Hoja ya tundu lissu na wingi wa wabunge wa ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya tundu lissu na wingi wa wabunge wa ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sulphadoxine, Apr 23, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa singida mashariki (chadema)Tundu lissu,wakati akijadili kipengele cha wajumbe wa kamati za maadili na nidhamu za mahakama.Lissu ambaye pia ni mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni alipendekeza wakuu wa wilaya na mikoa wasiwe wajumbe wa kamati za maadili na nidhamu za mahakama kwani kwa kufanya hivyo ni kupeleka watawala kwenye vyombo vya kutoa haki na hivyo kuingilia mgawanyo wa madaraka baina ya dola na mahakama.Kadhalika wakuu wa mikoa na wakuu wa wilya kimsingi ni makada wa ccm na hivyo unapowaweka kwenye vyombo hivyo vya kutoa haki ni kuingilia uhuru wa mahakama kwa kupeleka itikadi za chama chao,jambo lisilo kubalika na kwamba mambo ya kimahakama yanatakiwa kuendeshwa na wanasheria wenyewe bila kuingiliwa.
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Lissu ambaye kitaaluma ni mwanasheria alipendekeza wajumbe wakamati hiyo watoke ofisi ya mwanasheria mkuu,ofisi ya msajili wa mahakama kuu na kutoka chama cha wanasheria tanzania bara(TLS).Lissu sambamba na mbunge mwenzake wa chadema,Zitto kabwe,waliweka wazi kwamba wanashangaaa kuona chombo cha kutoa haki kinawekewa wanasiasa,tofauti na zilivyo kada nyinginekama wabunge wenyewe ambao kamati zao za maadili zinawahusu wenyewe,handishi na hata madaktari vivyo hivyo.Kwakweli hoja ya lissu kwa yeyote aliyezisikia zilikua zina mantiki na mashiko kuliko wale walio zipinga.Kwamba wanasiasa wanatafuta nini kwenye masuala ya mahakama?Nilishangaa mbunge Stellah Manyanya wa CCM akidai kwamba eti lissu anaeneza itikadi za chadema na kwamba anapoteza muda.Bila shaka jibu alilo mjibu lissu kuwa hajui alisemalo lilikuwa mwafaka.
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Sijajua hili ni swali ama ni ushauri ama ni pongezi!
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,923
  Likes Received: 2,071
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio unaweza kujua aina ya wabunge tulionao!
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hayo ni maoni tu binafsi.
   
 6. k

  kamimbi Senior Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijaona kama kuna kitu LISSU amekosea labda kama mtu ana interest binafsi, au waliyochomwa na kauli hii ni wale wenye magamba, maana kitu cha kushangaza ni pale wengine wanajivua magamba huku wengine eti ndo muda wa kuyavaa, i'm very sorry.:spy:
   
 7. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,648
  Likes Received: 5,242
  Trophy Points: 280
  Ha2na "AG" kwasasa ni "kiazi" 2 kipo bora tarehe imekua counted. Nilianza kumdisi jamaa toka ilpo letwa hoja ya mchakato wa katiba mpya, ilivyo mfikia jamaa aling'aka huku akionesha jazba kwa mbali utafikiri kaletewa talaka. Mwisho wa cku akatoa hoja eti hakuna haja ya katiba mpya labda ka inafanyiwa mabadililo. Kama mwana sheria msomi hakutakiwa kukurupuka na kunena vile. Hapo ndo'nilianza kuwa na mashaka naye, na kadiri cku zinavyojongea ndo'vumbi na moshi wa carbon dioxide linavyojizihirisha kwa kiasi gani limejaa kichwani mwa jamaa.
   
 8. B

  Bendera ya bati Senior Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu Stella Manyanya si mbuge wa viti maalum ccm?siwezi kushangaa kwa hoja aliyoitoa kwani hata hivi viti maalum sometimes vimeongeza sana vioja bungeni.Ni changamoto ya katiba hii mpya kuhakikisha linajadiliwa upya swala la wingi wa vit maalum katika bunge ndiyo maana mipasho na ndiyooooo......zinasikika katika bold kubwa kuliko siyo.Its so disgusting!
   
 9. gwino

  gwino JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ushauri mzur unaotolewa na upande wa upinzani imekuwa ngumu kufanyiwa kazi kwa staili hii hii inabidi next election 2ongeze idadi ya wabunge w upinzani ila ishu zenye maslahi ya taifa zisiwe zinapigwa chini kirahisi.
   
 10. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  tatizo wapinzani wanaonge ukweli, ukweli huo unauma, hivyo inabidi upingwe hata kwa hoja zaifu, lakini mpingaji ndani ya nafsi yake anatetemeka kama anasomewa hukumu...au kashikwa ugoni..
   
 11. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa ccm na wafuasi wao wengi wao hawapo kwenye chama kwa maslahi ya wanamchi,ndio maana wanageuza mchana kuwa usiku
   
 12. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Hoja ya Lissu imetufumbua kujua wabunge wetu wepi ni mchela na wepi ni pumba
   
 13. k

  kakini Senior Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  we unaonaje?
   
