Hoja ya "Muungano wa Mkataba" ni Muflisi!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Mtu akikuambia jambo la kijinga na anajua na wewe una akili nawe ukalikubali atakutumikisha. Nimebadili kidogo tu kauli ile ya Nyerere kuwa "Mtu mwenye akili akikushauri jambo la kipumbavu akijua nawewe una akili ukalikubali atakudharau". Kuna hoja inatolewa na baadhi ya watu Zanzibar ambao wanaamini wanatoa hoja ya kiakili pale wanapopendekeza kuwa wanataka Zanzibar itoke kwenye Muungano wa sasa ili iwe "dola kamili" na baadaye ufatiwe "muungano wa mkataba" na Tanganyika.

Katika hili kama maji machafu ya maporomoko wengi wamekumbwa. Wamekumbwa vijana, wamekumbwa wazee na wamekumbwa wasomi na wasio wasomi. Wengi wanaimba wimbo wa "Muungano wa mkataba" ambao kibwagizo chake hakipo zaidi ya 'Zanzibar kwanza'. Hoja hii imeanza siyo tu kukubaliwa na watu wengine wenye akili lakini inaonekana ndio hoja pekee inayoweza kutolewa na kuridhisha watu. Naomba kupendekeza kwa heshima na taadhima kuwa hoja hii ni ya kipuuzi, haina mantiki na inapaswa kukataliwa na watu wote wenye akili.

Hoja Mbili tofauti

HOJA YA KWANZA - 'DOLA KAMILI KWANZA'
Bahati mbaya sana watoa hoja hawa wamejaribu kwa kutumia akili kuchanganya hoja mbili zisizohusiana kabisa. Hoja ya kwanza ambao wanaitoa na labda ina nguvu zaidi kuliko ile ya pili ni kuwa "tunataka Zanzibar yetu kwanza, dola kamili, ikiwa na mamlaka yake yote". Hoja hiikwa Kiingereza inaweza kufupishwa kwa maneno mawili tu "FULL SOVEREIGNTY" yaani "HAKIMIYA KAMILI".

Katika historia ya dunia jamii za watu zinapodai 'DOLA KAMILI' wakimaanisha dola yenye hakimiya kamili manake ni kuwa jamii hizo zinatawaliwa na wengine, au hakimiya yake haipo ndani yake. Kwa mfano, baadhi ya mataifa yana uhuru wote wa ndani lakini hakimiya iko kwa Malkia wa Uingereza ambaye huitwa 'SOVEREIGN' manake ni mkuu wa dola hiyo. Nchi kama Canada, Australia na nyingine 13 ziko namna hii. Ziko huru kwa kila kitu lakini zinamtambua Malkia wa Uingereza kama Malkia wake. Baadhi ya hizi sasa zinataka kwenda kwenye mfumo wa Kijamhuri na kutoka kuwa chini ya Malkia.

Marekani ni mfano mzuri wa nchi ambayo kwa muda mrefu ilikuwa chini ya Mfalme wa Uingereza; walitawaliwa na watu walioko London. Harakati za Mapinduzi ya Marekani zilitokana kwa kiasi kikubwa na mengi ya malalamiko ya koloni la Marekani kupuuzwa na Mfalme George III na hivyo kusababisha vita vya mapinduzi. Wamarekani katika Azimio lao la Uhuru walieleza kabisa kwanini wanaamua kuachana na utawala wa mfalme na hivyo kujitangazia uhuru wao milele daima. Licha ya Uingereza kujaribu kuzima mapinduzi Marekani ilijitangaza huru July 4, 1776. Ilipata kuwa dola kamili.

Historia hata hivyo inaonesha kuwa ukaribu wa Uingereza na Marekani haukuvunjwa na vita hivyo kwani hadi leo hii udugu wao, ujamaa na ushirikiano wao unadumu kupitia makubaliano mbalimbali ya kimataifa. Makubaliano hayo hata hivyo siyo muungano wa "mkataba"; bali ni makubaliano (treaties) kama yalivyo makubaliano mbalimbali kati ya nchi mbili. Leo hii hakuna nchi rafiki kwa Mwingereza kama Marekani na hakuna nchi rafiki kwa Mmarekani kama Uingereza. Hakuna Muungano wa Mkataba baina yao isipokuwa ushirikiano wa karibu unaotokana na historia yao moja.

