Hoja za Lula-Maridhiano ya Zanzibar yatokane na kanuni

- Hapana ndugu yangu, wewe weka vitu hapa wengi tunakusoma sana, ila acha personal na muandishi maana inapunguza utamu wa dataz nyingi unazozitoa, tupingane kwa hoja tu mkuu unazo hoja nzito sana ila unaharibu kidogo tu na personal, ushauri wangu kidogo tu na wa bure!

Respect.

FMEs!

Haina noma...thanks
 
Lula inspirations inataka kujua nini kiko nyuma ya pazia la maridhiano.Auliza ni kwanini sasa na sio zamani au baada ya uchaguzi.Sio kwamba yamefanyika na tujaribu kuyapa nafasi kama yatafanikiwa?

...Sasa wazenj wanasema lets give this attempt a shot, yeye anaona bora tuache tusubirie hadi uchaguzi upite.Naona kama amesahau kama tatizo lenyewe limeanzishwa na uchaguzi....sasa kupata uchaguzi mwengine si ndio maafa zaidi???...i guess he doesnt even care about that :D

Makala hiyo ya kijana akijadili masuala ya Zenj.

Kuna nini nyuma ya pazia la mariadhiano ya Seif, Karume?
NIANZE kwa kumpongeza mwanasafu Lula wa Ndali Mwananzela. Nampongeza kwa kutekeleza vyema jukumu la kuhabarisha na kuelimisha umma wa Watanzania kupitia makala zake.
Lazima nikiri kwamba mimi ni msomaji mzuri wa makala zake kupitia gazeti la Raia Mwema. Licha ya kuwa kwangu nje ya nchi kwa sasa, hiyo hainifanyi nisifuatilie kinachoendelea huko nyumbani.
Nimevutika sana na hali ya kisiasa inayojitokeza kwa sasa huko nyumbani; hususani sehemu za Visiwani. Hata hivyo kuvutika kwangu si kwa uzuri; bali kwa mshawasha wa kujua siri ya hili jambo linalopigiwa kelele na kushupaliwa na karibu watu wengi; hasa wale wenye kujiita ‘Wazanzibari wenye kuijua historia yao’.
Nataka kukubaliana na Bw. Lula kuhusu suala moja; nalo ni kuwa mimi kuijua au kutokuijua historia ya Zanzibar, niwe au nisiwe Mzanzibari (Rejea Raia Mwema Na. 118), hakunifungi mdomo kuacha kuzungumzia ninachokiona kinaendelea huko Visiwani.

Hoja za hao wanaomsakama wakidai kwamba wao ndiyo pekee wanaoijua historia ya Zanzibar, ni hoja za watu wenye jazba ambao hufikiri kwa mdomo badala ya ubongo!
Suala linalotushtua tulio wengi; ni nini hasa kipo nyuma ya pazia la hayo yanayoitwa maridhiano ya hawa mabwana wawili – Seif na Karume? Ni kwa heri ya Zanzibari kweli kweli au kuna lililojificha nyuma ya pazia kwa manufaa yao wawili?

Iweje maridhiano ya wawili hao yaje leo tunapokaribia uchaguzi mkuu? Ni kipi kilichobadilika ambacho kilikuwa kinakwamisha haya makubaliano (sijui niyaite maridhiano au mapatano) yasifanyike huko nyuma pamoja na vikao na mijadala kadhaa kufanyika?
Kwa maswali yangu haya simaanishi kuwa napingana na hayo wanayoyaita ‘maridhiano au mapatano’; bali najaribu kujiuliza nia yake hasa. Ninachokiona ni kuwa, kuna ukungu mkubwa katika hayo yanayoitwa maridhiano. Na mbaya zaidi, ukungu huu umewafunika macho hao wanaojiita ‘Wazanzibari wenye kuijua historia yao’ kiasi kwamba hawataki hata kuhoji kinachoendelea, na badala yake wanakurupuka na kushupalia tu kwa ushabiki.

Inapotokea wengine kuuliza maswali kama haya ninayojiuliza ndipo tunapoonekana watu wa Tanzania Bara hatuitakii mema Zanzibar, na kwamba tunafurahia wao waendelee kuvurugana.
Ninachojiuliza ni kuwa; hivi hatuwezi kuzungumzia mapatano ya Zanzibar bila watu kuleta hoja za kuuvunja Muungano? Hivi dawa ya kutufunga midomo tunaohoji siri ya hayo makubaliano au maridhiano ya Seif na Karume ni kututishia kuvunja Muungano?

