jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,558
- 25,322
Wanabodi,
Kwanza nampongeza Mhe. Tundu Lisu Kwa kutokuwa muoga kuizungumzia dhana ya udikiteta Tanzania bila uoga, japo the way anavyoielezea anazungumza kwa style ya uropokaji hivyo kuonekana kama insane fulani, lakini ujumbe umefika.
Kwa vile Mhe. Tundu Lisu kwanza mwanasheria kisha ndio mwanasiasa, ametuasa tupaze sauti zetu kuupinga huu udikiteta kwa kupiga kelele. Naomba kutofautina na Mhe. Tundu Lisu katika hili la udikiteta, kuwa udikiteta haupingwi kwa Press Conference, kwa maandamano, kwa mikutano ya hadhara, kwa kupaza sauti na kupiga kelele.
Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia Mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3. (
Hivyo Lisu kama mwanasheria mbobezi, Mwenyekiti wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chadema alipaswa kwanza kutumia the legal local remedies available, kwanza kuuthibitisha huo udikiteta, zikishindikana ndipo sauti zipazwe ili kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.
- certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
- mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
- prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
- habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
- quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
- procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment) mtanisamehe sizijui Kiswahili chake.
No matter how good someone is, it's not necessarily he/she will always right, na kwa jinsi nilivyomsikia Lisu akimzungumzia rais Magufuli, kama Chadema ndio kinawategemea watu kama hawa kuuingiza ikulu, kiukweli Lisu atawaingiza chaka Chadema kama alivyowaingiza kwenye chaka la katiba.
Tundu Lisu is good in his own way ila sio mtu very dependable yanapokuja masuala nyeti yenye kuhitaji vichwa vilivyotulia. Aendelee kutumika kwenye amsha amsha lakini kwenye very serious issues zinazohitaji busara, Lisu anahitaji usaidizi wa wenye busara.
Chadema kuna tatizo kubwa la matumizi ya busara katika kauli za baadhi ya viongozi wake. Unaweza kukosoa kwa lugha ya kistaarabu na kwa unyenyekevu ukafikisha ujumbe vizuri zaidi kuliko kutumia lugha kali, machukizo, matukano na lugha isiyo ya staha.
Naomba kuwasilisha.
Paskali
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The ...
Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Nimetishwa, Kushitushwa na Kuogopeshwa na Kauli Hii ya Rais ..
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na ...
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa
Umetokota mbaya!
Compilation ya vi article vyako haifanyi hoja yako kuwa angalau na chembe ya ukweli.
Lissu yupo sahihi sana tena sana tu!
Kumbuka kuwa ameahtakiwa mahakamani kwa kumuita magufuli "dikteta uchwara"
Hapo ndio anaithibitishia jamii ya watanzania na ya kimataifa kwa ujumla kuwa huyu "magufuli" ni dicteta uchwara.
Ushahidi unazidi kuongezeka pale utawala wa dicteta uchwara unapomkamata na kumuweka ndani katibu mkuu wa chama cha upinzani kwa makosa ya kutekeleza majukumu yake halali kisheria na kikatiba majukumu ya kisiasa.
Shame on you Pascal Mayalla