Wazanzibari hivyo wanaweza kabisa kudai na kutoka kwenye Muungano huu na kuwa dola kamili. Hili wanaweza kulifanya bila kudai "muungano wa mkataba". Hawana haki nyingine ya kudai "muungano wa mkataba" haki yao ni kudai "dola kamili tu". Watoke kwanza na wakishatoka na kuunda utawala wao na serikali yatafuata mambo ya makubaliano mbalimbali na Tanganyika au na nchi nyingine yeyote ile ambayo viongozi hao watataka.

Kudai kutoka nje ya Muungano ni haki kama ilivyokuwa kwa baadhi ya nchi tena kwa utaratibu mzuri tu; Wazanzibari walete mswada kwenye Bunge lao (Baraza la Wawakilishi) wa kusimamia kura ya maoni na waulizwe tu swali moja jepesi "JE UNATAKA ZANZIBAR IJITOE KWENYE MUUNGANO NA TANGANYIKA IFIKAPO JANUARI 1, 2014?" Na kama asilimia kubwa ya watu (zaidi ya 2/3) wakisema "Ndiyo" basi vipengele vingine vya sheria hiyo vitaanza kutekelezwa ikiwemo kuweka utaratibu wa kuachana na Tanganyika, kugawana mali (haiwezi kuwa nusu kwa nusu isipokuwa kama katika kila gharama kila upande ulichangia nusu kwa nusu) na kupeana majukumu mbalimbali ili kuhakikisha kujiondoa kwa Zanzibar kunakuwa katika hali nzuri (smooth) na isiyoleta matatizo yoyote visiwani humo.

Hata hivyo sheria hiyo iweke wazi pia maana ya kukataa kujitoa ni nini? Kwamba mfumo wa Muungano utaendelea kuwa ulivyo sasa ambao ni 'nchi moja serikali mbili' ama "nchi moja serikali moja'. Wazanzibari wajue katika kura hiyo kusema ndio ni kutoka kwenye Muungano BILA kufuatiwa na "mkataba" wowote mwingine.

Watanganyika hawatakiwi kuamua hatima ya Zanzibar
Mojawapo ya maswali ambayo yanaulizwa na ndugu zetu ni kuwa "kwanini nyinyi Tanganyika mmetung'ang'ania hamtaki kutuachia?" au "Kwanini Tanganyika inaogopa Zanzibar kuondoka". Kwa upande wangu - na labda nawakilisha mawazo ya wengine - Watanganyika (Watanzania Bara) hawajali kabisa kama Zanzibar itatoka kwenye Muungano kwani hawajali upande mwingine kama Zanzibar ipo. Kwao uwepo wa Zanzibar ndani ya Muungano haubadilisha maisha yao kwa namna yoyote ile. Mtu wa Mara, Singida, Mbeya, au Kagera hatosikia chochote kama Zanzibar itajitoa kwenye Muungano na hivyo hawafikirii sana. Kitu pekee ambacho Watu wa bara watakisikia na Mwalimu alikisema vizuri kwenye ile hotuba yake ya "Nyufa" pale Kilimanjaro Hotel mwaka 1995 ni kuwa watanganyika watajikuta wamepigwa na butwaa "yaani Wazanzibari kweli wamejitoa?" Watakuwa wapweke kwa muda kwa sababu Tanzania kama Muungano wa nchi mbili haitokuwepo tena.

Lakini kama Nyerere alivyosema hata hivyo Watanzania bara "watabaki salama". Mshtuko wa Zanzibar kutoka utapita kama ukungu wa asubuhi. Na kuna uwezekano mkubwa watu wa bara wakaamua kuendelea kujiita Watanzania kwani hawana tatizo na utambulisho wao; kwani kwao Tanzania ni njozi ya umoja iliyounda taifa letu.

Ni kwa sababu hiyo Tanzania bara haipaswi kabisa kuamua Zanzibar inabakia au haibakii. Mwezi Novemba wananchi wa visiwa vya Puerto Rico walipiga kura kama wanataka kuwa dola kamili au wawe jimbo la 51 la Marekani. Kwa wingi wao waliamua badala ya kuwa nchi huru kamili wawe jimbo hilo. Wamarekani wote hawakuulizwa Puerto Rico iingie kama jimbo au ibakie. Ni suala la Puerto Rico siyo suala la Marekani nzima.

Mwezi Oktoba Waziri Mkuu wa Uingereza na Waziri Kiongozi wa Scotland waliingia makubaliano ili Scotland ipige kura ya kuamua kuendelea kubakia ndani ya United Kingdom au itoke na kuwa nchi kamili. Miaka 700 kabla George Wallace aliongoza vita vya kudai uhuru (filamu ya Mel Gibson 'Braveheart' iliigiza tukio hilo) na miaka 300 nyuma Uingereza na Scotland ziliingia kwenye Muungano. Makubaliano ya Cameron na Alex Salmond yametengeneza njia kuwa mwaka 2014 Scotland watapiga kura ya "ndio" au "Hapana" kuhusu nafasi ya Scotland kwenye Muungano. Kura hiyo haitopigwa na Waingereza wote. Kura za maoni sasa hizi zinaonesha ni asilimia kama 30 ya Wascot wanataka kutoka kwenye UK.

Mwaka 2005 serikali ya Sudan na uongozi wa Sudan ya Kusini waliingia makubaliano ya kuitisha kura ya maoni ili kuamua hatima ya eneo la Sudan ya Kusini ndani ya Sudan. Kura ile ilikuwa inataka kujua kama watu wa Sudan ya Kusini wanataka kubakia sehemu ya Sudan au watoke nje ya Muungano. Kura ile ilipopigwa January 2011 na asilimia zaidi ya 99 ya wananchi wa Sudan ya Kusini waliamua kujitenga na Sudan na kuunda taifa lao. Kabla na Baada ya kujitenga na kuwa nchi huru serikali hizo mbili zimekuwa zikifanya mazungumzo ya makubaliano mbalimbali ya ushirikiano baina yao. Hakuna Muungano wa Mkataba kati yao yapo makubaliano ya kimataifa baina ya nchi mbili. Hata hivyo, siyo Sudan nzima iliyopiga kura ya kuamua hatima ya Sudan ya Kusini ni watu wa Sudan ya Kusini tu waliokuwa na uhuru wote wa kuamua.

Zanzibar na wale wanaotaka kuwa nje ya Muungano hawahitaji kibali cha Watanzania bara wao kujitoa; wanaweza kabisa kuanzisha mchakato wao na watu wa bara hawapaswi hata kidogo kutoa maoni ya upande wowote ule. Watu wa bara watapaswa kubakia ABSOLUTELY NEUTRAL bila kutoa ahadi wala vitisho ili wananchi wa Zanzibar waamue hatima yao kwa uhuru wote. Ni kwa sababu hiyo baadhi yetu tunataka Wazanzibari kama kweli wanataka watoke kwenye Muungano waanze mchakato wa kuandika sheria ya kura ya maoni mapema ili kura ya maoni iitishwe Julai mwakani na Zanzibar iwe taifa huru ifikapo January 1, 2014.

HOJA YA PILI - UFUATIE MUUNGANO WA MKATABA


Hakuna Muungano wa Mkataba

Sasa kama nilivyosema hoja hizi mbili hazihusiani. Hakuna nchi yenye muungano wa mkataba duniani. Kuna nchi zenye Muungano wa kikatiba (ambao ni Mkataba Mkubwa zaidi kama ulivyo sasa) na kuna makubaliano ya mahusiano ya kimataifa (treaties on international cooperation). Hili ni muhimu kulielewa. Hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kuja kuingizwa kwenye hicho kinachoitwa "MUUNGANO WA MKATABA" ambacho hakiwezi kujadiliwa na kuingizwa katika Muungano wa sasa.

Tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tayari wamekuwa na mikataba mingi baina yao. Hii ni kweli ukiondoa kwanza makubaliano ya Muungano (Articles of the Union) ambao ni Mkataba mkubwa zaidi. Tayari kuna vitu ambavyo vinafanywa kwa mujibu wa mkataba wa Muungano na kuna vitu vingine ambavyo japo vipo nje ya Makubaliano ya Muungano lakini vimekubaliwa baina ya serikali mbili kwa mikataba mbalimbali.

Kumbe basi Muungano wa Mkataba upo tayari. Ni muungano huu wa mkataba umewezesha ushirikiano wa sehemu hizi mbili. Lakini, endapo Zanzibar itaamua kutoka kwenye Muungano huu makubaliano yote ambayo yamekuwepo hadi hivi sasa yatafutwa na itabidi waanze moja. Na hapo ndipo watakapokutana na wanasiasa wa Tanganyika ambao nao watahitaji kulinda maslahi ya Tanganyika katika makubaliano yoyote na Nchi ya Zanzibar. Wasije kufikiria kuwa Zanzibar ikijitoa kwenye Muungano basi itagawiwa kila "nusu kwa nusu"; kwa ujiko gani wapewe kila nusu kwa nusu?

Makubaliano yoyote baada ya Muungano wa sasa kuvunjwa yataangaliwa kwa kupima mchango wa kila sehemu, gharama mbalimbali na kiasi cha fedha ambacho kimetoka bara kwenda Zanzibar nje ya makato yanayotakiwa kisheria. Vitaangaliwa madeni mbalimbali ambayo Zanzibar inadaiwa bara na yale ambayo bara inadaiwa Zanzibar. Baada ya mahesabu yote kupigwa ndipo nini Zanzibar itastahili kitaamuliwa na bila ya shaka kutokana na uchumi wake mdogo serikali ya Tanganyika itajitolea mambo kadhaa ili kuipa nguvu serikali ya Zanzibar kama vile Sudan ilivyofanya kwa Sudan ya Kusini. Mojawapo ya vitu ambavyo naamini Tanganyika itaweza kufanya ni kulipa madeni ya kimataifa ya Zanzibar na kuendelea kulipa pensheni za wale waliowahi kuwa watumishi wa jamhuri ya Muungano.

Nje ya hapo mambo mengine yote yatazungumzika katika majadiliano kama yanavyofanyika baina ya nchi mbili.

HITIMISHO
Hivyo basi, kwa vile hakuna kitu kama Muungano wa Mkataba nje ya Muungano wa sasa ambao ni wa mkataba, hoja pekee ambayo nawahimiza Wazanzibari wote duniani kushikana pamoja na kuidai ni kuwang'ang'ania wawakilishi wao ili walete mswada wa kupiga kura ya maoni ili Zanzibar iamue hatima yake kwenye Muungano wa sasa wa Mkataba. Kama wabaki au watoke. Haitoshi watu kudai kuwa ni "waumini wa muungano wa mkataba"; wangejitangaza ni waumini wa Zanzibar nje ya Muungano huu wa Mkataba". Hapa wangepigiwa makofi.

LET ZANZIBAR GO!
LET ZANZIBAR DECIDE!
 
kuna maneno yako mengne yalinipasa niyarudi mara 3 tatu ili nipate maana zaidi,lakini ngoja nisome tena nipate ufahamu zaidi
 
Haya mawazo yako ya kijinga hayana mashiko yoyote kwa samaki, wewe huwezi kujua zanzibar inaisaidia vipi tanganyika ,mambo haya mtu wa kawaida kama wewe huwezi kujua ,samaki ukimuuliza atakuwambia.

Kuna mambo haya ambayo tanganyika hufaidika kwa muavuli wa muungano.

kwanza kimataifa, utambue jambo lolote ambalo la muungano au silo la muungano, akiindia rais wa united repulic of tanzania ujue linawakilishwa kimuungano, zanzibar huambulia patupu, kama kuna furushi la bilioni dola 200 zitatolewa huko UN basi munafaidika nyie zanzibar huambulia patupu.

zanzibar ikienda njee kuomba msaada wakifika tu huko, huwambiwa ah membe kafika hapa kashaondoka na furushi, kwani hamujapatiwa chenu huko zanzibar ? nyie si muna serikali ya muungano ? Ah hatujapata kitu, jibu mutajuana wenyewe.