Hii inakuwa kama mwanamke mwenye gubu – usimuulize swali lolote, ukimuuliza tu atakutishia kukuacha. Huu ni utoto. Swali hupewa jibu la hoja, na si vinginevyo.
Kitu ambacho wote mnapaswa kukumbuka ni kwamba vijana wengi hatukuwepo wakati huo mnaouita Muungano unazaliwa. Sisi tuliukuta tu. Tunafahamu faida za nchi kuungana lakini tunapojaribu kulinganisha aina ya Muungano tulionao Watanzania, hapo ndipo mazongezonge yanapotujia.
Amini usiamini, itafika kipindi vijana wa Watanzania Bara tutaona this is nonsense aina gani ya Muungano hii? Ama tuurekebishe au tuuvunje. Tukubali au tukatae, wengi wa vijana hawaoni faida ya huu unaoitwa Muungano.

Kwa hiyo kunapokuwa na sehemu moja ya Muungano inaamua kujifanyia mambo yake, ambayo kwa namna moja yanaweza kuathiri sehemu nyingine ya Muungano na hawataki waulizwe ama kutoa maoni, hapo ndipo tatizo linapokuja. Na hakuna taifa la leo ama la kesho la vijana wa Tanganyika litakalotaka kulea hali hii.
Tunachotaka kujua vijana ni je: Nini kipo nyuma ya pazia ya haya maridhiano ya Seif na Karume? Je Serikali ya mseto haiwezi kuundwa hata baada ya uchaguzi? Kwani ni lazima kuahirisha uchaguzi?
Kwa nini katiba haiwezi kuheshimiwa kwa sababu ya matakwa ya mtu mmoja, Karume au Seif? Kwani hayo makubaliano ya Seif na Karume hayawezi kuendelezwa na Rais mwingine yeyote ajaye isipokuwa Karume tu?

Haya ndiyo maswali ya vijana wa Bara yanayohitaji majibu, na si kutaka kutufunga midomo; eti hatuna haki ya kuzungumzia historia ya Wazanzibari. Kutuambia kwamba kila Mzanzibari anapozaliwa tu, basi, historia tayari ipo ndani ya damu yake, ni ushabiki usiomithilika na hoja za ubabe wa kitoto.
Serikali ya mseto ni jambo jema kwa mustakabali wa Zanzibar, lakini bila mapatano naona si suluhisho pekee la mivurugano ya Zanzibar. Tuambiwe ni nini kilichokuwa kinakwamisha hiyo serikali ikakawia siku zote hizo, lakini ghafla ije leo tena na kutaka kubadilisha katiba ili Karume aongezewe muda wa kuwepo madarakani. Kuna nini hapo? Mtujibu kwa hoja, msitutishie nyau!

Makala hii imeandikwa na kijana wa Kitanzania anayeishi nje ya nchi kwa sasa. Barua pepe: tanzafpm@yahoo.com
 
Tusiandikie mate na wino upo...chama cha CCM cha Nyerere, hakiwakilishi matakwa ya wazanzibari.Ni chama kilichopo ulingoni kutekeleza sera za Bara au zake binafsi yake kama chama.

Ndio sababu ya msingi ya kufeli chama hicho huku visiwani.Na hii haijaanza leo, tokea shina la ASP likiitwa TAA (if im right bout history).Hiki chama kitoto kilikuwa ni chama cha Nyerere behind doors, ndicho chama hichi hichi kilicho shiriki kupindua Zanzibar.

Na baada ya Mapinduzi, chama hicho kikiongozwa na Nyerere ndio kilichopoteza muelekeo mzima wa Zanzibar hadi ikapoteza mamlaka yake yote.Hapa sio tuu Mapinduzi, bali nguvu za ziada zilitumika kuuwa na kufumba wazanzibari wasipige hata chafya.

Hapa western walivyoleta vyama vingi Africa, walikuwa washasahau maasi yao katika historia au tuseme mungu hawatupi waja wake...ndio sasa unaona CUF imeanzishwa 1992, 3 years later imepanda juu na kufika kileleni kuwakilisha wazanzibari walio wengi ambao walikuwa hawana la kufanya ndani ya CCM (chama cha mafia's).

Sasa ndugu yangu mie nikisema ukweli usiumie, bali uvumilie....sawa na mimi ukipiga kelele za utumwa na uchafu wote mwengine....inanibidi nivumilie maana huo ndio ukweli.

