Hoja ya mkoa wa Arusha kutopewa nafasi ya uwaziri hata moja kutawala uchaguzi wa Longido

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Mkoa wa Arusha ni kama "umewekwa pembeni" kisiasa baada ya kutopewa nafasi hata moja ya uwaziri kamili

Natumai hii ajenda itawaumiza CCM katika uchaguzi wa Longido endapo utarudiwa.

Pia hii ni fursa kwa Lowassa kuwathibitishia CCM kwamba yeye ndiyo Leigwanan,akiongea lazima asikilizwe na watu anaowaongoza.
 
Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi anatokea wapi?
Si bora hata wao wana naibu waziri.

Kuna mikoa haina hata naibu waziri.
Bawacha punguzeni malalamiko.
 
Rais ana nafasi ya kikatiba kuteua wabunge kumi ili kubalansi hali ya kisiasa ya nchi na kuweka umoja....hizo si nafasi za kuwapa marafiki na wapambe
kwahiyo kama ni hivyo basi ulitaka ateue watu wa arusha,hii akili ya wapi ??unataka kuniambia mikoa yote 30+ imetoa waziri karibu mikoa yote kasoro arusha peke yake??
 
Naibu waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi anatokea wapi?
Kaongelea Waziri Kamili
Lkn ww unaongelea Naibu Waziri
Vitu viwili tofauti ingawa hoja yake mleta mada ni nyepesi sana

Dar wanae hata huyo Naibu Waziri?
Pwani?
List goes on

Mawaziri wengi wa Magufuli wanatoka Dodoma na kanda ya Ziwa!!
 
Mbona wamepata naibu waziri wa kilimo, wangelalamika dar-es-salaam ambao wamenyimwa kabisa hakuna cha waziri wala naibu waziri .
 
Rais ana nafasi ya kikatiba kuteua wabunge kumi ili kubalansi hali ya kisiasa ya nchi na kuweka umoja....hizo si nafasi za kuwapa marafiki na wapambe
Kwa nini mh rais ahangaike kuteua mbunge halafu ampe uwaziri, wakati wabunge waliochaguliwa na wananchi na wenye uwezo wapo!
 
Mkoa wa Arusha ni kama "umewekwa pembeni" kisiasa baada ya kutopewa nafasi hata moja ya uwaziri kamili

Natumai hii ajenda itawaumiza CCM katika uchaguzi wa Longido endapo utarudiwa.

Pia hii ni fursa kwa Lowassa kuwathibitishia CCM kwamba yeye ndiyo Leigwanan,akiongea lazima asikilizwe na watu anaowaongoza.
Arusha inamajibo mangapi ya ubunge na mangapi mumewapa ccm.
Ukianza kuangalia maswala hayo kila mkoa upate waziri jiulize RUKWA imepata waziri gani na ilhali majimbo yote ya RUKWA wamechukuwa ccm na hakuna waziri hata mmoja alie toka Rukwa.
 
Back
Top Bottom