Hoja ya Madaraka Nyerere kuhusu barabara ya Serengeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Madaraka Nyerere kuhusu barabara ya Serengeti

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Saint Ivuga, Jun 8, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  Sunday, June 5, 2011

  Mada yangu ya leo: Umaskini mbaya  Mojawapo ya habari ambazo zimeandikwa kwa kina sana kwenye kipindi cha hivi karibuni ni nia ya Serikali ya kujenga Barabara ya lami kuunganisha mikoa ya Arusha na Mara kupitia mbuga ya Serengeti.


  Ni habari ambayo pia imeleta mvutano mkubwa baina ya pande mbili. Upande moja ina wale wanaopinga kuwepo kwa barabara hiyo, wakidai kuwa ujenzi wake utaathiri majaliwa ya wanyamapori waliyopo Serengeti. Upande wa pili ni wale ambao wanadai kuwa ujenzi wa barabara hiyo ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wakazi wa mkoa wa Mara na mkoa wa Arusha na kuwa umefika wakati kwao pia kufaidikia ni ujenzi wa barabara kama maeneo mewngine ya Tanzania.


  Wanamazingira wa ndani ya nchi na nje ya nchi wameungana kupinga kwa nguvu kabisa ujenzi wa barabara hiyo wakidai kuwa Serikali ya Tanzania imeweka sahihi mikataba ya kimataifa ya kutunza na kulinda mazingira na kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakiuka mikataba hiyo. Aidha hifadhi ya Serengeti imeorodheshwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Elimu na Sayansi (UNESCO) kama eneo la urithi wa Dunia na ujenzi wa barabara hiyo unaweza kusababisha kufutwa hadhi hiyo na kuleta athari mbalimbali kwa nchi, ikiwa ni pamoja na kupunguka kwa watalii watakaotembelea Serengeti na hivyo kuathiri biashara ya utalii na mapato yanayotokana na utalii. Na vitisho siyo vidogo, ikiwa ni pamoja na tishio la Tanzania kunyimwa misaada mbalimbali kutoka nje.


  Hoja ya kwamba kwa kujenga barabara hiyo Tanzania itakuwa inakiuka mikataba ya kimataifa ambayo imeweka sahihi ni hoja yenye nguvu. Lakini tunayo mifano mingi ya nchi ambazo zinafanya maamuzi yanayokiuka sheria za kimataifa kwa misingi ya kulinda maslahi ya nchi hizo. Sisi tunaathirika na tatizo la kuwa omba omba. Maslahi ya nchi yetu tunapangiwa na nchi nyingine kwa hiyo hatuna ubavu wa kujenga hoja kuwa jambo fulani linaathiri maslahi yetu, na hivyo basi kudai mapitio ya vipengele ambavyo vitazingatia mahitaji yetu kwenye mikataba ya Kimataifa ya aina hiyo.


  Hoja kuwa barabara ya lami inaweza kufuta misafara ya msimu ya wanyama kuhama kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine nina wasiwasi nayo. Kwamba nyumbu na pundamilia wanaovuka mbuga zenye wanyama hatari kama simba, na chui, na wanaovuka mto Grumeti uliyojaa mamba watashindwa kuvuka barabara ya lami ni mojawapo ya yale masuala ambayo wengine tunayakubali kwa shingo upande kwa sababu tu wanayoyasema ni watu ambao wanasemekana ni wataalamu wa wanyamapori na mazingira. Lakini ni hoja ya kitoto, kwa maoni yangu. Inawezekana ipo athari ya kiasi fulani itakayosababishwa na barabara ya lami, lakini siamini kuwa athari hiyo itafuta kabisa uwepo wa wanyama hao kwenye sura ya dunia kama inavyodaiwa na hawa wataalamu.


