KisaUnamtafutia Gwajima matatizo, hizi nyuzi zikiendelea endelea zinaweza kusababisha avulie ubunge wake.
Mwili wako una Kinga za Magonjwa mbalimbali au hauna? Kama unazo mbona Huwa unaugua na kuambukizwa hayo magonjwa?Kwanini mtu akichanjwa anaendelea kuambukiza /kuambukizwa?
Kama chanjo ni kinga, kwanini mtu aliyechanjwa anaendelea kuvaa barakoa?
Kwanini kwenye vaccine form serikali imejitoa kuwajibika endapo mtu aliyechanjwa atapata madhara?
Toa majibu
Nasikitika nimeenda kituo kimoja nimeambiwa Sina kigezo Cha kuchanja nisubiri mpaka tamko jingine la serikali.Nikawambia watu si hawataki kuchanja mie nipo tayari nichanjeni,wapo tunaanza na makundi maalum.Mimi nimeshachanja 09.08.2021.
Wataalam wetu wanaujua ukweli shida moja hawajapewa Uhuru was kueleza ukweli.Kila kitu kinaratibiwa na siasaHatuna wataalamu, tuna wachumia tumbo. Wananchi wamefanywa majuha, jana wataalamu wanasema wazungu hawaaminiki, chanjo haziaminiki. Leo hao hao, akiwemo na Samia wamebadiri wimbo, wananchi mkachanjwe, chanjo ni bora kwa kinga ya corona. Hawana aibu, wanaongea kwenye majukwaa bila kupepesa macho.
Ninachokumbuka ni kuwa wanasema chanjo inakuwa effective kabisa wiki mbili baada ya kuchanjwa yaani sio leo unachanjwa na kesho unakuwa na askari mwili mzima...kwa hiyo tunasubiri wiki mbili zipite tuone mwelekeo...Hata hivyo chanjo hazina ufanisi wa asilimia 100 ni kama 70 hivi kwa hiyo na kujikinga kimtindo sio mbaya hasa wale wa makundi maalum kama hao wa miaka 50 au 60 plus. nawasilishaHata mm sijawahi kupata majibu haya nikaridhika. Tujiulize kama kweli Samia kachanja kwanini anavaa barakoa? Yeye ana tofauti gani na mimi ambaye sijachanja? Kuna umuhimu gani wa chanjo kama utaendelea kuchukua tahadhari zile zile?
Kufufua watu na wengine kufa ni mtindo wa maisha. Hata wakati wa Yesu Kristo watu walikuwa wanakufa na kuumwa kama kawaida. Maana yake ni kwamba sio wafu wote waliopata bahati ya kufufuliwa na Yesu kadhalika sio wagonjwa wote waliopata bahati ya kuponywa na Yesu.Huyo gwajima aulizwe nae swali moja. Yeye si anafufua wafu. kwanini asimfufue mwwndazake? Au atupe jibu zile zilikuwa propaganda hazina ukweli.
Muwe na akili basi,kwa sasa chanjo iliyopatikana ni hiyo ya kukuongezea immunity!Sasa kama unasubiri kinga kamili basi subiri!Ni sayansi gani ya chanjo inayosema ujikinge baada ya kupata chanjo? Wewe ulipopigwa ndui (ikiwemo chanjo ya TB) uliambiwa uvae barakoa?
Kama inaongeza immunity kwa nini utumie barakoa? Ulipopigwa chanjo ya polio ulihitaji booster?Muwe na akili basi,kwa sasa chanjo iliyopatikana ni hiyo ya kukuongezea immunity!Sasa kama unasubiri kinga kamili basi subiri!
Gwajima amewatia dole kinoma nomaUnamtafutia Gwajima matatizo, hizi nyuzi zikiendelea endelea zinaweza kusababisha avulie ubunge wake.
Hoja ya kwanza:Nilitegemea wataalam wetu wa afya pamoja na washauri wa Rais waliomshauri kuagiza chanjo ya corona watakuwa mstari wa mbele kujibu hoja za askofu badala yake wamekuwa watu wa kumshambulia yeye binafsi na kumpa vitisho badala ya kujibu hoza zake kitaalam.
