Zanzibar 2020 Hoja za Dkt. Hussein Mwinyi zinatosha kumpa nchi Oktoba 28

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
HOJA ZA DK HUSSEIN MWINYI ZINATOSHA KUMPA NCHI OKTOBA, 28

Dkt. Hussein Mwinyi mgombea wa nafasi ya Urais Zanzibar anastahili kuchaguliwa kwa kura za ndio nyingi na kupewa nchi ili awaongoze Wazanzibar, nimefatilia mikutano yake ya kampeni na kubaini kuwa ni miongoni mwa wagombea bora wenye kujenga hoja zinazo mulika kutatua matatizo ya Wazanzibari, Mwinyi anaendesha siasa za hoja na ahadi mpya za kutatua kero wala si mashambulizi kwa wenzake, Pia hoja zake zinajikita kwenye ubunifu wa vyanzo vipya vya ajira kwa Wazanzibari.

Aidha Mwinyi anaguswa fika kizalendo na changamoto za Wazanzibari na ndio maana yupo tayari kuziishi na kuzitatua kwa vyovyote vile.

Mpaka sasa nimegundua Dkt. Mwinyi ana uwezo wa kipekee wa kujenga hoja za Kiuchumi dhidi ya watu na vitu aidha ni mwanaujamaa anayeamini katika falsafa ya kuwakomboa watu wa rika la chini ambao ndio wenye huitaji zaidi, Kwa kutumia jicho la tatu Zanzibar iliyostawi chini ya Mwinyi inarejea mikononi mwa Wazanzibari, Ni rai yangu kuomba Wazanzibar kuitumia fursa hii ya kumchagua kwa wingi Dkt. Mwinyi ili aweze kutimiza ndoto zao, ni nadra sana taifa kuwapata viongozi wenye kariba ya Mwinyi, hivo tuitumie vema fursa hii.

Ndoto za Dkt. Mwinyi kwa Wana-Zanzibar ni ndoto za kizalendo ambazo uwezi kuzisikia kwa kiongozi mwingine kati ya wanaogombea urais visiwani humo.
 
Naungana na mleta mada,

Jamaa anafanya siasa safi , za hoja yakinifu.

CCM kwa ujumla wake hawamshambulii mtu wanakwambia wamefanya nini na watafanya nini.

Mwinyi ni mtu sahihi kwa Zanzibar, wazanzibari msiipoteze nafasi hii adhimu ya kufikia aina ya maendeleo mnayoyataka.
 
wazanzibari wanataka raisi wao wanamtaka sio raisi wakuletewa kutoka Dodoma. Hata Mwinyi akisema atatuletea mwezi hapa chini, hilo haliwezekani kubadilisha mioyo yetu wazanzbari. Usishituliwe na kauli za majukwaani. Juzi Dr. Shein amelazimisha wafanya kazi wote wapeleke vitambulisho vyao vya ukaazi na vya kupiga kura. Asiefanya hivo atawachishwa kazi. Sasa kauli kama hii inatoa ishara gani?.
 
Mwaka huu uweke historia. Msichague Rais wa kuletewa kutoka Dodoma. Msimpe kura kabisa. Na akipandikizwa kijecha Jecha, fanyeni mapinduzi mapya kama ya 1964.
 
Matatizo makubwa yanaanzia na baadhi ya watu kupewa nchi badala ya dhamana ya uongozi
 
Matatizo makubwa yanaanzia na baadhi ya watu kupewa nchi badala ya dhamana ya uongozi

Tatizo wanasema Zanzibar si nchi , ni ngawira ya Uvamizi , waache wapeane mwisho wao ni OKTOBER 28. 2020
 
Thubutu.
Unadhani wazanzibar ni watu wa mchezo mchezo eeeh! Wazanzibar wanataka taifa lao lenye uhuru kamili na mamlaka ya kinchi. Hussein Mwinyi hana huo ubavu wa kuweza kuahidi hilo, maana akifanya tu hivyo, keshokutwa atavuliwa uanachama wa CCM na uchaguzi kufutwa!!

Muulize Salmin Amour, Amani Karume, Shein ni kwanini walishindwa kupata kura za wazanzibar mpaka wakabebwa na ZEC?

Kwa taarifa yako tu, katika wagombea wote wa urais wa CCM Zanzibar kuwahi kutokea, Hussein Mwinyi ndio mgombea mwepesi mnoo kwa kuwa haungwi mkono hata na wanaCCM wenzake. Mchawi mkuu wa mwaka huu kwa Hussein Mwinyi ni CCM Zanzibar. Kama hutaki kuamini subiri utaelewa.

Mwaka huu CCM ili kupata ushindi Zanzibar itabidi jeshi litumike kwa 100%.
 
Hakuna CCM hata Mmoja anaeweza kusimama na kusema kuwa Zanzibar itakuwa na mamlaka kamili, hawathubutu. CCM kama angelikuwa na sera ya Zanzibar yenye mamlaka kamili basi ningesema Oktoba Maalim ajipange kweli kweli. Wazanzibari hawataki story sijui za uchumi, ajira na mengine. Wazanzibari wanataka MAMLAKA kamili, kitu ambacho CCM haiwezi kufanya.

Kuna mbinu CCM wanazirudia rudia katika kupora ushindi. Mbinu yao ya mara hii ni ya Tarehe 27 Oktoba. Hii ndio siku ambayo CCM watajiwekea kura za uporaji.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom