Hoja ya mh. January makamba kuhusu kodi za pango- maoni na mtazamo wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya mh. January makamba kuhusu kodi za pango- maoni na mtazamo wangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ExpertBroker, Feb 1, 2012.

 1. E

  ExpertBroker JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 454
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hoja ya Mh. January Makamba kuhusu serikali kuthibiti wenye nyumba kukusanya kodi ya pango ya mwaka mzima ni ya kuunga mkono kama ukiliangalia suala lenyewe katika mtazamo finyu (narrow-perception). Tatizo hapa si wenye nyumba! Nafafanua! Kwa miaka mingi hapa nchini suala la nyumba limekuwa halipewi kipaumbele na wachumi wetu wanapopanga au kuandaa sera za maendeleo za taifa! Ndio maana Prof. Tibaijuka (Mchumi) ameamua kuandika kitabu cha HOUSING in ECONOMICS, akiamini kwamba wachumi hawalichukulii suala la housing kama linachangia maendeleo ya taifa!
  [FONT=&amp]
  "[/FONT]
  This book is a much-needed account, with numerous detailed examples, of the role of housing in economic growth and development by an author in a unique position to understand its importance and the practical measures for delivering that growth. While the linkages between housing and the macroeconomic environment in developed countries has been studied, the case of developing and transitional countries has been mostly overlooked. The author establishes these linkages with great clarity, supported by detailed case studies chosen to reflect regional diversity as well as differences in socio-economic development and political systems. On the basis of this analysis, the author goes on to develop specific policies and practices to enable governments to enhance the contribution of housing in economic growth."
  [FONT=&amp][/FONT]

  Ni katika hili ndio maana sheria za mortgage haziko friendly kwa mkopaji, viwango vya riba ni vikubwa sana kwa mkopaji kuweza naye kununua na kumiliki nyumba! Benk nyingi zinafanya biashara na serikali na kupata riba nono (risk free), na ndio maana zinakuwa na kiburi kufanya biashara na Hii inafanya wanaomiliki nyumba wawe wachache, na wapangaji kuwa wengi!

  Karibu zaidi ya 70% kwa DSM ni unplanned, na hivyo maeneo machache yaliyopimwa na kupewa hati, bei za viwanja ama nyumba ziko juu! Hili nalo linafanya wamiliki (Landlords & Landladies) kuwa wachache na wapangaji(Tenants) kuwa wengi!

  Tukirudi kwenye hoja ya Mh. Makamba, ni dhahiri kwamba demand ya housing DSM na mikoa mingine ni kubwa kuliko supply ya nyumba! Utakuta zaidi ya watu watano wanagombania kupanga nyumba moja, na mwingine yuko tayari kulipa hata kodi ya miaka miwili, nini kodi ya mwaka?

  Tuelewe kwamba hakuna sheria inayowapa nguvu wenye nyumba walipwe kodi ya mwaka, hapa ni suala la soko, MARKET FORCES OPERATION! Serikali inabidi kujipanga zaidi katika hili kwani hata ikipitisha sheria bado utekelezaji wake utakuwa hafifu just like EWURA, waulize mkoani bei ya lita moja ya petrol au diesel, ni bei elekezi? Nawasilisha!
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  January ni mbwiga sana siku hizi,kwani hatulipi hizo buku kumi kumi za majengo? Kama wakianza kukata kodi za rents waanze na ya dada yake Mwammy
   
 3. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Binafsi nimepokea hili la Makamba kama ahueni kwa Watanzania.

  Pamoja na kuwa kinachosababisha kodi ya miaka/mwaka mzima ni market forces/ demand/competition btn tenants. ila kuna cases nyingi sana pia landlords wanaweka masharti kuwa wanataka kodi ya mwaka n.k.

  mimi nikiwa muathirika pia, recently last few months, nilijadiliana na Landlord niliekuwa najiandaa kupanga kwake, akitaka kodi y mwaka. Kwa kweli hili la kodi ni la kuangalia.

  unakuta kodi kwa mwezi ni 300,000. kwa mwaka ni 3,600,000/= na 300000 ya dalali.

  wakati mshahara ni monthly.


  Si sahihi. Makamba go on with hoja hiyo, itatukomboa kwa kiasi kikubwa.
   
 4. E

  ExpertBroker JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 454
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi mwenyewe kama mpangaji naathirika sana na hilo la kulipa annually in advance, na ninakuunga mkono SMARTER katika hoja ya January! Kama umesoma hoja yangu, word to word, ni kwamba nimetoa angalizo kwa serikali na wala si kwamba ninapinga hoja!
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ExpertBroker

  je utaratibu wa upangaji kwenye housing sector upoje?

  pili, kwa mtazamo wangu, hapa pa kulipa kodi ya mwaka, haya nadhani ni makubaliano ambapo an offer visa verse acceptance makes an agreement, jee tutamlazimisha mwenye nyumba kupangisha nyumba yake at a set period of time, huyu mwenye nyumba pia anaangalia time value of money against what he/she has invested

  mbona tunalipa prepayment za bill za simu na umeme (LUKU)

  hii haikutakiwa kutungiwa sheria bali taratibu zilitakiwa kuwa improved

  haya ni maoni yangu binafsi
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kodi ya TShs. 300,000 kwa mwezi kama mpangajaji atalipa kwa mkupuo kodi ya mwaka; na kama riba katika mabenki yetu ni 18% inapaswa alipe pungufu kwani thamani ya hiyo pesa kwa leo ni tofauti na miezi ijayo