  Umaskini ni tatizo, lakini wenye hoja inayounga mkono ujenzi wa barabara ya lami kupita ndani ya mbuga ya Serengeti tungekuwa na uwezo wa kifedha ingewezekana kabisa kupata wataalamu wetu wakatufanyia utafiti utakaoonyesha kuwa athari ya barabara ya lami kwa nyumbu na pundamlia siyo ya kutisha. Huu ndiyo utaratibu uliyopo nchi zilizoendelea pande zinazokinzana zinapotaka kuvunja hoja ya upande mwingine. Umesikia hivi karibuni kuna tafiti zinaonyesha kuwa matumizi ya simu za kiganja yanaweza kuleta ugonjwa wa saratani, wakati miaka yote tafiti zimeonyesha kuwa matumizi ya simu hizo hayana athari zozote?


  Barabara zilizopo kwenye hifadhi za wanyama katika mataifa mengi yaliyoendelea kunakotoka shinikizo kubwa dhidi ya ujenzi wa hii barabara zimewekwa lami. Tungekuwa tuna uwezo wa kuweka msimamo tungeomba wale wote wanaopinga barabara za lami kwenye mbuga za wanyama kwanza wafumue lami zilizopo kwenye barabara zinazopita kwenye mbuga zao halafu ndiyo waje tukae meza moja kupanga namna ya kuepusha kuweka lami ndani ya mbuga ya Serengeti.


  Sishabikii kumaliza wanyama, lakini naamini mahitaji ya binadamu yanawekwa nyuma ya mahitaji ya wanyama. Tatizo ni kuwa wanaharakati wa mazingira hawaambiliki, na hawana muafaka. Tunaamrishwa kusikiliza wanaosema wao, na hawasikilizi hoja nyingine zozote. Ni baadhi ya hao ambao katika jitihada za kuzuwia kuuwawa kwa baadhi ya wanyama kwa ajili ya kutengeneza makoti ya baridi kwa ajili ya binadamu, wako tayari kuua binadamu hao hao wanaovaa hayo makoti.


  Hakuna tusi kubwa kwa Watanzania kama kusema kuwa mnyama ni muhimu kuliko mwanadamu. Ni kweli kwa baadhi ya wenzetu, wanyama ni muhimu sana hata kuliko binadamu. Na tumeshuhudia wanyama kufanyiwa upasuaji na madaktari bingwa kuwatibu maradhi wakati binadamu wenzao wanalala nje bila kufahamu wapi watakula, wacha kupata huduma ya matibabu.


  Hoja yangu ya leo ni kuwa umasikini si sifa nzuri, na ina athari kubwa kwa nchi ambayo inajaribu kuwahudumia raia wake lakini inapata shinikizo kutoka kwa wahisani ambao kauli yao ina nguvu kuliko ile ya raia Watanzania
   
 2. K

  Kicheche Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  "Hoja kuwa barabara ya lami inaweza kufuta misafara ya msimu ya wanyama kuhama kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine nina wasiwasi nayo. Kwamba nyumbu na pundamilia wanaovuka mbuga zenye wanyama hatari kama simba, na chui, na wanaovuka mto Grumeti uliyojaa mamba watashindwa kuvuka barabara ya lami ni mojawapo ya yale masuala ambayo wengine tunayakubali kwa shingo upande kwa sababu tu wanayoyasema ni watu ambao wanasemekana ni wataalamu wa wanyamapori na mazingira. Lakini ni hoja ya kitoto, kwa maoni yangu. Inawezekana ipo athari ya kiasi fulani itakayosababishwa na barabara ya lami, lakini siamini kuwa athari hiyo itafuta kabisa uwepo wa wanyama hao kwenye sura ya dunia kama inavyodaiwa na hawa wataalamu."

  Nakushauri ndugu yangu siku nyingiine ukitaka kujibu hoja ya kitaalamu uwe na takwimu na mifano hai sio kukurupuka na kukosoa hoja za msingi ambazo tayari zimeshafanyiwa tafit na wataalamu waliobobea.
   