Sometimes ukweli hata ukisababisha machozi kudondoka...lakini tutafanyaje?Ukweli ndio huo, Zenji ishachoka kuburuzwa....tusubirie hiyo kura ya maoni....sisi wengine ni waumini, tunaomba dua zetu hili la GNU lipite ili vibabu vyetu huko visiwani vipate kupunga upepo wa karafuu BADALA WA MABOMU YA KUWASHA :D

What if baada ya hayo maridhiano hicho chama cha mafia's as you call it, kikishinda uchaguzi tena. Utakikubali kama chama cha wazanzibar?

Kati ya CCM, CUF na ASP unataka nini?
 
Honestly, mimi sina tatizo na kukubali matokeo.Ni mtu mmoja wa ajabu sana kwenye masuala ya vyama maana si supporter wa chama fulani.Mimi natetea maslahi ya wazanzibari tuu, kitu ambacho sioni kama CCM ina maslahi yoyote visiwani humo.

CCM kama ikishinda kidemokrasia nitaikubali na kuipongeza kama kawaida ya uchaguzi na utaratibu wa demokraisia.Lakini naogopa kuwa haijawahi kushinda Zanzibar.Mimi ni katika wale watu ambae hawababaishwi na kelele za kwenye viriri, nafuata scientific data kutoka kwa wataalamu.

Na election data za Zanzibar kutoka kwa international observers, zinaonesha election za Zanzibar hazijawahi kuwa Free and Fair elections.Kwa upande wenu Tanganyika, they are far from perfect but at least it shows CCM wins on the mainland.

Kati ya CCM, CUF na ASP unataka nini?
ASP unfortunately sikijuwi wala sijawahi kukiona na wala sijawahi kuisoma katiba yake.

Baina ya CCM na CUF kama nikiambiwa nipige kura, obviously nitaipigia CUF.Nina sababu zangu za msingi kufanya maamuzi hayo kama nitakuwa kwenye chumba cha kupiga kura.

1.CUF iko katika nafasi nzuri ya kutetea maslahi ya mzanzibari ndani ya muungano (federal govern policy) na internationally kuliko CCM.CUF hawawezi kuguswa na ubabe wa Butiama, hivyo kutakuwa na kujadili hoja tuu bila kuuwa wanasiasa.

2.CUF kidogo inaonesha kuwa na wazalendo wengi na watu wenye uchungu na visiwa vya Zanzibar kuliko CCM ambao huingia madarakani kwa mgongo wa Bara.

3.By the way CUF iko katika nafasi nzuri kuleta umoja wa kitaifa, kwani inakubalika visiwani pemba na Unguja.

4.CUF naiona kama ina wataalamu wengi na wasomi zaidi, kwani wale wasomi wote walifukuzwa na CCM wamejiunga na CUF.Nadhani mifano ipo mingi tuu ya CCM kuwasumbua wasomi visiwani humo hususan kipindi cha Salmin.

Note:
**By the way, kama nilivyosema awali mimi si mwanasiasa ni mwananchi ninaejadili maslahi ya jamii yangu zaidi kuliko ushindani wa vyama.
 
Nazipenda na 'kuzizimia' articles za Lula Mwananzela na Mzee Mwanakijiji because they always provide 'food for thought'!
 
Lula inspirations inataka kujua nini kiko nyuma ya pazia la maridhiano.Auliza ni kwanini sasa na sio zamani au baada ya uchaguzi.Sio kwamba yamefanyika na tujaribu kuyapa nafasi kama yatafanikiwa?

...Sasa wazenj wanasema lets give this attempt a shot, yeye anaona bora tuache tusubirie hadi uchaguzi upite.Naona kama amesahau kama tatizo lenyewe limeanzishwa na uchaguzi....sasa kupata uchaguzi mwengine si ndio maafa zaidi???...i guess he doesnt even care about that :D

Makala hiyo ya kijana akijadili masuala ya Zenj.

