hoja ya mdau kuhusu libeneke la globu ya jamii katika kipindi hiki cha kampeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hoja ya mdau kuhusu libeneke la globu ya jamii katika kipindi hiki cha kampeni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by TingTing, Aug 31, 2010.

 1. TingTing

  TingTing Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Katika pitia pitia zangu katika blogu ya Issa Michuzi (MICHUZI) nimekutana na hii habari;

  "HOJA BINAFSI KUHUSU MALALAMIKO YA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA GLOBU YA JAMII KUA GLOBU YA JAMII INAPENDELEA ZAIDI CHAMA TAWALA. JE NI KWELI?

  NANI KASEMA ANKALI ANAFAGILIA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI TUU ?NA NANI KASEMA ANKALI KANUNULIWA NA CHAMA HICHO?SASA MBONA ANATURUSHIA NA VYAMA VINGINE?

  JAMANI TUSIMLAUMU SANA ANKALI MIMI KAMA MDAU MKUBWA SANA WA BLOG NIMESIKITISHWA SANA NA KAULI ZA WATU KUSEMA ANKALI HATENDEI HAKI VYAMA VINGINE SI KWELI NI KWAMBA HAO WENGINE HAWATUMI HABARI ZAO SASA ANKALI AOTEEE JAMANIIIII TUJIREKEBISHE MIMI NALETA HOJA APA KWENU........

  MAANA INAKERA WEWE ANGALIA FACEBOOK NA MITANDAO MINGINE ATA APO KIJIWENI KWAKO MNASHADADIA TUU ANKALI KUA ANAPENDELEA CHAMA CHA MAPINDUZI. TUFIKE MAHALI TUBADILIKE WATANZANIA. NAOMBA KUTOA HOJA

  MIMI MDAU WA GLOBU YA JAMII."  Binafsi nimetofautiana na aliyepost ujumbe huu na mwenye blogu kuirusha hewani kama kujikosha kwa jamii. Nilimjibu lakini naona hajaiweka hewani kwani haikuwa inamsifia bali kuelezea yaliyonikumba mie na watu watatu ambao nawafahamu. Majibu yangu yalikuwa kama ifuatavyo;

  "Mimi natofautiana na wewe. Hoja ni vyama vya siasa ila pia hata kwa mambo mengine huwa haweki hewani ingawaji ujumbe aanakuwa ametumiwa. Labda angetupa vigezo vyake anavyotumia ili watu tuwe tunamletea habari kwa kufuata hivyo vigezo. Ni kweli blog ni yake lakini kwa kuwa ni inahusu mambo ya jamii na habari za hapa na pale, ni vizuri basi akawa "fair" pande zote na kwa kila kitu. Nasema hivi kwa kuwa mie nimemtumia habari tofauti tatu ambazo ni za kusaidia wananchi wenzangu lakini mara zote hajaweka hata moja. Isitoshe kuna watu kama wawili tena ambao nao walimtumia habari kadhaa lakini hajawahi kupost hata moja yapo. Ni vyema tukajua vigezo; kama ni vya picha au vya uandishi wa habari za magazetini au mtandaoni. Maana kwa uelewa wangu ni kuwa habari za issamichuzi zote ni za kutumiwa na si ya yeye mwenyewe kuziandika. Kibaya zaidi kuna tofauti kati ya uandishi habari na upiga picha."
   
Loading...