Climate change

Imetoa furushi kwa maneo ambayo yamezungukwa na bahari kwa mfano mafia, zanzibar, comoros, na sehemu nyengine, ambazo huwathirika na tabia nchi, maji kupanda juu na mengine , mfuko huu hutolewa na jumuiya ya mataifa, tanzania hupata dongo nono sana ,bahati mbaya zanzibar huambulia patupu,tukienda kuomba msaada huo tunaambiwa tushapewa,tukiulizia huko tanganyika jamani tupeni chetu, ah hichi chetu tumepewa sie dai chenu, haya ndio matunda ya muungano ,wewe mwanakijiji unajidai hufaidikia basi muulize membe waziri wako atakuwambia.

Kuna mengi sana ambayo munafaidika na muungano,lakini hayo ni machachetu mpumavu kama wewe ambae hukusoma au sijui ukaidi tu huelewi ,hutaki ukweli, nafikiri ungelisoma masuala ya uchumi, ungelielewa zaidi na vipi munafaidika katika muungano huu. zanzibar imeanguka kiuchumi kutokana inashindwa kujiamulia mambo yake wenyewe hasa pale inapotaka kufanya ushirikiana na nchi nyengine katika nyanja za kiuchumi, haiwezi bila ya kuomba kibali kwa membe, na hilo ndio kikwazo.

zanzibar ilitaka kujiunga na OIC kwa vile zanzibar ina asilimia 99 waislamu, muungano umewazuiya hilo suala kwa nini ? Munajenga hoja za siasa chafu na kibaguzi eti waislamu sijui magaidi, sijui usultan tunataka kuleta , yaani upumbavu mtupu,,, kwa nini munatuingilia katika maamuzi yetu ?

Hatutaki tena, tunataka zanzibar yetu.

Na kumalizia jiulize kwa nini tunataka muungano wa mkataba ? wakati huo huo tunadai zanzibar huru? Suali zuri sana, na nitakujibu .

Ukweli ni kwamba sheria ambayo inatupa uhuru wa kujadili muungano, ni sheria ambayo inatupa kuuboresha tu na sio kuvunja, na hilo ndilo suala ambalo wazanzibari limetugusa katika katiba mpya, muungano tu na sio chengine katiba yetu tunayo.

kama ulitaka tutoe maoni ya kudai zanzibar huru tu, na tuukatae muungano kabisa tukutae eac basi mwambie rais wako kikwete aabadilishe kifungu chake katika hadidu rejea kuwa kila raia ana haki ya kuhoji muungno kuvunja au kubosha atamke hivyo kisheria basi sisi wazanzibari mutakuwa mushatufungulia mlango,lakini kwa sasa inabidi tuvunje ukuta ndio tupate mlango, ndio huo mkataba, na najua mkata muta ukataa wenyewe, sio ndio heri yetu, mutuachie zanzibar huru hatutaki muungano ,just ujirani mwema ka uk na marekani huko unako kusifu wewe.
 
. huo ndio ukweli uliopo hamna kingine tena. wazenji wenyewe ndio wenye uwezo wa kujitoa ktk muungano kwa kutumia wawakilishi wenu barazani. thats all and no other way. precedent zote kuhusu wengine walivyojitoa mwanakijiji ameeleza vizuri sana hapo juu. kwa hiyo jusa and muungano wa mkataba company limited wahamasishe wazenji to act accordingly.
 
. huo ndio ukweli uliopo hamna kingine tena. wazenji wenyewe ndio wenye uwezo wa kujitoa ktk muungano kwa kutumia wawakilishi wenu barazani. thats all and no other way. precedent zote kuhusu wengine walivyojitoa mwanakijiji ameeleza vizuri sana hapo juu. kwa hiyo jusa and muungano wa mkataba company limited wahamasishe wazenji to act accordingly.
 