Kuna nini nyuma ya pazia la mariadhiano ya Seif, Karume?
NIANZE kwa kumpongeza mwanasafu Lula wa Ndali Mwananzela. Nampongeza kwa kutekeleza vyema jukumu la kuhabarisha na kuelimisha umma wa Watanzania kupitia makala zake.
Lazima nikiri kwamba mimi ni msomaji mzuri wa makala zake kupitia gazeti la Raia Mwema. Licha ya kuwa kwangu nje ya nchi kwa sasa, hiyo hainifanyi nisifuatilie kinachoendelea huko nyumbani.
Nimevutika sana na hali ya kisiasa inayojitokeza kwa sasa huko nyumbani; hususani sehemu za Visiwani. Hata hivyo kuvutika kwangu si kwa uzuri; bali kwa mshawasha wa kujua siri ya hili jambo linalopigiwa kelele na kushupaliwa na karibu watu wengi; hasa wale wenye kujiita ‘Wazanzibari wenye kuijua historia yao’.
Nataka kukubaliana na Bw. Lula kuhusu suala moja; nalo ni kuwa mimi kuijua au kutokuijua historia ya Zanzibar, niwe au nisiwe Mzanzibari (Rejea Raia Mwema Na. 118), hakunifungi mdomo kuacha kuzungumzia ninachokiona kinaendelea huko Visiwani.

Hoja za hao wanaomsakama wakidai kwamba wao ndiyo pekee wanaoijua historia ya Zanzibar, ni hoja za watu wenye jazba ambao hufikiri kwa mdomo badala ya ubongo!
Suala linalotushtua tulio wengi; ni nini hasa kipo nyuma ya pazia la hayo yanayoitwa maridhiano ya hawa mabwana wawili – Seif na Karume? Ni kwa heri ya Zanzibari kweli kweli au kuna lililojificha nyuma ya pazia kwa manufaa yao wawili?

Iweje maridhiano ya wawili hao yaje leo tunapokaribia uchaguzi mkuu? Ni kipi kilichobadilika ambacho kilikuwa kinakwamisha haya makubaliano (sijui niyaite maridhiano au mapatano) yasifanyike huko nyuma pamoja na vikao na mijadala kadhaa kufanyika?
Kwa maswali yangu haya simaanishi kuwa napingana na hayo wanayoyaita ‘maridhiano au mapatano’; bali najaribu kujiuliza nia yake hasa. Ninachokiona ni kuwa, kuna ukungu mkubwa katika hayo yanayoitwa maridhiano. Na mbaya zaidi, ukungu huu umewafunika macho hao wanaojiita ‘Wazanzibari wenye kuijua historia yao’ kiasi kwamba hawataki hata kuhoji kinachoendelea, na badala yake wanakurupuka na kushupalia tu kwa ushabiki.

Inapotokea wengine kuuliza maswali kama haya ninayojiuliza ndipo tunapoonekana watu wa Tanzania Bara hatuitakii mema Zanzibar, na kwamba tunafurahia wao waendelee kuvurugana.
Ninachojiuliza ni kuwa; hivi hatuwezi kuzungumzia mapatano ya Zanzibar bila watu kuleta hoja za kuuvunja Muungano? Hivi dawa ya kutufunga midomo tunaohoji siri ya hayo makubaliano au maridhiano ya Seif na Karume ni kututishia kuvunja Muungano?

Hii inakuwa kama mwanamke mwenye gubu – usimuulize swali lolote, ukimuuliza tu atakutishia kukuacha. Huu ni utoto. Swali hupewa jibu la hoja, na si vinginevyo.
Kitu ambacho wote mnapaswa kukumbuka ni kwamba vijana wengi hatukuwepo wakati huo mnaouita Muungano unazaliwa. Sisi tuliukuta tu. Tunafahamu faida za nchi kuungana lakini tunapojaribu kulinganisha aina ya Muungano tulionao Watanzania, hapo ndipo mazongezonge yanapotujia.
Amini usiamini, itafika kipindi vijana wa Watanzania Bara tutaona this is nonsense aina gani ya Muungano hii? Ama tuurekebishe au tuuvunje. Tukubali au tukatae, wengi wa vijana hawaoni faida ya huu unaoitwa Muungano.

Kwa hiyo kunapokuwa na sehemu moja ya Muungano inaamua kujifanyia mambo yake, ambayo kwa namna moja yanaweza kuathiri sehemu nyingine ya Muungano na hawataki waulizwe ama kutoa maoni, hapo ndipo tatizo linapokuja. Na hakuna taifa la leo ama la kesho la vijana wa Tanganyika litakalotaka kulea hali hii.
Tunachotaka kujua vijana ni je: Nini kipo nyuma ya pazia ya haya maridhiano ya Seif na Karume? Je Serikali ya mseto haiwezi kuundwa hata baada ya uchaguzi? Kwani ni lazima kuahirisha uchaguzi?
Kwa nini katiba haiwezi kuheshimiwa kwa sababu ya matakwa ya mtu mmoja, Karume au Seif? Kwani hayo makubaliano ya Seif na Karume hayawezi kuendelezwa na Rais mwingine yeyote ajaye isipokuwa Karume tu?

