Hoja ya Muungano yalifunika baraza la wawakilishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Muungano yalifunika baraza la wawakilishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 26, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  [h=1][/h]Posted on June 26, 2012 by zanzibaryetu


  SUALA la Muungano limezidi kutawala mijadala katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea huku baadhi ya wajumbe wakitamka wazi kuwa hawataki Muungano. Katika kikao hicho ambacho tayari kimepitisha bajeti kuu ya serikali ya Zanzibar wajumbe wa baraza hilo jana walijadili bajeti ya ofisi ya makamo wa pili wa rais wakitaka serikali isimamie kupata uhuru zaidi wa kiuchumi katika muungano.
  Ofisi ya makamo wa pili wa rais ndio inayotambulika kuwa msimamizi mkuu wa shughuli za serikali ndani ya baraza la wawakilishi.
  “Mheshimiwa Naibu Spika mimi niseme wazi kwanza kwamba sitaki muungano na katika kitu ambacho nakichukia sana basi ni huu muungano maana kwa miaka 48 ya muungano huu kila siku tunaambiwa kuna kero wala hazitatuliwi basi ni uvunjike tu” alisema Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma.
  Juma alisema kupigania haki ya Zanzibar haimaanishi chuki katika muungano na kwamba muungano uliyopo ni wa nchi mbili huru ambazo lazima kuwepo na haki sawa kwa pande zote mbili.
  Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kitope (CCM) Makame Mshimba Mbarouk alisema “Lazima mheshimiwa makamo wa pili wa rais tuamke muungano huu, siwo…tunataka maslahi ya Zanzibar na tunataka haki zetu zote kuanzia mapato ya gesi. Nitazuwia bajeti hii mpaka niambiwe katika accounti ya Zanzibar imepata kiasi gani kwa mapato ynayotokana na gesi maana ni haki yetu” alisema Mbarouk.
  Abdallah Juma Abdallah Mwakilishi wa Jimbo la Chonga (CUF) alisema viongozi wa serikali na vyama wamewekwa madarakani na wananchi hivyo sio sahihi kubeza maoni ya wananchi ambayo hawautaki mfumo huu wa muungano na kuahidi kusimama pamoja na wananchi wa jimbo lake iwapo waamua kuukataa.
  “Kiongozi yeyote kuanzia rais, wabunge na hata sisi wawakilishi tumewekwa hapa kwa kuchaguliwa na wananchi na tunasimama kuwasilisha maoni ya wananchi sasa ikiwa wananchi watasema hawataki muungano, mheshimiwa naibu spika lazima tusimame nao” alisema Mwakilishi huyo na kuongeza.
  “ Mimi kama mwakilishi wa chonga nasema wananchi kama watasema hawataki muungano basi nitasimama nao na nitakuwa bega kwa bega na kwa sababu wamenichagua kwa kuniamini na pia nahitaji tena kurudi katika nafasi hii na nikidharau maoni yao au matakwa nayo hawatanirejesha tena” alisema Abdallah.
  Mwakilishi wa nafasi za wanawake Asha Bakari Makame (CCM) kwa upande wake aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kutoka CCM na CUF kwamba wanadhamana kubwa ya kuwatetea wazanzibari bila ya kuhofia nafasi zao na kwamba wazanzibari wanawatazama wao kwa kuwaamini.
  “Mheshimiwa naibu spika ni CCM na CUF pekee tuliyopo humu ndani wananchi wanatuamini na lazima turejesha imani kwa wananchi wetu ikiwemo suala kuu la kutetea Zanzibar ndani ya muungano…kero gani hizi zisizokwisha?” alihoji Asha ambaye aliwahi kuwa waziri wakati wa SMZ .
  Asha Bakari ambaye ni naibu mwenyekiti wa umoja wa CCM Tanzania (UWT) alisema ni umoja na mshikamano miongoni mwa wazanzibari ndio silaha pekee itakayoweza kuwavusha wazanzibari katika kudai maslahi yao ndnai ya muungano.
  “Mimi siogopi chochote na kwa umri huu tena naona lolote litakalonifika ni sawa tu lakini nawaambia wenzangu kwamba tuiteteni Zanzibar na tusiwe na woga maana wengine wamezowea kututisha” alisema kwa kutoa tahadhari.
  Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alisema serikali ya Zanzibar inafanya makosa makubwa ya kuridhia kila kitu ambacho kinatolewa na serikali ya muungano.
  “Ni muda mrefu wimbo ndio huo huo wa ahadi ya kushughulikia kero za muungano na kero zenyewe hazishi …kwa sababu hata hizo kamati hazipo kisheria za kutatua kero” alisema.
  Jussa alitaka viongozi wa serikali kuwaunga mkono wananchi katika madai yao ya msingi kwa kuwaelekeza nini waseme wakati wa kutoa maoni ya katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na kwamba bila ya kutoa muongozo wananchi watababaika.
  “Mimi nina imani kubwa na serikali yangu ya umoja wa kitaifa na ninaipenda lakini naomba itoe msimamo hapa katika kuwaelekeza wananchi wakadai nini wakati wa tume itakapokuja kukusanya maoni” alisema Jussa na kupigiwa makofi na wajumbe wenzake.
  Aidha mwakilishi huyo aliwataka wananchi na viongozi wa siasa kutokuchanganya misimamo ya siasa pamoja na dini katika kutoa maoni kwani inaweza kuharibu na kuwagawa wazanzibari.
  Awali akiwasilisha hutuba ya bajeti ya makamo wa pili ya kuomba kuidhinishiwa shilingi billioni 12.3 kwa mwaka wa fedha za 2012/2013 Waziri wa nchi Ofisi hiyo Mohammed Aboud Mohammed alisema juhudi zimekuwa zikiendelea katika kutatua kero za muungano na kwamba wajumbe wa baraza la wawakilishi wawe wavumilivu.