Katika hoja ya kwanza, Askofu gwajima ana hoji: Endapo mtu akichanjwa bado ataendelea kuambukiza na kuambukizwa virusi vya corona na kama ndivyo, kuna maana gani ya kuchanja?
Hoja ya pili Askofu anahoji endapo mtu amechanjwa bado atatakiwa kuchukua tahadhari zote ikiwemo kuvaa barakoa ili kujikinga na maambukizi. Askofu anataka kujua, kama kweli chanjo ya corona ni kinga kwanini mtu aliyechanjwa anatakiwa tena kuvaa barakoa?
Askofu anaendelea kuhoji, mataifa makubwa kama vile marekani yote yana chanjo zao. Kwa mfano, marekani wana chanjo ya jonhson&jonhson na moderna, china wana sinovac, uiongereza wana Astrazeneca, germany wana Pfizer, urusi wana ya kwao, Cuba pia wana ya kwao na mataifa mengine yana chanjo zao. Je ni kwanini haya mataifa yenyewe kwa yenyewe yanaogopana kutumia chanjo ya mwingine?
Gwajima ana hoji kwamba katika kipindi cha zaidi ya miezi sita iliyopita wataalam wetu wanaotaka tupambane na corona kwa njia ya chanjo ndio hawa hawa walisema tusiziamini chanjo kwamba zinaweza kuwa na madhara na kwamba tutumie njia za asili ikiwemo kujifukiza wakajenga hadi banda la kujifukizia pale muhimbili wengine wakafanya mahojiano TBC kuonyesha wasi wasi wao juu ya chanjo ya corona, kwanini leo wamebadilika?
Swali la nyongeza: kwenye fomu ya chanjo ya corona kuna kipengele kinasema serikali haitahusika kwa namna yoyote ile endapo mtu aliyechanjwa atapata maudhi ambayo kwa sasa hayafahamiki. Tunataka wataalam wetu watwambie kama hii chanjo wameifanyia utafiti wa kutosha kwanini wanasema tena kwamba mtu aliyechanjwa anaweza kupata maudhi ambayo hayafahamiki?
Napenda sana wataalam wajibu hoja za gwajima kwa sababu vile wanavyomshambulia badala ya kujibu hoja zake ni kudhihirisha kwamba hawana utaalam wa walichosomea kitu ambacho ni hatari kwa uhai na afya za watanzania.
Hivi hakuna mpinga Islam? Kila siku nasikia mpinga kristo 666.hoja kwamba chanjo ni mpango wa 666 na agenda ya mpinga kristo?
Hili swali lielekezwe kwa kibwetere wa kawe.Hivi hakuna mpinga Islam? Kila siku nasikia mpinga kristo 666.
Mbona huelewi?Hii chanjo iliyopatikana so far ni kwa ajili ya kuongeza uwezo wa mwili kupambana na virus!Haizuii wewe kupata Corona ila inakusaidia ukipata uwe na chance kubwa ya kuishinda kuliko kama hujachanjwa!Kama inaongeza immunity kwa nini utumie barakoa? Ulipopigwa chanjo ya polio ulihitaji booster?
Unaielewa sayansi ya vaccine lakini?Mbona huelewi?Hii chanjo iliyopatikana so far ni kwa ajili ya kuongeza uwezo wa mwili kupambana na virus!Haizuii wewe kupata Corona ila inakusaidia ukipata uwe na chance kubwa ya kuishinda kuliko kama hujachanjwa!
Hiyo ndiyo iliyopatikana,kama unataka chanjo ambayo itazuia kabisa usipate Corona basi subiri,wataalamu bado wako wanapambana!
Usichanje kama unaona bado hujaridhika!Ila hao waliokufundisha ukajua vaccine ndio hao wamekuja na suluhisho la muda mfupi la Covid!Ukitaka hicho unachotaka basi subiri!Unaielewa sayansi ya vaccine lakini?