Hoja ya Mnyika(Katiba Mpya) na hoja ya Dowans(kafulila) zakataliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Mnyika(Katiba Mpya) na hoja ya Dowans(kafulila) zakataliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lokissa, Feb 7, 2011.

 1. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  WanaJf kwa mujibu wa taarifa ya habari TBC Taifa saa 2 usiku huu Katibu wa Bunge ameweka bayana amekataa hoja ya Dowans kuwasilishwa kwa vile itaingiliana na uhuru wa mahakama na hoja ya katiba mpya kwa vile katiba iliyopo haina kifungu cha kuruhusu katiba iliyopo ifutwe. Mhh kwa majonzi makubwa sijui nchi inaelekea wapi? kakataa kwa maslahi ya nani? Bungeni kesho kutakalika??? hebu tujuzane tafadhali
   
 2. W

  We can JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani wabunge wote wa CCM, CUF, CHADEMA, TLP nk wenye mapenzi mema na nchi hii, wataongelea DOWANS na KATIBA hata kama nani katataa. Wananchi wanataka hayo mambo mawili yaongelewe kwa kina na ni hayo tu ndo muhimu kwa sasa. Kama Spika atasema kuna kanuni, basi wao waseme, wananchi wako juu ya kanuni, na hakuna kanuni kubwa isiyoweza kutenguliwa kwa maslahi ya umma.

  Kila mbunge akiinuka na kuongela DOWANS, KATIBA, hata kama ajenda iliyoletwa siyo hiyo, Spika wa Bunge ataruhusu tu. Akikataa bila hoja, yaani kwa nguvu, basi ashitakiwe kwa wanachi. Wabunge wote wa vyama vyote wenye mapenzi mema, WAKATAE KWA NGUVU ZAO ZOTE kuingizwa mjini.....

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki WADANGANYIKA.....
   
 3. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2013
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,886
  Likes Received: 267
  Trophy Points: 180
  hivi ilikuwaje tena hoja hizi hasa hasa hoja ya katiba mpya ilizungumzwa?

  nini kilibadilika? je uhuru wa mahakama haukuingiliwa?

  kuna la kujifunza kutoka kwenye mvutano huu mwaka ule na mwelekeo wa majadiliano ya rasimu ya katiba mpya juu ya serikali 3 (maoni ya wengi) dhidi ya serikali 2 (Nape wa CCM)?
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2013
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  mkuu long time since 2011
  Ukitaka kuisoma hiyo hoja cheki hapa JOHN MNYIKA: December 2010   
Loading...