  MWISHOUJENZI WA BANDARI
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema itatumia kiasi cha dola za kimarekani 400 millioni kwa ajili ya mradi wa bandari ya Mpigarudi Visiwani Zanzibar.
  Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Gavu alipokuwa akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliyetaka kujua mradi wa ujenzi huo utagharimu kiasi gari cha fedha.
  “Kwa gharama ambazo zinakisiwa kulingana na ‘concept paper’ ya wizara, mradi huu usingeweza kuzidi USD$ 400 millioni.” alisema Naibu Waziri Alisema hata hivyo kwa vile gharama hizo zilikisiwa miaka mitano iliyopita ingewezekana akuweka ongezeko la asilimia 10% ambapo mradi usingezidi dola za kimarekani millioni mia tano. (USD$ 500).
  Akijibu suali la la fedha hizo zitatokea wapi na zina masharto gani, Gavu alisema fedha hizo hazijapatikana na hivyo masharti ya fedha yasingeweza kupatikana vile vile.
  Awali Jussa alitaka kujua bandari hiyo iliyokusudiwa kujengwa ambayo ni ya kisasa pendekezo hilo limefanyiwa kazi kwa kiasi gani na limefikia hatua gani, ambapo Naibu Waziri alisema ni ya ujenzi huo upo na serikali inaendelea na mchakato wake.
  Akizungumzia pendekezo hilo Naibu alisema linaendelea kufanyiwa kazi na kwa sasa serikali imeshakamilisha upembuzi yakinifu uliofanywa na kampuni ya CRB- ya China.
  Naibu huyo aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba baada ya kuipitia wataalamu wameona bei iliyopendekezwa na kampuni hiyo ni millioni 800 fedha za kimarekani.
  “Millioni 800 ni nyingi sana na hiyo bado serikali imo katika kutafuta njia mbadala ya kufanikisha suala hili” alisema Naibu waziri huyo.
  Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba licha ya baadhi ya wajumbe wameonesha wasiwasi wao juu ya kampuni ya kichina lakini bado serikali ina matumaini na ufanyaji wa kazi ya kampuni hiyo kwa mujibu wa mkataba waliofunga.
  “Mheshimiwa mwenyekiti haina maana kwa kuwa kampuni moja ya kichina imefanya vibaya na hii itakuwa imefanya vibaya kwa zile kampuni ambazo zimefanya vibaya za kichina ni nyengine lakini hii ni nyengine na bado serikali ina matumaini ya kufanya kazi yetu vizuri” alisisitiza naibu huyo.
  MWISHOUKOSEFU WA WALIMU YA SAYANSI
  WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imekiri kuwepo kwa uhaba wa walimu wa sayansi katika visiwa vya Unguja na Pemba.
  Naibu Waziri wa wizara hiyo, Zahra Ali Hamad aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kufuatia suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua ni sababu gani zinazochangia kuwepo kwa uhaba wa walimu wa sayansi nchini.
  Zahra alisema uhaba wa walimu wa sayansi katika skuli za Unguja na Pemba unatokana na wanafunzi wengi kutofaulu masomo ya sayansi katika mitihani ya kidato cha nne na kidato cha sita na hivyo kupelekea vijana wachache wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya ualimu kwa masomo ya sayansi.
  Akijibu suali la kwa nini wizara ya elimu imeshindwa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo Zahra alisema “Ni kweli waheshimiwa wajumbe wizara iliahidi kulipatia ufumbuzi suala hili lakini ufumbuzi huo hauwezekani kupatikana mara moja na inahitaji muda wa kuweza kulitatua tatizo la upungufu huo”.
  Alisema wizara imepata vibali vya uajiri wa walimu wapya katika mwezi wa Aprili 2012, amabpo wizara iliajiri walimu 197 wenye shahada na stashahada mbali mbali wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi.
  Katika mwezi wa juni 2012 alisema wizara imepata kibali chengine cha uajiri wa walimu 111 wenye shahada na stashahada za ualimu wakiwemo walimu 48 wenye shahada ya kwanza ya masomo ya masomo ya sayansi.
  Naibu waziri huyo alisema kukosekana kwa walimu hao kunaweza kuchangia katika kushindwa kwa wanafunzi kufnaya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha nne na cha sita.
  Aidha kushindwa kwa wanafunzi hao pia kunachingiwa na wanafunzi kutopendelea kusoma masomo ya sayansi kwa dhana ya kuwa ni masomo magumu au wanafunzi huliogopa somo la hisabati ambalo ndilo somo la msingi.
  “Ni kweli skuli ya Muyuni na skuli nyengine zina uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi. Uhaba huu unatokana na wanafunzi wengi kushindwa kufaulu masomo yao na kujiunga na vyuo vikuu” alisema Naibu huyo.
  Zahra alisema wengi wa waombaji wa mafunzo ya ualimu wamefaulu katika masomo ya sanaa kuliko sayansi na hivyo masomo ya sayansi hukosa walimu na tatizo hilo ni sio kwa skuli za zanzibar peke yake bali ni Tanzania nzima.
  Hata hivyo alisema wizara imeandaa mafunzo ya ualimu kazini kwa walimu wasio na sifa za kufundisha masomo ya sayansi ili kuinua uwezo wao na hatimae waweze kudumu kuyafundisha masomo hayo.
  Akizungumzia mikakati ya wizara yake katika kuhakikisha tatizo hilo linapungua Naibu Waziri alisema mpango wa wizara yake ni kuajiri vijana waliomaliza kidato cha sita na kufaulu masomo ya sayansi ili kusaidia kupunguza uhaba wa walimu wa sayansi.
   