Haya ndiyo maswali ya vijana wa Bara yanayohitaji majibu, na si kutaka kutufunga midomo; eti hatuna haki ya kuzungumzia historia ya Wazanzibari. Kutuambia kwamba kila Mzanzibari anapozaliwa tu, basi, historia tayari ipo ndani ya damu yake, ni ushabiki usiomithilika na hoja za ubabe wa kitoto.
Serikali ya mseto ni jambo jema kwa mustakabali wa Zanzibar, lakini bila mapatano naona si suluhisho pekee la mivurugano ya Zanzibar. Tuambiwe ni nini kilichokuwa kinakwamisha hiyo serikali ikakawia siku zote hizo, lakini ghafla ije leo tena na kutaka kubadilisha katiba ili Karume aongezewe muda wa kuwepo madarakani. Kuna nini hapo? Mtujibu kwa hoja, msitutishie nyau!

Makala hii imeandikwa na kijana wa Kitanzania anayeishi nje ya nchi kwa sasa. Barua pepe: tanzafpm@yahoo.com

Nashangaa saana watu wa aina hii ambao wamo wengi tu humu, sasa kwanini msiseme cuf wapewe nchi yao kwani wao ndio mara zote wanashinda na kwa ushahidi tosha,mnaleta ati kwanini isiwe baada ya uchaguzi,sijui kwanini ibadilishwe katiba, kwani wewe huwelewi kilichozungumzwa hasa ni tatizo kuwa uchaguzi znz ndio unaleta matatizo? tena basi ikifika nyinyi wabara na vifaru vyenu mnakuja zenji,sasa bado tung'ang'anie tu uchaguzi.. sasa mnaogopa nini ikiwa muungano utakufa wakati nyinyi muna nchi kubwa tu na rasili mali kibao.. duh! watu wengine kama vidudu mtu. ANDIKENI KUWA AMANI YA KUDUMU IMEFIKA ZANZIBAR
 
Honestly, mimi sina tatizo na kukubali matokeo.

2.CUF kidogo inaonesha kuwa na wazalendo wengi na watu wenye uchungu na visiwa vya Zanzibar kuliko CCM ambao huingia madarakani kwa mgongo wa Bara.

3.By the way CUF iko katika nafasi nzuri kuleta umoja wa kitaifa, kwani inakubalika visiwani pemba na Unguja.

4.CUF naiona kama ina wataalamu wengi na wasomi zaidi, kwani wale wasomi wote walifukuzwa na CCM wamejiunga na CUF.Nadhani mifano ipo mingi tuu ya CCM kuwasumbua wasomi visiwani humo hususan kipindi cha Salmin.

Note:
**By the way, kama nilivyosema awali mimi si mwanasiasa ni mwananchi ninaejadili maslahi ya jamii yangu zaidi kuliko ushindani wa vyama.
Unashangaza kwa nini huwi uinayakubali basi?

Acha kusema uongo hapa jamvini. Lete vithibitisho vya 2,3,na4.
 
2.Ushahidi ni kwenye kufanya maamuzi, CCM Msekwa && Makamba are on top of Zanzibar.Wakati CUF Maalim is free to decide on Zanzibar issues....au huoni hata hilo???

3.Sasa soma idadi ya kura na seats zilizopatikana kwenye Zanzibar elections.CUF ina seats kutoka kwenye visiwa vyote viwili, especially 95 kabla CCM hawajafanya ujanja wa kugawa majimbo.

4.Wataalamu wangapi wametolewa SMZ kwasababu za kisiasa?....pengine hao CUF wote walikuwa ndani ya CCM, sasa wako CUF.Example Dr.Muchi huyu jamaa ni mtaalamu wa afya, na alikuwa na project nyingi ndani ya SMZ kama Malaria, mkuu wa hospitali ya Mnazi mmoja...amesumbuliwa na Salmin, sasa hivi yuko CUF...mifano mengine sina wakati tafuta mwenyewe, but in general wataalamu wote wa CUF wametoka ndani ya CCM.
 
Back
Top Bottom