Hoja ya Pinda kutetea posho anavunja katiba ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Pinda kutetea posho anavunja katiba ya nchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Jan 28, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Huduma zinazotelewa na baadhi ya wabunge kwa wapiga kura wao haziwezi kuhalalisha kwamba serikali iwaongezee wabunge posho za ziada kwa kuwa wanaishiwa kutokana na kutoa misaada kwa wapiga kura wao. Katiba ya Jamhuri ya Muungano haina kifungu kinachoainisha kwamba kazi za Mbunge ni kutoa misaada na huduma za jamii kwa wapiga kura wake, ila ni mwakilishi, msemaji na mtetezi wa wananchi wa jimbo lake kwa serikali pamoja na jukumu la kuwa katika jopo la nchi la kutunga sheria.

  Kuna wabunge kadhaa ambao wamediriki kutoa misaada ya kiutu kwa wapiga kura wao ni kutokana na walicho nacho au mbinu wanazojua wenyewe kukokotoa misaada ambayo kama inasimamiwa kiufanisi inaweza kurudisha gharama hizo kwa vile huduma kama za magari ya kubeba wagonjwa si bure kwani wanalipia gharama hizo ili huduma hizo zijiendeshe.

  Lakini kujenga hoja ya kuongeza posho kwa wabunge kwa ajili ya kuhudumia wapiga kura wao ni kufuru kwa vile serikali inazo wizara na idara husika kwa kazi hiyo kila kona ya nchi. hali kadhalika kuna mashirika kadhaa ya kiserikali, dini na kimataifa yanayofanya kazi hiyo, ni dhana potovu kuwamegea watu binafsi wabunge pesa hizo kwa kisingizio ambacho kinapingana na mfumo wa majukumu na utendaji wa mihimili mitatu ya nchi yetu.

  Kwa upande mwingine serikali inatoa rushwa kwa wabunge na kuamsha ari ya wabunge kudai posho zaidi ili kuwa na akiba ya kutosha kuwarubuni wapiga kura wakati wa uchaguzi ujao. CCM kwa vile imezoea kushinda kura kwa kutumia pesa kuwahonga wapiga kura, hii ni mbinu ya kuwaandaalia mazingira wabunge wao kuwa na akiba ya kutosha kutoa rushwa uchaguzi mkuu ujao ili kujihakikishia viti vingi bungeni.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pinda alipoongea na waandishi wa habari majuzi kama utakubaliana na mimi nikwamba alisema hayuko tayari kugombea urais kwa vile ni kazi ngumu, na inaelekea anakusudia kustaafu, hapa hakuna kitu kingine zaidi ya kutetea kujilimbikizia mali kwa ajili ya kustaafu kwake ingawa ana pesheni nzuri tu kutokana rekodi ya utendaji serikalini muda mrefu na kuwa Waziri mkuu wenye kipato cha juu sana, ubinafsi utamwaibisha sana mzee huyu.
   
 3. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kumjadili Kilaaza Pinda ni sawa na kujadili kwa nini kichaa anatembea uchi.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa vile ana nafasi muhimu katika mfumo wa utawala wa nchi yetu na bado yuko active, hatuwezi kukwepa, madhara yanayojilia yanatukumba sote, tumjadili tu.
   
 5. N

  Njele JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi Pinda ana washauri au huwa anaamua tu kufanya vitu kwa utashi wake?
   
Loading...