 2. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  bora muungano uvunjike muwachukue wenzwnu wanaokaa bara. Sis tumewachoka huku. Sijui mtawaweka wapi nxhi ywnyewe kiduchuuu. Na hao waarabu wakiwachoka mtaomba tena muungano.
   
 3. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hili nalo Litapita,........
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huu ni upepo tu, utapita.
   
 5. H

  Hydrobenga JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 1,124
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wewe nna wasiwasi kichwani umejaa majivu ..... watu wanadai chao wewe unaleta habari za waarabu....tatizo lako udini umekujaa....hawa wazungu ambao unawaona watu huku Tanaganyika wametusaidia nini? zaidi ya kuiba madini yetu na kutia sumu kwenye maji ya kunywa huko vijijini...au kwa sababu ni wakristo wenzako umeamua kuwapotezea ?
   
 6. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio utakapojua kuwa wanachoma makanisa ni Serikali mbuzi ya Zanzibar, yaani siku ya tarehe 26 ambayo ilipangwa kuwa siku ya fujo kubwa ndio wawakilishi wao nao wanasisitiza ndani ya baraza kuwa hawautaki muungano? Kama sio kuunga mkono Uamsho ni nini? Thanks JWTZ na Polisi jana walijaa kila sehemu ya Zanzibar ndio maana mashog a hawakuweza kusanyika
   
 7. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo jimbo la Wawi lina wabunge 2, Hamad Rashid na Salehe Mansour Juma. Kwa hili afadhali uvunjike misri naona tunaibiwa tu watanganyika, majimbo yenyewe yanaukubwa kama mbegu ya chungwa afu haya yanapewa bajeti sawa na Jimbo la Kalenga lenye vijiji 62 huu ni wizi wa waziwazi tumeuchoka muungano hii ni sehemu ya ufisadi. Bora ufe
   
 8. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [​IMG][TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 27 June 2012 09:50 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  Wananchi wakishangilia viongozi wa Uamsho