 3. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanyama hao wanafaida gani kwetu? Hebu chura wa kihansi wameshaingiza faida gani kwa taifa hili? CCM jibuni maswali haya simple
   
 4. k

  kinyongarangi Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni propoganda tuu ya wanamazingira. kwa taarifa yenu barabara ya sasa kutoka Ngorongoro mpaka gate mpaka ikoma gate inapita ndani ya mbuga ya serengeti tena katikati. hii inaypendekezwa ni kilomita hamsini tu. tatizo ni lami au barabara?. Mbona masai mara kule kesho ambayo ni mbuga iliyoungana na serengeti kuna rami mpaka kwenye mpaka wa tanzanina na bado wanyama wanahama na kwenda huko. Watanzania tunakuwa kama hatufikiri. masai mara na serengati ni mbuga moja inayotengwa na mpaka wa tz na kenya. lEO HII watalii wengi wanapenda kufikia kenya kwa sababu ni rahisi kusafiri kuja serengeti kwa kutumia rami upande wa kenya hadi mpakani. HUKU KWETU VUMBI TUPU. KARAGABAHO
   
 5. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Kuweni wasikivu wa jambo fulani na kwa umakini kisha baada ya hapo ndo uanze kuinamia keyboard.Ni nani aliyesema kuwa atajenga barabara ya lami ndani ya hifadhi ya serengeti??????? Mbona mnaudanganya ulimwengu na hao wanamazingira feki????.Ieleweke waziwazi kuwa inakopita barabara hiyo ya Musoma Arusha inapofika eneo la Tabora B kuna geti pale ndipo itakoishia barabara ya lami na itaanza barabara ya vumbi ndani ya hifadhi yenye km 50 hadi geti ya Klensi na ndipo itakapoanzia barabara ya lami tena kupitia Loliondo mto wa mbu hadi Arusha.Na si kama inavyoelezwa sasa kuwa ujenzi wa barabara ya lami ndani ya hifadhi ya serengeti.TUNASAINI NAKUKUBALI MIKATABA YA KIFISADI TUNAKATAA NA KUPINGA MIPANGO YA MAENDELEO kwa vigezo vya kipumbavu!!!!!!!!!!!!!!!????????
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  si hilo tu mbona wanyama wa serengeti wanaibiwa kila siku kwenda nchi za kiarabu na hakuna mwanamazingira hata mmoja anayelalama? kati ya wizi na uuwaji wa wanyama unaofanywa na waarabu kwa kuratibiwa na kusimamiwa na wizara ya maliasili na utalii Vs ujenzi wa barabara kipi kina madhara na faida kwa watanzania?
   
 7. m

  mzalendo kwanza Member

  #7
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bwana utingo jifunze kuwasilisha mada kwa takwimu sahihi na ushahidi wa kutosha..kuna tofauti kubwa kati ya "national park" na "game reserve" serengeti ni national park na hakuna shughuli zozote za uwindaji but waarabu wapo loliondo game reserve na wanaruhusu kuwinda kwenye reserve.ENVIRONMENTAL AND SOCIAL IMPACT ASSESSMENT UNDER TANZANIA STANDARDS NDO INA JUKUMU LA KURUHUSU MRADI AU KUSIMAMISHA KUTOKANA NA ATHARI ZA KIMAZINGIRA PIA INA JUKUMU LA KUTOA MAONI JINSI GANI MADHARA YANAWEZA KUPUNGUZWA KAMA MRADI WA KIMAENDELEO NI MUHIMU..Barabara itajengwa bt ndani ya park (50kms)itakuwa ya vumbi.
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  unasoma wapi?
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jun 20, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  dah! Wewe ni kicheche kweli ndugu yangu, unauma upande mmoja tu. Sasa mbona wanaopinga kujengwa kwa barabara hiyo hawajatoa takwimu zozote lakini hujawauliza swali hilo? Nimefuatilia mjadala huu kwa kirefu sana tangu ulipoanzishwa na yule mwandishi wa Kenya ambaye alianza hiyo effort ya kutangaza kwenye Facebook na kuwaomba waandishi wengine huko Ulaya na Marekani wapige kampeini za kuzuia serikali ya Tanzania isijenge barabara hiyo. Mpaka leo sababu zinazotolewa ni hizo za kitoto tu, kuwa eti Serengeti ni World Heritage lakini hakuna statistical data zozote zilizowahi kutolewa kuonyesha jinsi barabara hiyo itakavyowaondoa wanyama wale wahame kutoka Serengeti waende sehemu nyingine kama Kongo. Binafsi niliwahi kuvuta mifano mingi sana ambayo ni World Heritage lakini zina bado barabara za lami. Mfano rahisi sana niliotoa ni ule wa Yellowstone National Park iliyoko Marekani ambamo kuna barabara nyingi sana za lami zikiwa na jumla ya zaidi kilometer 300 lakini bado wanyama wa pale hawajatoweka, ukilinganisha na serengeti ambapo wanataka kupitisha barabara ya kilometer 10 tu. Vile vile nilionyesha jinsi Kruger national park huko Afrika ya kusini ilivyo na barabara za lami lakini bado watalii wanakwenda kule, hata mama Obama anaelekea huko wiki hii.

