Hoja ya waislam dhidi ya filamu ya kimarekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya waislam dhidi ya filamu ya kimarekani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sunguruma, Sep 22, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. s

  sunguruma Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 14, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jana waislam walifanya maandamano kupinga kitendo cha raia mmoja wa Marekani kutengeneza filamu inayomkashfu na kuudhalilisha uislam. Maandamano hayo yaliisha kwa kutoa tamko la kuitaka serikali ya Tanzania kuufunga ubalozi wa Marekani mara moja katika kipindi cha siku Saba, la sivyo kama serikali itakaidi amri hiyo baada ya kipindi cha siku saba waandamanaji hao wataufunga ubalozi huo wao wenyewe.

  Hata hivyo mimi nimeona mambo kadhaa hapa.
  1. Kukosea kwa bwana Sam Bacile kutengeneza hiyo movie (ambayo mimi nimeiona)
  2. Haki za kujieleza zilivyo juu sana huko Marekani, kwani pamoja na filamu hiyo kuleta kupingwa na waislam kote duniani na hata kusababisha mandamano na machafuko sehemu mbali mbali za dunia na kupelekea balozi za Marekani huko Misri, Libya, na Sudani kuchomwa mioto, na hatimaye kusababisha kifo cha balozi wa Marekani nchini Libya bado serikali ya Mrekani imeshindwa kuiondoa filamu hiyo katika mitandao hata kutoa tamako la kuipiga marufuku.
  3. Serikali ya Marekani imeshindwa kumchukulia hatua huyo Bwana Sam bacile mtengenezaji wa filamu ya Innocent Muslim ambayo inachafua nyongo za waislam

  Baada ya matatizo hayo Serkali ya Mrekani iliiandikiwa manejiment ya Google kuiomba iondoe filamu hiyo katika mtandao wake wa You tube hata hivyo google walisema filamu hiyo haija violate haki za mtandao wake hivyo basi haiwezi kuiondoa.

  Sasa binafsi nawapa pole ndugu zangu waislamu kwa kuumizwa na filamu hiyo. Lakini mambo machache ningependa kupendekeza.
  1. Nadhani waandamanaji wa jana hawakuwa sahihi kutaka ubalozi wa Marekani Tanzania ufungwe, kwani ubalozi huo haupo Tanzania kwa ajili ya waislam pekee, uwepo wa ubalozi ni kiashiria cha ushirikiano wa watanzania wote (wakristo, waislam, wahindu, wasio na dini nk) hivyo basi kusema ubalozi ufungwe kwasababu ya kundi moja kuwa limeathiriwa na sera za wamarekani ni kuyaumiza makundi mengine.

  2. Hivyo basi mimi ningeshauri waislam wangetangaza kuutenga ubalozi wa marekani, yaani kusiwe na Muislam yeyote atakayefanya kazi na ubalozi wa Marekani. Hakuna kuomba Visa za marekani, hakuna kutembelea wala kusoma marekani.
  Ningekuwa mimi ningewataka waislam wote wanaofanya kazi katika mashirika ya Kimarekani, kama USAID, FHI, BARRICK GOLD, kuacha kazi mara moja, na waislam wote wanaofanya kwenye mashirika yanayopokea mishahara kutoka kwa makampuni au mashirika yanayopata ruzuku kutoka USA kama CARE kuacha kazi zao mara moja. Pia ningetangaza kususia kutumia bidhaa zote za wamarekani kama Coca Cola, ARVS, nguo, viatu, Ipad, Iphone, simu, DELL, nk, waislam wawapige marufuku watoto wao kuingia kwenye website za kimarekani kama google, You tube, Facebook nk.

  Mwisho waiombe serikali ya Tanzania kuifunga hiyo filamu isionekane katika server za Tanzania. najiuliza kwanini serikali yetu mpaka sasa haijachukua hatua ya kuifunga hiyo filamu isicheze kwenye movie serve zetu hapa bongo?? Kijana January Makamba anaweza kuhakikisha hilo linawezekana ili kuhakikisha hakuna watanzania wengi zaidi wanaingia katika kuiona filamu inayookashfu dini ya watanzania na mtume.

  Ni tabia ya watanzania kutozungumza mambo yanayotugusa na kuzungumza yale yasiyotugusa.
   
 2. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ............tunaelekezwa na. viongozi wetu wenye mamlaka ya kutoa "fatwa" kwa niaba yetu !
  Hatufanyi maamuzi kwa kufuata maelekezo ya Mgalatia !
   
 3. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Huo ulikuwa ni ushauri tuu mkuu, na wala si maelekezo
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...