  Na Mwandishi Wetu
  WAKATI tukielekea katika mchakato muhimu wa kutoa maoni yetu juu ya uundwaji wa Katiba mpya ya Tanzania, ni wazi kuwa jambo litalokuwa na mjadala mkubwa , hasa kwa upande wa Zanzibar , ni suala la Muungano. Hii ni kutokana na sababu kuu tatu. Kwanza , kwa vile Wazanzibari kama ilivyo kwa Watanzania Bara, hawajahi kupata fursa ya kuutolea maoni na ridhaa Muungano huu kwa ujumla wake , muundo wake na uendeshaji wake – na kwa vile umedumu hivyo ukielekea kutimiza nusu karne, hii ni fursa muhimu ya kuufanyia tathmini yakinifu kwa kuzingatia wakati mpya tulionao , mahitaji tuliyonayo na mazingira ya kisiasa na kiuchumi yanayotuzunguka wakati huu.
  Pili ni kutokana na ukweli kuwa Wazanzibari , kwa mujibu wa muundo wa Muungano huu wao wana mfumo wao kamili unaoongoza mambo yao yote yasio ya Muungano – wana Katiba yao, Serikali yao, Mahkama zao, Bunge lao (Baraza la Wawakilishi), Vikosi vyao vya Ulinzi, Serikali zao za Mitaa nk – hivyo kwa upande wa Zanzibar mjadala wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwao utajikita zaidi kwenye suala la Muungano tu, nje ya Muungano wao wana yao, na nje ya Muungano yanayobaki katika Katiba hiyo ni ya Tanzania Bara tu.
  Tatu ni kutokana na ukweli kuwa Wazanzibari walio wengi wanaamini kuwa Muungano katika muundo wake huu umejengeka katika udhaifu wa kimaumbile na hivyo umepelekea kudumaza maendeleo na mustakbali wa Zanzibar katika nyanja takriban zote- malalamiko yao ni mengi mno .
  Watakwambia Zanzibar imepoteza hadhi yake, Rais wake aliyepokelewa kwa heshima kubwa Umoja wa Mataifa na kuwa na kiti chake sambamba na mataifa yote ya ulimwengu huu kabla ya Muungano na wakati wa Muungano akathaminiwa kwa kufanywa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano , leo kafanywa Waziri asie na hadhi yoyote ndani ya Baraza la Mawaziri la Tanzania.
  Watakwambia Zanzibar haina hadhi ya kujiunga hata na Taasisi tu za Kimataifa na hapa watakukumbusha mkasa wa OIC, jumuiya ya Kiislamu yenye kujikita katika kutoa misaada ya kiuchumi na kijamii na iliyo na wanachama nchi ambazo idadi ya Waislamu nchini humo ni chini ya asilimia kumi kama Uganda na Msumbiji.
  Zanzibar ina Waislamu zaidi ya asilimia 97 hivyo haiwezi kuwa na haja ya kujiunga na taasisi za kiislamu kwa kutangaza uislamu bali ni suala la maslahi ya kiuchumi na si suala la udini.
  Lakini kama ni udini watakuuliza mbona Vatican ina Ubalozi Tanzania? Watakwambia juhudi za wanamichezo wa Zanzibar pamoja na msaada wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili waweze kujiunga na FIFA na hivyo kunufaika na maslahi ya Shirikisho hilo zilivyoshindikana, kisa muundo wa Muungano!
  Watakwambia wanavyotozwa kodi mara mbili na taasisi hiyo hiyo kwa bidhaa hizo hizo pale wanapopeleka bidhaa hizo Tanzania Bara.
  Watakwambia kuwa ukweli ni kuwa mfumo wa Muungano ndio umeifanya Zanzibar leo kuwa tegemezi kwa soko la Bara vinginevyo kama ingekuwa na uhuru wa kimaamuzi katika mambo ya kodi na sera za kifedha Zanzibar ingeweza kuwa kituo kikuu cha kibiashara na kamwe wasingefungika na soko finyu la Tanzania Bara tu.
