Hoja ya VIJANA kwa Ndg. Dr Wilbrod Peter Slaa Kuhusu Dowans.! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya VIJANA kwa Ndg. Dr Wilbrod Peter Slaa Kuhusu Dowans.!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donyongijape, Feb 5, 2011.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Leo vijana zaidi ya Ishirini hapa mtaani kwetu tumekuwa na kikao kisicho rasmi kujadili mambo yanayohusu taifa letu hasa Dowans na Migomo..Hasira zilikuwa nyingi lakini kwa kuwa tuna raisi tuliyemchagua,tukaamua kukubaliana, mimi na wenzangu tukateuliwa kumpa Ujumbe Ndugu Dr. Slaa na CHADEMA kwa ujumla. Njia pekee na rahisi tuliyoona itafaa ni hapa JF kwa vile hatuna namba yake ya CM au E-mail. Hivyo tunaomba apokee ujumbe huu..!

  ''Tunakuomba Ndugu Raisi wetu,Dr Wilbrod Peter Slaa, uandae mkutano na waandishi wa habari au mkutano wa hadhara na uwataje wote walihohusika kwenye Dowans bila kumung'unya maneno kama ulivyofanya pale ulipoteua 1st Eleven ya Mafisadi. Sisi tunaamini Raisi wetu ni wewe japo upo nje ya Ikulu. Pia tunaamini kuwa hukurupuki hivyo hata sasa una data kamili na za wazi kuhusu huu uhuni unaondelea so hata wakikupeleka mahakamani utashinda na wataabika wao!

  Tunaamini kuwa watu wengi wanachanganywa na hasa hizi sarakasi kwa sababu leo wanasikia hiki, kesho kile na pia wengi hawawezi kuelewa sana hizi 'terms' za mikataba ya kisomi na sheria za huko mahakamani ila wangependa kuelimishwa 'straight forward' bila kupinda pinda.Kwa sasa Wamefanywa kama bendera inayopeperusha na upepo.

  Hivyo Ndugu Raisi wetu,Dr Wilbrod Peter Slaa, weka mambo hadharani moja kwa moja usimung'unye...kama unajua na una uhakika kuhusika kwa JK,RA,EL au yeyote yule tafadhali tunakuomba tutangazie hawa watu bila kificho na sisi tutapanga mikakati ya kudeal nao..! Roho Inauma sana, wanatuchanganya hawa, usituangushe Ndugu Raisi wetu..hebu tuzibie hili Ombwe la Uongozi lililoko pale Ikulu tafadhari.

  Ni sisi Vijana wako,
  Tupo na wewe daima mpaka kieleweke.".
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  thumb up. Dr anaweza na anawajua hata mie nawajua tu
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Alishawataja labda haukumsikia, Salva alimjibu kwa matusi, vijembe na vimaneno vya umbeya umbeya a.k.a Vijembe. Alimtaja Mhusika namba moja kuwa na JK na rafiki yake mkubwa Rostam. Akaenda mbali zaidi kwa kusema trip za Marekani zilikuwa kukamilisha hiyo deal. Ikiwa nimekosea mtanisahihisha.
   
 4. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Its OK..kuna baadhi walimsikia lakini aliongea na Tanzania Daima Peke yake na hata salva alipojibu alijibu kwa kuponda tzdaima..tunataka aongee na sisi wananchi maalum kwa ajili ya hilo tu..kama akiamua kufanya press conference afanye kwa vyombo vyote..mpaka kwenye redio zetu za mikoani kama Iringa,Moro,Karagwe,Kahama,Tandahimba etc tutaisikia hii habari. Au afanye Mkutano wa hadhara popote na awataje laivu siyo kuongea na gazeti moja tu na isiishie hapo wafanye kama operesheni sangara mpaka kieleweke. CHADEMA na Dr. Slaa Zibeni hili Ombwe la uongozi tafadhari
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Slaa ni blabla tu.
  Mbona ameshindwa kuleta ushahidi wa kuibiwa kura na usalama wa taifa?
  Mbona ameshindwa kuleta the so called CHADEMA version ya yaliyojiri Arusha?
  Mbona ameshindwa kutokumtambua Rais Kikwete?

  Yeye sasa hivi ni mshtakiwa.
  Mke wake ana kovu kichwani, he is frustrated - mwacheni apumzike.
   
 6. tartoo

  tartoo Senior Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Craaaaaap:laugh::clap2:
   
Loading...