  Thamani ya leo ya mkupuo wa kodi ya miezi 12 ni sawa na TShs. 3,272,251
   
 7. mooduke

  mooduke JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kama huna kitu kizuri cha kuongea ni kukaa kimya pia
   
 8. E

  ExpertBroker JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 454
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  LAT, hakuna utaratibu wa upangaji mucha as laws and regulations of the country are concerned! Wakati wa ujamaa tulikuwa na sheria ya Rent Restriction act, ambayo miaka ya 2000 ilifutiliwa mbali! Tuna sheria ya Ardhi No.4 ya mwaka 1999 ambayo inakipengele cha LEASE kinachoonesha re/ship ya landlord na Tenant, basi! Haielezi kodo ilipwe kwa mwaka ama lah! Hata marekebisho ya sheria, The Courts (Land Disputes Settlements) Act ya 2002, http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/2-2002.pdf, imeeleza tu taratibu za kuchukua mpangaji anaposhindwa kukulipa kodi yako!

  [FONT=&quot]Jambo la msing serikali iache kukopa ndani ili interest rates ziweze pungua kwa sababu hali tuliyo nayo mabenki mengi yana prefer kufanya biashara na serikali(kukopesha) badala ya wananchi wa kawaida[/FONT]. Ndio maana nikasema tatizo si wenye nyumba tatizo ni serikali na mfumo mzima! Kama serikali ingeamua kukopa nje ama kutoa riba kidogo, haya mabenki yangetukimbilia sana! lakini matokeo yake hayaoni iweje wakupe wewe mkopo ambapo risk yake ni kubwa wakati kuna risk free business na serikali!
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  ExpertBroker
  ^^^^^^^^^^^^ thank you for your point
   
 10. M

  Makfuhi Senior Member

  #10
  Feb 1, 2012
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiyo sheria itakuwa ngumu kutekelezwa kwa sababu ni wenye nyumba WACHACHE WANAOTAFUTA WAPANGAJI. wapangaji ndio wanaopanga foleni kwa wenye nyumba. NHC ijenge nyumba za kutosha ili kupunguza kiburi cha wenye nyumba.
   
 11. E

  ExpertBroker JF-Expert Member

  #11
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 1, 2009
  Messages: 454
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bravo mkuu, umeeleza kwa ufupi na uelewa zaidi! So simplified!
   
 12. G

  Godwine JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  wenye muswada huo waweke ubaoni ili tuusome kabla ya kuuchangia
   
 13. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba amenikiwa kuteka hoja ya CHADEMA kuhusu gharama za makazi. Makamba ameyafanya hayo kupitia hoja binafsi aliyoiwasilisha bungeni.

  Hoja hiyo imetekeleza kwa vitendo ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010 ambayo Dr Slaa alikuwa akizungumzia gharama za ujenzi na kodi kubwa. Hoja hiyo ya CHADEMA ilizungumzwa na kambi rasmi ya upinzani baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kupitia maoni ya wanayemuita Waziri Mkuu Kivuli Freeman Mbowe ambaye alitaka itungwe sheria ya kuanzisha Real Estate Regulatory Authority.

  Maoni hayo yalirudiwa na Waziri wao kivuli wa Ardhi Halima Mdee kwenye hotuba yake bungeni. Hata hivyo, wote walikuwa wakizungumza maneno matupu mpaka leo mbunge makini na machachari Januari Makamba ameleta hoja binafsi na serikali imekubali kutunga sera ya makazi. Hoja hiyo imemkuna hata kiongozi wa Upinzani na kumfagilia Januari Makamba.

  ........ndiyohiyo
   
 14. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kama anafanya kwa ajili ya watanzania hakuna shida
   
 15. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  tunajenga nyumba moja, so hakuna haja ya kugombea fito
   
 16. m

  mwanachademapure Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  binafsi nampongeza Mh. January Makamba kama kijana anayeonyesha taswira ya kweli ya mabadiliko hasa yatakayomnufaisha mlalahoi wa taifa hili. ILA NDUGU YANGU MAKAMBA PAMOJA NA DHAMIRA ZAKO SAFI NINAZOZIONA KUTOKA KWAKO MARA KWA MARA LAKINI HAUKO SEHEMU SAHIHI, NJOO CHADEMA KAKA TUJENGE NCHI.
   
 17. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kwani zile fedha za uchaguzi ,dada yake alizopewa na mzungu wake zitarudi vipi?Au ndio ulikuwa ujira wa dada kupopolewa!Kuna kitu huyu dogo anakitafuta,wala watu kama hawa hatuwahitaji CDM.Bado nazidi kumfuatilia kwa karibu.
   
 18. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Imetulia
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mbona kule FB anasema hoja ni yake binafsi? Hajatoa acknowlegdement kwa Chadema hata kidogo.
   
 20. m

  mwimbule JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 485
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  haya ndio mambo tunayotaka kila mbunge anayeitakia mema nchi hii na ambaye anaweka maslahi ya nchi kwanza anafaa kuungwa mkono. hongera sana JM hili ni jambo jema.
   
Loading...