  Watakusimulia kuwa hata hivi punde miaka ya karibuni ilipotokea msukosuko wa kiuchumi duniani na Benki Kuu ya Tanzania kutoa fedha kuokoa uchumi usiporomoke, Zanzibar haikuambulia kitu ingawaje hio ni Benki ambayo mbali na kuwa ni ya Muungano lakini katika kuanzishwa kwake Zanzibar ilitoa mtaji wa asilimia 11.
  Watakwambia benki hiyo huwa mstari wa mbele kiuwezeshaji kilimo kwa kunyanyua mazao ya korosho, pamba na kadhalika, lakini haifanyi hivyo kwa karafuu. Watakusimulia mengi juu ya kero katika usimamizi wa uchumi na rasilimali, masuala ya kodi na fedha , misaada kutoka nje, mapato na matumizi yanayohusiana na Serikali ya Muungano, na mengi mengineyo. Kwa ufupi watakupa msururu wa kero mpaka utajisikia kukereka.
  Hivyo kwa vigezo kadhaa wa kadhaa mjadala juu ya Muungano ndilo kiini cha mjadala wa Katiba kwa upande wa Zanzibar ; na kwa msingi huu hapana budi Wazanzibari waitumie fursa hii kwa ujasiri mkubwa, umakini na zaidi ya yote kuweka mbele maslahi ya Zanzibar na sio maslahi binafsi, ya makundi au kivyama.
  Ni wazi wapo wataosukuma ajenda zao katika mjadala huu kwa maslahi yao binafsi hasa ya kisiasa hata kuweza kupotosha mambo , waiangamize nchi na hata itoweke kabisa ili wao wafaidike na maslahi yao binafsi tena ya muda mfupi bila kujali mustakbali wa vizazi vijavyo.
  Marekani na Ulaya yanatamba duniani kwa sababu yameungana. Hivi tujiulize ni kweli mataifa haya yameendelea kwa sababu ya Muungano tu?
  Mataifa ya Ulaya na Marekani yana historia refu ya kiuchumi duniani tokea enzi za biashara ya utumwa na ukoloni, yana rasilimali kedekede, yameweza kusimamia ipasavyo chumi zao, yamekuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kila fani ya kimaisha, yameweza kunufaika hata na chumi za nchi nyengine kwa mifumo ya kifedha na kibiashara ya kinyonyaji ya kiulimwengu waliyoitandaza, uwezo wao mkubwa wa sayansi na teknolojia, ubabe wao wa kijeshi wanaoutumia kwa lengo la maslahi ya kiuchumi , jinsi walivyowekeza katika elimu na jinsi walivyoendesha nchi zao kwa misingi ya kidemokrasia.
  Kwa wasaka madaraka tatizo kubwa kwao katika Muungano huu watakwambia kuwe na kupokezana Urais ili mara ijayo iwe ni zamu ya Mzanzibari ili ndoto zao zitimie lakini hawawezi kuwa na msaada wowote wa kiuchambuzi yakinifu ambao utaleta maslahi kwa wananchi .
  Lakini hata tukikubaliana kuwa muarobaini wa matatizo yao (Marekani na Uingereza) ni huo Muungano wao tujiulize je, muungano wao unafanana kimuundo au kwa namna yoyote na huu wetu?
  Wanasheria mahiri wote wanakubaliana kuwa hakuna muungano wowote duniani wenye muundo kama huu na huishia kuuita muungano wa kipekee.
  Kwa kawaida Muungano hutegemewa uongeze nguvu kwa walioungana na sio kupototoa nguvu zote za upande mmoja na upande huo ukabaki bufuru tupu (kwa maneno ya Professor Shivji).
  Katika muundo huu Zanzibar imepoteza nguvu, uwezo na madaraka yake yote kama nchi na yametumbukizwa katika himaya ya Tanganyika lakini Tanganyika ilipoteza jina tu lakini nguvu , uwezo na mamlaka viliongezeka.
  Lakini kuufananisha muungano wa Zanzibar na Tanganyika na ule wa Jumuiya ya Ulaya au ule wa Marekani ni kufananisha tembo na chura . Sawa wote ni wanyama. Lakini fanya uchambuzi wa hali zao uone tofauti zao!
  Itaendelea wiki ijayo…