Muungano Wa mkataba gani unaotakiwa wakati tayari articles of union kuhusu muungano zipo. Si ndo mkataba wenyewe huo ?

Akina seif yapaswa sasa wawape wananchi pumzi kwa kutokuwachanganyia maneno ya muungano Wa mkataba ambao tayari tunao hivi sasa kuipitia articles of union ! Labda waseme Wanataka mkataba unadumu kwa siku au miaka kadhaa halafu ndio uwe reviewed hapo wataeleweka!

Pili .... Itakuwa ni uhaini kuyapinga Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Kama wanataka kuondoka SMZ kwenye muungano maana ni SMZ chini ya karume walio act kwa niaba ya wazanzibar na hadi sasa kuna Chombo cha kuyalinda Mapinduzi hayo !

Haya ya tunaitaka Zanzibar huru ni uchochezi maana tayari iko huru .

Kama wazenj hawa taki muungano , hakuna awalazinishaye kukaa kwenye ndoa wasiyo iafiki!

Ndoa iliyojaa maneno maneno kati ya baba na mama, baba na watoto au mama BA watoto au na watu wengine haiwezi dumu kamwe! Na ndoa sio ndoana!

Sasa basi nawaomba wazenj wajitoe maana wanatulazimisha kujadili mambo ya nyumbani kwao ambayo hayatuhusu na sana sana yanatupa headache tu!

Binafsi Kama m-bara nimechoka kujadili mambo ya wazenj sijui wanataka nini! Si wajitoe tu halafu ndio waombe mengineyo ikiwemo mkataba !

Kwa niaba yangu binafsi Sitaki ndoa na mke Anaye bwabwaja kila siku bila kuja na suluhisho la matatizo katika ndoa ! Yeye kila siku ni kulalamika tu !

Waende wakatafute mkataba na serikali nyingine Kama Hilo ndilo wanalong'ang'ania !

Mkikasirika kasirikeni tu lakini ukweli ni kwamba hata wazenj wenyewe hawajui wanataka nini ... Ni mkataba , kujitoa kwenye muungano , kubaki au ni yote ? SMZ sasa itoe tamko kwa SMT ili tujue wananchi Wa zenj wanataka nini baada ya hapo tuendelee na mengineyo !
 
The truth is Rais Kikwete pia anaweza kuanzisha mchakato wa refurendum kama alifanya rais wa Indonesia B.J. Habibie kuhusu East Timor ambayo kwa maneno yake mwenyewe imekuwa mzigo mkubwa kwa Indonesia na hauubebeki tena! Wapiga kura walitakiwa ama kukubali East Timor iendele kuwa semi autonomous region ndani ya indonesia au kuwa uhuru.kambi ya East Timor huru ilishinda kwa asilimia 78.
 
Kuwemo au kutokuweno kwenye muungano , mkataba au la , referendum au kura ya maoni , yote ni ya wazenj na hawahitaji elimu ya UPE kujua kwamba mambo yao ya ndani yatamalizwa kindani ndani kabla ya wao kutulazimisha kuwa bebea matatizo yao!

Mbona serikali ya mseto waliitoea jibu na sasa ni GNU! Kwa nini wasifanye Kama walivyofanya kwenye serikali ya umoja Wa kitaifa? Ni nini kinawatatanisha ?
 
The truth is Rais Kikwete pia anaweza kuanzisha mchakato wa refurendum kama alifanya rais wa Indonesia B.J. Habibie kuhusu East Timor ambayo kwa maneno yake mwenyewe imekuwa mzigo mkubwa kwa Indonesia na hauubebeki tena! Wapiga kura walitakiwa ama kukubali East Timor iendele kuwa semi autonomous region ndani ya indonesia au kuwa uhuru.kambi ya East Timor huru ilishinda kwa asilimia 78.

Akifanya hivyo atakuwa anaenda kinyume na katiba uliyomuweka madarakani na ambayo aliapa kuilinda!
 