  Afterall Serenegeti leo hii kuna barabara ya vumbi hadi leo, ila kinachotakiwa kinachotakiwa ni kuiwekea lami tu, lakini bado kuna magari yanapita pale miaka yote na wanyama wale hawajawahi kuhama. Kinachotusumbua hapa kwa kweli ni umaskini na ujinga tu. Hili swala la barabara ya lami isijengewe ni kamepini inayotokana na hofu isiyokuwa na msingi wowote iliyoanzishwa Kenya wakidhani itasababisha wanyame wasiende Maasai Mara. Hakuna ushahidi wowote kuwa barabara hiyo itazuia wanyama waseinde Maasai Mara hata kidogo.

  Kama hawataki tuijenge, basi waje watujengee sehemu nyingine lakini kwa kufuata specification zetu, Barabara watakayotaka kutujengea wao ni lazima iwe na lane sita sita ili kutufanya tuwe ni spidi limit kubwa ili kuokoa muda wa usafiri utakaokuwa unatokana na kuzunguka.
   
 10. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Wanaopinga kujenga hiyo barabara ukifuatilia kwa umakini sana utakuta wanatoka mikoa fulani fulani ambayo lami kwenda kwao 'imtulia', pia utakuta ni watu wa nje ya Tanzania, mimi nasema hao ni wasaliti kwa binadamu wenzao na ni wabinafsi saana.
  Haiwezekani hata siku moja kwa mtu mwenye akili timamu aone maendeleo ya binadamu yawekwe kando kwa manufaa ya wanyama, kwa kutoa maneno maneno ya kijinga tu kwa kujifanya mwanaharakati, wakati nchi nyingine wamejenga lami kwenye hifadhi za wanyama
   
 11. M

  Marytina JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Napinga ujenzi wa hiyo barabara 100% pamoja na kwamba home ni ARUSHA
   
 12. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Hongera kwa upinzani wako. Hebu niambie ile barabara itokayo Morogoro kwenda Iringa inapita wapi? (mikumi). Na ile treni ya tazari, si inapita selou game reserve? Acheni kuonea wananchi wa Musoma, Mugumu na Serengeti ingawa nia ya barabara hiyo ilikuwa kwenda kwenye viwanja vya wakubwa waliojipanga kujennga mahoteli eneo la Mugumu. Na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mugumu
   
 13. e

  eltontz JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 825
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  ""km 50 zitakuwa za vumbi; kwingine lami"""" Hivi hawa nyumbu wanajua lami au vumbi na kuamua kutovuka? Science zingine za kipuuzi, lakini ndo ajira yao. Lengo la kuwa na lami ni kufanya sehemu ipitike. yawekwe matuta kibao ya kupunguza mwendo ila lami iwekwe.
   
 14. e

  eltontz JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 825
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Wanamazingira hawaoni uwanja wa kimataifa mugumu na mikelele ya boeing 737; ila kipande cha lami tu cha km50. Very sick people.
   
 15. Prosper82

  Prosper82 New Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa ndo wale wale kasoro tarehe
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Sikio la kufa kweli halisikii dawa. Umeona hao wanyama wanvyouawa katika barabara hiyo inayopita Mikumu kuelekea Iringa? Jengeni tu hiyo barabara na yakija tokeo mnayoambiwa yatatokea msiwalaumu kwa kutowatahadharisha.

  Amandla....
   