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 9. b

  bdo JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  kazi kwelikweli......kila lenye mwanzo lina mwisho, akili zao zote zipo sawa, ila jengo lao zuri
   
 10. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama kweli sio maneno matupu, wangekwamisha hiyo bajeti ya makamu wa Rais hadi Muungano uvunjike! Kelele za chura hazimuzuii ng'ombe kunywa maji.
   
 11. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Muungano saizi ni bao la kisiasa!! WANALITUMIA wote!! Cha msingi ni kukaa na kukubaliana hakuna haja ya kuleta dharau au kukebehiana!
   
 12. a

  abousalah2 Member

  #12
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe acha kutoa stori za uwongo nani wamejaa huku , muungwana hafedheheki kama ni uamsho kila siku mihadhara iko njoo uwanja wa malindi! sawa hii ni serkali mbuzi lakini serikali nguruwe na mbwa hatutoikubali kwetu! ama kweli umesahau nani amehalalisha ushoga kama sehemu ya ibada! tuliungana kwa hiyari tutauvunja kwa hiyari! uarabu ni kasumba zenu tu kwani hao wazungu sio waliochukua zahabu zenu kubadilishana gololi! aliyemo yumo na asiyekuwemo haingiii.
   
 13. a

  abousalah2 Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  usiloweza kulila usilitie ila una maanish awwkilishi wetu ni watu wajinga? fuatilia prifile zao ! acha kukuripuka! utaadhirika mno! huu ni uwongo na dharau hebu ni kuulize ni mtanganyika gani aliyeingia katika orodha ya wanazuoni bora mia duniani? wazanzibari tunao mmja ni pro IDRISA ABDALLAH RAI fuatilia acha kuengea kwa chuki!
   
