisi.

Mawakili wa serikali hawakatai kuwapo mtu akiteswa Moshi. Wanatilia shaka kuwa Ling'wenya anaweza kuwa alisikia mtu mwingine.

Pamoja na kuwa waliomba kesi kuahirishwa kumsubiria shahidi wao #4 Jumanne, katika hali ya kushangaza pamoja na kuwa Jumanne alionekana kwenye viunga vya mahakama siku ya shauri, mawakili wa serikali waliamua ghafla kufunga sehemu yao ushahidi.

Macho yote sasa kwa Jaji. Akitupilia mbali pingamizi hili maana yake kakubaliana na upande mashtaka kuwa yote ilikuwa kwa mujibu wa PGO.

Yuko wapi Moses Lijenje?
hakuna ushahidi wa kuteswa hapo hizo ni porojo.
naamini mahakama haiwezi kukubali porojo zisizo na uthibitisho.
hizo ni POROJO za Adamoo.
hivi ulitegemea mke aseme tofauti dhidi ya mume wake?!! hamna kitu hapo!!
ushahidi wa mke kwa mume wake
 
hakuna ushahidi wa kuteswa hapo hizo ni porojo.
naamini mahakama haiwezi kukubali porojo zisizo na uthibitisho.
hizo ni POROJO za Adamoo.
hivi ulitegemea mke aseme tofauti dhidi ya mume wake?!! hamna kitu hapo!!
ushahidi wa mke kwa mume wake

Kwani wewe ulikuwepo kwenye sakata hilo la ukamataji na kupatikana kwa maelezo?

Aliyekamatwa na kuchukuliwa maelezo kaeleza sehemu yake. Waliomkamata wameeleza ya kwao.

Mashahidi walioona katika hatua mbalimbali wameeleza yao.

Mawakili wa Serikali wanadhani mtu angeweza kuiga sauti ya Adamoo Moshi kama Steve Nyerere tu. Wanadhani Ling'wenya aliona mtuhumiwa mwingine akiteswa kavaa kama Adamoo.

Mawakili wa Serikali wanadhani Ling'wenya alimfananisha mtu mwingine akiteswa siyo Adamoo.

Mawakili wa Serikali wanadhani hata mkewe Adamoo alimfananisha mumewe Segerea. Wanadhani pia hakuwa mkewe Adamoo kwani hakujua hata namba ya mumewe kichwani.

Wanakazia uelewa wao huo kwani hakuwa hata na cheti cha ndoa mahakamani.

Hiiiiii bagosha!

Jaji kasema isiwe zaidi ya page 5 maana yote naye anayo.

Ila zandrano yuko wapi Lijenje?
 
Jwtz we wako wapi mpaka kamandoo mwenzao apotee kienyeji hivyo!Shida nchi siasa zimeingia mpaka jeshini Hilo ndo tatizo.Komandoo anateswa kienyeji kias hicho kweli jaman?
 
Siku ya kwanza Adamoo alisema alipigwa na Mahita ,pia alipata vitisho kutoka kwa Kingai. Siku ya pili anahojiwa na Wakili was serikali akasema hakupigwa. Hii inaonyesha aliporudi magereza alipapata vitisho au alirubuniwa ili akubali. Hii inadhirisha hii kesi ni ya hila.
 
Siku ya kwanza Adamoo alisema alipigwa na Mahita ,pia alipata vitisho kutoka kwa Kingai. Siku ya pili anahojiwa na Wakili was serikali akasema hakupigwa. Hii inaonyesha aliporudi magereza alipapata vitisho au alirubuniwa ili akubali. Hii inadhirisha hii kesi ni ya hila.

Vipigo vilikuwa Moshi akikamatwa na alipopelekwa Central.

Kutokea huko vingine vikawa kukumbushana nini kitakuwa isipokuwa nini.

Adamoo na Ling'wenya wamekuwa wazi kwenye hayo.

Mnyonge mnyongeni.
 
watajuta walio kuwa wanapanga mipango haramu ya kuchafua Amani ya nchi.
vipo vya kuchezea kama kitambi chako, kidevu n.k lkn kamwe usijaribu kuchezea Amani ya nchi.
Amani ya nchi ni zaidi ya mboni ya jicho.
Ila ww ni mtu au robort!? maana kwa mtu hawz andika haya matapsh.

sjui kwann Baba yako hakuvaa salama, na kama alkosa salama angtumia hata soft tu nafkr ingekinga kuleta hii takataka.
katuletea hasara watz
hata kama unalpwa kwa kuandka huu uharam wako, kuna mengne ungkuwa unaona aibu moyo ungkuwa unakusta na sio huu upumbavu ulio dhihrsha hapa https://jamii.app/JFUserGuide
 
Adamo ndio kamtaja Mzee Mbowe kumtumia ktk Ugaidi.
ndio maana anapapatua ili maelezo yake yasipokelewe, ila kazidisha uongo hadi unanuka!!
eti anadai hajala siku 10!! hiyo ni dalili ya mtu muongo! na mzushi!
Kwenye maelezo yapi? Aliyaandika wakati akimkaza mamako au?
 
Back
Top Bottom