GHIBUU Dawa ya hayo unayosema ni Zanzibar huru - isiyofungamana na Tanganyika kwa namna yoyote ile. Zanzibar hailazimishwi kufuata kifungu chochote cha sheria kwenye Katiba ya Muungano. Mifano halisi ipo. SUK imeundwa bila ya kubadili kifungu chochote cha sheria kwenye Katiba ya Muungano. Nafasi za makamu (wawili) zimeundwa, sambamba na kufutwa cheo cha waziri kiongozi tofauti na ilivyo kwenye katiba ya Muungano.

Hivyo basi, kama Wanzanzibar watatumia process ile ile iliyotumika kubadili katiba ya Zanzibar, badi Zanzibar huru itapatikana. Sikubaliani na hoja kuwa kizuizi ni sheria! Mbona hizo sheria nyingine zimebadilishwa, hii iweje? Especially kama inahusu hatma ya Zanzibar na watu wake? Ni lini muswada wa kudai Zanzibar huru ulipelekwa BLW Tanganyika ikakataa?

Kuhusu climate change. Msimamizi mkuu wa mambo ya Climate ni Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano. Huyu ni mzanzibari. Sina hakika kama unajua kiasi cha fedha kilichotengwa kwa Zanzibar?

Na kwenye misaada. Zanzibar wanapata misaada kwa kutumia formula ilipitishwa na pande zote mbili. Mwanzoni ilikuwa 4.5% ikaja 7% na kuna hoja kwamba sasa iwe 11%. Hata hivyo, Zanzibar hawalipi madini yoyote ya nje, hakuna gharama za ulinzi, elimu ya juu, balozi, wala passport.

Ninapata shida sana ninaposoma kuwa Zanzibar inachangia hela. Na hii ni kwa sababu naangalia mapato ya Zanzibar (domestic revenue), bajeti nzima ya Zanzibar/matumizi. Hizo za kupeleka Tanganyika zinatoka wapi?
 
Last edited by a moderator:
The truth is Rais Kikwete pia anaweza kuanzisha mchakato wa refurendum kama alifanya rais wa Indonesia B.J. Habibie kuhusu East Timor ambayo kwa maneno yake mwenyewe imekuwa mzigo mkubwa kwa Indonesia na hauubebeki tena! Wapiga kura walitakiwa ama kukubali East Timor iendele kuwa semi autonomous region ndani ya indonesia au kuwa uhuru.kambi ya East Timor huru ilishinda kwa asilimia 78.

Yeah, lakini serikali ya Muungano haijawahi kulalamika kuwa kuibeba Zanzibar ni mzigo. Lakini vile vile akianzisha Rais wa Muungano mchakato Wazanzibari hawa hawa wataanza "unaona hawatutaki kwenye Muungano". Hili linatakiwa kuwa ni suala la Wazanzibari wenyewe. Lakini mfano wa East Timor unaweza usiwe mzuri kwa sababu East Timor haikuwa na serikali yake na vyombo vyake isipokuwa vile vya Umoja wa Mataifa.

Na pia historia ya East Timor siyo sawa na Zanzibar; East Timor ilijitangaza huru lakini ikavamiwa na Indonesia na kufanywa Jimbo la 27 la Indonesia. Serikali ya Muungano wa Tanganyika haikuvamia Zanzibar wala kuigeuza Zanzibar mojawapo ya mikoa yetu. Mfano wako wa East Timor hapa haufai.
 
Kelele nyiingi.....mnasema kuwa hamuutaki muungano, mnapewa jukwaa la kueleza maoni na msimamo wenu, mnabadilika na kuanza kudai muungano wa mkataba. Yaani ninyi muingie mkataba na sisi?? Tutaendelea kuhakikisha mnabaki mpaka tutakajiridhisha kuwa mna akili zilizo komaa badala ya hizi za sasa zinazowaza kulelewa na waarabu. Kama mnabisha jaribuni kutoka muone kama mtaweza.
 
kama ulitaka tutoe maoni ya kudai zanzibar huru tu, na tuukatae muungano kabisa tukutae eac basi mwambie rais wako kikwete aabadilishe kifungu chake katika hadidu rejea kuwa kila raia ana haki ya kuhoji muungno kuvunja au kubosha atamke hivyo kisheria basi sisi wazanzibari mutakuwa mushatufungulia mlango,lakini kwa sasa inabidi tuvunje ukuta ndio tupate mlango, ndio huo mkataba, na najua mkata muta ukataa wenyewe, sio ndio heri yetu, mutuachie zanzibar huru hatutaki muungano ,just ujirani mwema ka uk na marekani huko unako kusifu wewe.

