Hoja ya udini ni toy tulilopewa tugombanie,ili wazidi kutuibia. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya udini ni toy tulilopewa tugombanie,ili wazidi kutuibia.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mrimi, Nov 6, 2011.

 1. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Ni nani asiyejua kuwa mabishano yanohusu imani(dini) hata kama ni kijiweni kwa kawaida hayawi na hitimisho?

  Niseme tu kwamba kama kuna kitu watawala wetu wamethubutu, wakaweza na sasa wanasonga mbele ni kuchezea saikolojia ya watanzania. Si wasomi, si watu wa dini wala wanasiasa, wote wametumbukia ndani ya huu mtego, na bila kujua wanashangilia na kuchekelea tu.

  Siku hizi utasikia watu wanatupiana maneno(makali) na lawama kwamba, ooh, idara fulani au kampuni fulani ni (ya umma) ni ya dini fulani, au chama fulani cha (siasa) ni cha dini fulani, au dini fulani inapenda machafuko, na hata wengine wanadiriki kusema serikali hii ipo kwa maslahi ya dini fulani nk. ili mradi tu upuuzi mtupu. Siku hizi ni kawaida kabisa kusikia maneno kama 'aah waislam hao' au 'aah hiyo si mikristo tu!'Hakuna imani tena miongoni mwa watu.

  Sasa naomba tukumbushane kidogo, ingawa najua wote tunalijua hili. Tuchukulie mfano wa wakristo, hawa watu si wamoja kama tunavyoaminishwa. Ukibahatika kuhudhuria mikutano yao utabaini ninachosema hapa. Hawa huwa wanasemana hata wanafikia kutukanana matusi, na kuna wakati tunasikia wakitishia kushitakiana. Wasabato wako kivyao, wakatoliki kivyao, walokole(nao wana varieties) kivyao nk. Kila kikundi(dhehebu) kinajiona ndicho chenye ukristo wa kweli na kinaona vikundi vingine kama vilivyopotea njia. Jamani, hili liko wazi wala halihitaji phd kulibaini.

  Sina maelezo ya kutosha kuhusu waislam, ila mara nyingi nimekuwa nikiona kwenye mfungo, siku ya kufungua naona wafungua siku tofauti. Kwangu huu ni ushahidi tosha kwamba hata ndani ya uislam kuna tofauti, hata kama ni kwa mujibu wa misingi ya imani yao, lakini bado ni tofauti. Kwa maneno mengine ni kwamba hawajafungamana kwa kila kitu kwa 100%. Ukifanikiwa kwenda mashariki ya kati ndipo utakapojua kwamba uislam, sio uislam tu bali utapata wanaoitwa Washia na Wasunni, siamini kama hizo tofauti hapa kwetu hazipo.

  Sasa, binafsi naona ugumu kiukweli kuamini kwamba kitu fulani kimefanyika kwa maslahi ya wakristo; wakristo gani hao? wasabato, walokole, waanglikana au wepi sasa? Hata ile jumuia ya wakristo(sijui baraza) nashindwa kufahamu dhima yao hasa maana mbona hawajadili jinsi ya kuondoa hizi tofauti zilizopo huku makanisani? Kwa mantiki hiyo, sioni uwezekano wa hawa watu kukaa pamoja na kupanga nani awe rais, maana litakuja swala la usabato na ukatoliki-kumbuka watu hawa hawapikwi chungu kimoja ingawa wote ni wakristo.

  Lakini pia sijapata mtu akisema(kwa ushahidi) kwamba katika kanisa au msikiti wake amefundishwa akaibe, au amefundishwa akafanye zinaa, au akachukue rushwa au akafanye uchafu mwingine wowote tunaoufahau. Dini zote ziafundisha maadili mema.Zote zinakemea uchafu na kutuhimiza kuishi kwa staha na kupendana. Mimi sioni mantiki ya ku generalize mapungufu ya waumini wachache waliokengeuka na kusema kwamba dini yote imechafuka. Hii siyo kweli. Kuasi kwa muumini mmoja hakuna maana kuwa dini nzima imeasi, hebu ahukumiwe yeye kama yeye. Kwa mfano hii issue ya ufisadi, kama vile Dowans watuhumiwa ni watu wa dini mbalimbali tofauti, wahanga wake ni sisi sote(wakristo+waislam) ambao kila siku tunatupiana kejeli huku mtaani. Wao hawajui habari ya ukristo wala uislam, wanachojua wao ni pesa tu.

  Ufike wakati tufumbuke macho jamani. Hebu bongo zetu zitimize wajibu wake wa kufikiria. Hawa watawala baada ya kuona watu sasa wamechoka na umasikini na dhiki ndani ya nchi yao yenye rasilimali karibu sawa na South Africa, wakagundua kuwa ipo siku watu watakosa uvumilivu. Ikabidi watafute weak point yetu ilipo wakagundua,wameitumia. Je, tunakumbuka kisa cha Mnara wa Babeli? Mwenyezi Mungu aliwaadhibu waja wake kwa kupandikiza hizi lugha tunazotumia siku hizi(ingawa hakusema kama kuna lugha bora kuliko nyingine).

  Sasa hawa wenzetu wao wametuletea hili toy linaloitwa udini wametuachia tunang'ang'aniana na kukimbizana kama manyang'au huku wao wakiendelea kukomba na kugawana rasilimani za watoto na wajukuu zetu. Na sisi tukidhani kwamba labda swala hili ndiyo suluhu ya matatizo yetu, tunapoteza muda wetu kwa ubishi wa mambo yasiyokuwa na tija hata kidogo.

  Hivi tunadhani rais akiwa mkristo au mwislam kuna mantiki gani, endapo ataongoza kwa mujibu wa katiba. Sisi tunataka rais afuate katiba kutuongoza. Ni mawazo mgando ya wachache waliofilisika kifikra kutegemea upendeleo fulani kutoka kwa kiomgozi eti kwa kuwa ni dini yako.

  Zinduka ewe mwana wa watanzania... Hii miaka 50 ya uhuru tujiulize watanzania tutarusha lini roketi kwenda anga za mbali. Si kusema rais anaangushwa na dini fulani, wala si muda wa kusema dini fulani inapenda ghasia nk.

  Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika.

  Nawasilisha...........
   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hii ya udini alianzisha jk wakati wa kampeni japo sio kitu kilichokuwepo kweli
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kuna siku nilitembelea Bagamoyo, nikakutana na babu mmoja ambaye anaendelea kuamini dini za mababu. Nilipomuuliza kwa nini anafanya hivyo, akanieleza kuwa Mungu hakuanza kuwepo wakati waarabu na wazungu walipokuja, kwani hao ndiop waliotuletea dini hizi tunazozifuata hivi sasa. Akaniambia kuwa hata kabla wao hawajaja, wazee wetu walikuwa wakiabudu katika nguvu fulani kuu (Mungu) na walikuwa na njia zao za kupeleka maombo ambayo yalijiwa kama vile ambavyo dini hizi ngeni zinavyofanya. Akaniuliza, kuna tofauti gani katika hayo kwa sababy wote wanaamini nguvu ile ile? Sikuweza kumjibu kwa ufasaha
   
 4. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wazungu walituletea dini zao ili watutawale, wakatutawala kweli. Hatukujifunza kutokana na makosa.
  Leo watawala wetu wanatumia tena dini kutufarakanisha, tupoteze muda wetu kwenye ugomvi na mabishano yasiyo na tija,
  wao wanaendelea kumega mkate wetu. Kweli tunafarakana kama wajinga. Hivi ni lini tutazinduka kutoka katika huu usingizi huu wa fikikra?
   
Loading...