MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 590
- Thread starter
- #21
Ninachofahamu ni kwamba huko Butiama walikuwepo Wazanzibari vile vile (Karume, Nahodha, et al) na kama waliona hilo wazo la Wabara (kama waliolianzisha ni wabara anyway, maana hujatoa ushahidi kuhusu hili) wangelikataa! Hapa nako unawaweka Wazanzibari waliokuwepo Butiama kuwa si lolote kama ilivyokuwa kwenye BLW! Anyway, kama nilivyosema tangu mwanzo, ikitokea hitilafu mahali fulani, Wazanzibari wanawekwa pembeni, hata kama walikuwa ni wenyewe watupu kama ilivyokuwa kwenye BLW, "mzigo mzito anabebeshwa Mnyamwezi!" Sasa hivi mmekaa mkao wa lawama kuhusu kura za maoni, ikitokea Wazanzibari wakakataa Serikali ya Mseto (Umoja wa Kitaifa?) Your hypocricy (undumilakuwili, ukinyonga, etc) will come to light soon!
Tusiandikie mate na wino upo...chama cha CCM cha Nyerere, hakiwakilishi matakwa ya wazanzibari.Ni chama kilichopo ulingoni kutekeleza sera za Bara au zake binafsi yake kama chama.
Ndio sababu ya msingi ya kufeli chama hicho huku visiwani.Na hii haijaanza leo, tokea shina la ASP likiitwa TAA (if im right bout history).Hiki chama kitoto kilikuwa ni chama cha Nyerere behind doors, ndicho chama hichi hichi kilicho shiriki kupindua Zanzibar.
Na baada ya Mapinduzi, chama hicho kikiongozwa na Nyerere ndio kilichopoteza muelekeo mzima wa Zanzibar hadi ikapoteza mamlaka yake yote.Hapa sio tuu Mapinduzi, bali nguvu za ziada zilitumika kuuwa na kufumba wazanzibari wasipige hata chafya.
Hapa western walivyoleta vyama vingi Africa, walikuwa washasahau maasi yao katika historia au tuseme mungu hawatupi waja wake...ndio sasa unaona CUF imeanzishwa 1992, 3 years later imepanda juu na kufika kileleni kuwakilisha wazanzibari walio wengi ambao walikuwa hawana la kufanya ndani ya CCM (chama cha mafia's).
Sasa ndugu yangu mie nikisema ukweli usiumie, bali uvumilie....sawa na mimi ukipiga kelele za utumwa na uchafu wote mwengine....inanibidi nivumilie maana huo ndio ukweli.
Sometimes ukweli hata ukisababisha machozi kudondoka...lakini tutafanyaje?Ukweli ndio huo, Zenji ishachoka kuburuzwa....tusubirie hiyo kura ya maoni....sisi wengine ni waumini, tunaomba dua zetu hili la GNU lipite ili vibabu vyetu huko visiwani vipate kupunga upepo wa karafuu BADALA WA MABOMU YA KUWASHA