 14. a

  abousalah2 Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama hujui kusema usijilazimishe kusema! wazanzibari huko si omba omba kama mulivyo nyinyi huku , watu wanashughuli zao! au umesikia mzanzibari kufungwa kwa wizi huko? njoo huku utajionea idadi yenu! fikiri ndipo utende, usijifanye wjua kumbe kilaza! nenda huko sauzi utajionea! mm binafsi huku najionea shida kuitwaMTZ
   
 15. BabuK

  BabuK JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 1,847
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hakuna jambo ZURI kama kuwa na subira na kufanya maamuzi muhimu kwa wakati muafaka.... HAKUNA JAMBO BAYA kama kuwa kama bendera ifuatayo upepo. Kila upande una hoja lakini kubwa zaidi ni kufuata sheria na taratibu zilizopo maana kwenye demokrasia ya kweli tunafuata MAAMUZI YA WENGI HUKU TUKILINDA MASLAHI YA WACHACHE.

  Kama hoja ni mwuungano kwanini hao wakereketwa wa kuuvunja wakachome makanisa.. kwanini wasiende kuichoma ikulu ya Zanzibar???

  Kama hoja ni muungano kwanini tushambuliane kwa misingi ya dini, au hivi karibuni kuilaumu serikasli iliyopewa mtihani na mataifa ya magharibi juu ya kukubali haki za mashoga? takwimu za miaka mingi zilionyesha kwamba zanzibar na pemba zinaongoza kwa masula ya ushoga hata kabla ya tamko la kututaka tutambue haki za mashoga.

  Kama ni mwuungano kwanini tulumbane juu ya mali zilizopo ardhini ..mafuta na gesi.... Hapa mimi napata kigugumizi cha mawazo! Inaelekea kuna msukumo fulani ambao bado nautafiti.

  Kama Mwuungano mbaya Bajeti ya maendeleo ya Zanzibar inachangiwa na Serikali ya Mwuungano.


  Kama ni mwuungano kwanini tusifuate utaratibu.. Tume ya kukusanya maoni ya Katiba mpya imesema itachukua inputs zinazohusu Mwuungano.
  Waasisi wa Muungano wajijenga hoja kwanini tufanye Mwuungano.. Na tukiona unapitwa na wakati basi Tusitaka Muungano tujenge hoja na tufuate taratibu..HUU NDO USTAARABU NA HUU NDO UUNGWANA. kinyume cha hayo hoja za wapinga Mwuungabno hazitachukuliwa kwa uzito na zitaonekana za Kihuni!
  Bado inanitatiza kwamba wakati matafaifa makubwa yanaungana na kuleta mwuungano wa kiuchumi na kiutawala ..sisi Tanzania ambao ndo mfano wa Mwuunganio Afrika tunafikiria kuuvunja kwa sababu za tende, mafuta, nguruwe,mbuzi.dini au nyingine zozote!

  HAWA WAWAKILISHI WASIO NA MSIMAMO WA KUTETEA KATIBA WALIYOAPA KUILINDA NADHANI WALIKOSEA NJIA WAONHYESHWE MLANGO WA KUJIUZULU NDANI YA BARAZA!!!!
  Tuache kucheza ngoma ya kitoto isiyokesha!!!! Tufunguke kimawazo na tuone dunia inavyokwenda.
   
 16. m

  mugosha JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 570
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
   
 17. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo ndiyo mafundisho ya bwana yesu kutukana watu ???
   
 18. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 19. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu usitoe povu bure!
  Kikao cha wawakilishi kinaendelea, washwishini wapige kura kuukataa muungano ili mkate mzizi wa fitna.
  Na yule sheikh Farid ulitaka "kumuua" hajambo?
  We kweli kichaka.
   
 20. m

  mr.dominick JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sisi huku Tunganyika tumo tunawashughulikia hawa madaktari uchwala wanaotumiwa na waarabu kuleta usultani Tanganyika

  Maana tunaona wanatumiwa na UAMSHO na kidogo tumempa kafunzo yule anayejifanya ni kiongozi wao
   
Loading...