mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,583
- 11,659
Mhe. James Mbatia aliwasilisha hoja binafsi muhimu sana bungeni juu ya ''hali mbaya ya mfumo wa elimu'' wa nchi yetu akitaka bunge lijadili na kupendekeza mfumo bora wa elimu.
Hoja ile ikatupwa mbali na Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndungai ikipigiwa makofi na wabunge wa CCM, Mbatia akaonekana kituko na asiyejua lolote kuhusu mfumo wa elimu ya nchi yetu. Hata miaka mitatu haijaisha, Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ameeleza kuna haja ya kuwa na Mjadala wa Kitaifa juu ya elimu yetu maana inaporomoka na ni dhaifu sana?
Hoja ya Mbatia ilikuwa; "mitaala na mfumo mbovu wa elimu Tanzania" wabunge wa CCM mkagoma kuipokea hii hoja binafsi. mkaitupa kapuni.
Mkapa amekuja na hoja kama ile ya Mbatia, nafikiri wabunge wa CCM sasa wataiona ni Hoja tanzu. Tusubiri kuona rangi mbili wakigeuka kitandani.
Mr mkiki.