Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Hamza Juma, amejitokeza kutaka kupeleka hoja binafsi ili Baraza la Wawakilishi litunge sheria kuzuia wagombea ambao hawajtimiza miaka miwili ya uanachama wa chama cha siasa, wasigombee katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Hii ni hoja mbovu isiyo na mantiki. Ukimchunguza huyu mtu ni kama yule Jecha wa November 2015. Ametumwa.
Yote hii ni moja ya mambo yanayofanywa na CCM kuvuruga uchaguzi.
Hoja ya Hamad Juma haina tofauti na ubadilishaji wa ramani za majimbo ya uchaguzi ili kudhoofisha nguvu za wagombea wa upinzani, kama ulivyofanywa maeneo ya Segerea Tabata, Temeke/Kigamboni, Ubungo/Kibamba nk.kabla ya uchaguzi 2015. (Hii inaitwa Gerrymandering)
Bahati nzuri huyu mwakilishi ameongea kupitia DW leo mchana kwa kujiamini kabisa kwamba amesema kitu ambacho ulimwengu utamwona ana busara sana! Na hii ndiyo tabia ya baadhi ya wanasiasa wengi upande wa watawala.
Ni juzi tu dunia imeshuhudia mbinu chafu za POTUS DT dhidhi ya mtarajiwa mgombea mwenzake Joe Biden; hadi Congress kufikia hatua ya kupitisha hoja ya kumfukuza kazi.
Halafu leo anajitokeza mtu hapa nchini kutaka ulimwengu ujue kwamba tunao watu kama Trump wanaoandaa kuvuruga Uchaguzi Mkuu ujao kwa makusudi tu?
Imefika sasa hata baadhi tuliokuwa tunavumilia madudu ya muungano tunaanza kukata tamaa. Kwasababu kitu alichosema huyu mwakilishi kinahusu vyama kwanza kabla ya kuingizwa ktk sheria ya uchaguzi, ambayo ni ya Jamhuri mzima.
Kiutaratibu angeanzia kwenye katiba za vyama. Kwasababu kikatiba kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Pendekezo lake linapingana na Katiba ya JMT, ingawa kwa CCM ataungwa mkono na hoja yake kupitishwa katika Baraza la Wawakilishi.
Ni wazi hizi ni njama za kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa November huko visiwani na lengo lao liko wazi mno.
Lakini yote kwa yote tusubiri tuone kama wataendelea?
Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app