 14. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Naungana na wewe; viti maalumi viwe level ya madiwani tuu ili kina mama washiriki kufanya maamuzi huko kwenye "grass root". Bungeni wanatakiwa watu makini wanaoelewa "impact" ya kila muswaada wanaoupitisha.
   
 15. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kwanini usiwe na mawazo wale wa ndiyooooooo warudi upande wa upinzani?
   
 16. F

  Froida JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CCM ni makorokoto kama mwenyekiti wao wa Zamani Mkapa alivyowahi kutumia neno hilo kubeza upinzani,wanawake wamekalia Maaaaaaaaaaaaaaatako mbwata wanaume vitambi vinawatetema ni kupiga mambao yale kama vile wamepelekwa pale kama magari yanayokaa kwenye shooo ovyo kabisa nadhani wananchi wanaona upuuzi wao
   
 17. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa Bunge letu halina Spika makini kama alivokuwa Mhe. Sitta na kibaya zaidi hata AG mwenyewe ni BOMU la machozi kabisaaa!
  Hoja ya Tundu Lissu ilikuwa na mantiki na uzito wa kipekee na ndiyo maana Mtoto wa Mkulima Pinda ikabidi akubaliane na mawazo ya Tundu Lissu!

  Inasikitisha kuja kupitisha hoja hiyo Spika a.k.a RACHEL PRODUCT akarudia mara 4 kumhoji Pinda kama anakubaliana na Lissu. Hii ilitosha kuonyesha kuwa Makinda alikuwa tayari amepanga jibu la Pinda liwe hapana! Huu ni upuuzi ambaa inabidi ukomeshwe. Hatuwezi kuwa na spika ambaye yuko pale kwa ajili ya maslahi ya Chama chake na si maslahi ya Nchi. Pambaf kabisa!

  Mibunge yote ya Chama Cha Magamba/Mafisadi/Majambazi/Malimbukeni wakapinga hoja ya Lissu simply because ni Mpinzani! This is reslly nonsense. Inabidi kwenye Katiba tunayoitaka maswala kama haya yaangaliwe. Kuwa hata pale hoja ni ya upinzani lakini ni kwa maslahi ya Taifa basi kuwe na namna ya kuikubali na si kutumia ushabiki wa kijinga wa THE WINNER TAKES ALL!

  Tunatakiwa tuwe na Bunge lenye kuheshimika kama Mabunge mengine yanayoheshimika kama Bunge la Uingereza au USA ambako kuna mchanganyiko wa vyama vya siasa lakini wapinzani wanasikilizwa.
   
 18. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Namkubali Lisu sana na kabwe kwa hoja na jinsi wanavojiamini bungeni, huyo mbunge manyanya sijui manyege ni viti maalumu na alichofanya nikulipa fadhila ndio maana nimewaandikia wanene kibao nikitaka hii viti maalumu ifutwe kwenye katiba na ibakie ubunge wa kuchaguliwa, na wabunge wawe ni wa kanda na sio majimbo ili kupunguza ukubwa wa bunge, kuunganisha wizara 2 au 3 kuwa moja na kurudisha azimio la arusha ili watu wawajibike, hii itasaidia kupunguza matumizi ya serekali na pia kuongeza mapato kwa watendaji ili kuboresha ufanisi na kupunguza rushwa ndogondogo, nk   
 19. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Viti maalum wawepo ila wachaguliwe na wananchi kutoka vyama tofautitofauti mfano. Labda mkoa wa arusha unhitaji viti maalum labda vitatu wajitokeze wagombea kadhaa wa kike kutoka vyama tofauti wapigiwe kura na wananchi hapa tutapunguza ushabiki wa ajabu ajabu bungeni na tabia za kishankupe zinazoonyeshwa hasa na wabunge wa viti maalum haswa CCM ambao wampeata kwa kuhongwa na mabwana zao vigogo au wamevinunua uwakilishi wa kupewa haumuwakilishi mwananchi ila yule aliyekupa ndo maana huu upuzi unaendelea bungeni
   
 20. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shida kubwa la bunge la sasa hivi ni ushabiki wa kisiasa wa wabunge wa CCM na inferiority complex ya Spika wa bunge kwa vile hana sifa isipokuwa amewekwa kwa maslahi ya Magamba!! Spika ni kilaza, ana jaziba, na mropokaji anayepinga hoja yoyote ya wabunge wa CHADEMA bila kuangalia maslahi ya taifa mbele! CCM wana takiwa kujua kuwa ipo siku watakuwa wapinzani na kwahiyo sheria wanazopitisha kwa kudhani wanawakomoa CHADEMA na watanzania itakula kwao siku moja waliosema sheria ni msumeno hawakuwa wajinga. CCM inadhani nchi hii ni yao pekee yao ndio maana wanarithishana madaraka na watoto wao akina January, Nape, Rizwani etc. CCM kumbukeni tanzania ni nchi ya watu zaidi millioni 44, sio mali ya kikundi cha watu wachache!!!
   
Loading...