Hamtaki kutoka nyinyi; unadhani kama mngekuwa ni watokaji nyinyi mngekuwa na kizuizi chochote kile. Watu wamepigana na kumwaga damu kudai uhuru wao; we unasema ati 'sheria inatukataza kutaka kutoka'! Kama kweli mnaamini katika kutoka hata kwenda kwenye tume ya maoni msingeenda!
 
Naona watanganyika vipovu vya mdomo vinawatokeni midomoni kisa waz'br kutaka muungano wa mkataba,jamani c kila mtu ana mawazo yake acheni kuwa na akili za samaki,kabla hamjakosoa mawazo ya wenzenu wekeni na nyie mawazo yenu ili yajulikane,kama mnaona bora uwe hivihivi muungano huu sasa kuna haja gani ya tume ya warioba kuharibu pesa za walala hoi kuchukua maoni?hivi hadi leo bado watanganyika mnaogopa kivuli cha nyerere?
 
Yeah, lakini serikali ya Muungano haijawahi kulalamika kuwa kuibeba Zanzibar ni mzigo. Lakini vile vile akianzisha Rais wa Muungano mchakato Wazanzibari hawa hawa wataanza "unaona hawatutaki kwenye Muungano". Hili linatakiwa kuwa ni suala la Wazanzibari wenyewe. Lakini mfano wa East Timor unaweza usiwe mzuri kwa sababu East Timor haikuwa na serikali yake na vyombo vyake isipokuwa vile vya Umoja wa Mataifa.

Na pia historia ya East Timor siyo sawa na Zanzibar; East Timor ilijitangaza huru lakini ikavamiwa na Indonesia na kufanywa Jimbo la 27 la Indonesia. Serikali ya Muungano wa Tanganyika haikuvamia Zanzibar wala kuigeuza Zanzibar mojawapo ya mikoa yetu. Mfano wako wa East Timor hapa haufai.

Zanzibar pia ilijitangazia uhuru wake mnamo tarehe 10-12-1963 na kuwa mwana chama wa UN siku moja na kenya,watanganyika waliivamia z'br tarehe 12-1-1964,hadi leo wameifanya z'br kama mkoa,rejea pinda pale bungeni aliposema z'br sio nchi,unataka mfano upi tena kama c wa timor,rudi darasani.
 
Naona watanganyika vipovu vya mdomo vinawatokeni midomoni kisa waz'br kutaka muungano wa mkataba,jamani c kila mtu ana mawazo yake acheni kuwa na akili za samaki,kabla hamjakosoa mawazo ya wenzenu wekeni na nyie mawazo yenu ili yajulikane,kama mnaona bora uwe hivihivi muungano huu sasa kuna haja gani ya tume ya warioba kuharibu pesa za walala hoi kuchukua maoni?hivi hadi leo bado watanganyika mnaogopa kivuli cha nyerere?
Tunataka serikali 1.
 
Kuwemo au kutokuweno kwenye muungano , mkataba au la , referendum au kura ya maoni , yote ni ya wazenj na hawahitaji elimu ya UPE kujua kwamba mambo yao ya ndani yatamalizwa kindani ndani kabla ya wao kutulazimisha kuwa bebea matatizo yao!

Mbona serikali ya mseto waliitoea jibu na sasa ni GNU! Kwa nini wasifanye Kama walivyofanya kwenye serikali ya umoja Wa kitaifa? Ni nini kinawatatanisha ?

Unaishi sayari ipi ndugu yangu?mkataba ni maoni ya waz'br kwenye ile tume,na nyie pelekeni yenu kwenye ile tume tupate kuwaelewa mkitakacho.
 
Back
Top Bottom