 17. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mimi ni mmoja wa watu wanaopinga hiyo barabara kwa 100% na ninafanya hivyo kwa kuwa ni mmoja wa watu wapendao mazingira by natural na kwa profession! Kwa wale wote wasioona umuhimu wa kulinda our wildlife, napenda kuomba wale rejee the Arusha manifesto iliyotolewa na Julius Nyerere wakati wa uzinduzi wa ofisi za hifadhi za taifa. Pia kwa wale wanaolinganisha barabara hii ya serengeti na ile ipitayo mikumi kwenda hadi Zambia, niwaambie tu barabara hii ya mikumi inaigharimu hifadhi ya mikumi a big deal, kila siku wanyama wa size zote hugongwa pale na bila kusahau ajali za magari na watu ambao hufariki baada ya ajali hizo, reli ya tazara licha tu ya kusababisha ajali za wanayama pale Seluu, imesababisha kutoweka kabisa kwa wanyama wakubwa ikiwemo tembo na nyati katika milima ya Uzungwa iliyo kati ya Ifakara na vijiji vya chita na ikule, pia reli hii imeongeza biashara ya nyamapori kwa vijiji vyote vilivyo kando ya reli hii na upande wa pili wa milima ya uzungwa! Madaraka anasema eti barabara itakuwaje hatari kwa wanyama wanoweza kuvuka Grumeti na wanaoweza kuwakwepa simba, well ushauri mdogo tu kwa mdaraka Nyerere kabla ya kujenga hoja hii na kuuita eti ni ya" kitoto" arudi darasani akaome juu ya "ecological interaction" au mahusiano ya wanyama na mazingira yao. ila kumsaidia tu ni kuwa Gari linaloendeshwa na binadamu ikapita pale serengeti ni HATARI sana kwa nyati, pundamilia na nyumbu pale serengeti kuliko SIMBA na MAMBA wa mto Grumeti!
   
 18. T

  Tata JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Huko kwa wanaopinga ujenzi wa barabara ya serengeti wamejenga barabara za lami mpaka juu ya vilele vya milima ya Rocky. Hiyo hapo chini inaitwa Trail Ridge Road inatangazwa kuwa barabara iliyojengwa juu zaidi toka usawa wa bahari huko kwao. Na ni kivutio cha utalii huko kwao.

  Trail Ridge Road is the name for a stretch of U.S. Highway 34 and is the highest continuous highway in the United States. Also known as Trail Ridge Road/Beaver Meadow National Scenic Byway, it traverses Rocky Mountain National Park from Estes Park, Colorado in the east to Grand Lake, Colorado in the west.
  [​IMG]


  Nilishawahi kutembelea mbuga hizi na tulipanda hiyo milima mpaka kwenye kilele cha juu kabisa kwa magari. Na pote huko kulikuwa na barabara za lami zilizojengwa kwa umahiri wa hali ya juu kabisa zikiwa na Observation points nyingi kwa ajili ya kupumzika na kushangaa uumbaji na wanyama wa pori. Hii dhana kwamba lami ni haramu kwa mbuga za africa lakini ni halali kwao mimi siielewi kabisa. Wangetupa mifano hai ya sehemu ambapo wanyama ama walikimbia mbuga au kutoweka kufuatia ujenzi wa barabara za lami tungewaelewa. Vinginevyo ni upuuuzi mtupu na kulishana upepo.
   
 19. T

  Tata JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Kila siku watu wanakufa kwa ajali za barabarani je utakubaliana na hoja kuwa ni wakati muafaka nchi hii ikaacha kabisa kujenga barabara na kutumia magari ya moto ili kulinda maisha na mali za wananchi? Kwa ufupi hoja yako haina mashiko.
   
 20. T

  Tata JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Hii dhana ya kuacha kipande cha kilometa 50 cha vumbi ni upuuzi mwingine. Mimi naunga mkono uwekaji wa lami kwa asilimia mia moja yaani barabara yote. Ni wajibu wa watu wa game reserve kuweka na kusimamia utaratibu wa kudhibiti mwendo ndani ya mbuga.
   
Loading...