Elections 2010 Hoja ya Kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,466
2,000
Katika uchaguzi huu imedhihirika tena haja ya kuwa na tume huru ya uchaguzi. Ukiangalia nchi nyingine kama Uingereza kwa mfano wana tume huru inayowajibika kwa bunge. Sijui hii ni kwa sababu wanafuata system ya utawala ambayo ni tofauti na wa kwetu, lakini kwa kweli kuna hoja ya kuwa na tume huru ili kuepukana na yanayotokea sasa. Nimesikiliza majibu ya tume juu ya tume kutokuwa huru. Kwa kweli naona kama hawako serious na concerns za watu wengi. Wanachulia vitu very simple.

Kama hali itabakia kuwa kama ilivyo, nina wasiwasi damu itamwagika 2015. Watu watachoka. Kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko mapema yasije yakatukuta yaliyowakuta ndugu zetu Wakenya. Wao walisubiri mpaka damu ikamwagika ndio wakaanzisha tume huru (japokuwa bado ni interim). Je, mnaonaje wabunge wa upinzani kupeleka bungeni hoja binafsi ya kuwa na tume huru?
 

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Kama Bunge lilishavunjwa kabla ya uchaguzi na litaundwa baada ya uchaguzi, Tume itawajibikaje kwa hilo Bunge ambalo halipo wakati wa uchaguzi?
 

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,466
2,000
Kama Bunge lilishavunjwa kabla ya uchaguzi na litaundwa baada ya uchaguzi, Tume itawajibikaje kwa hilo Bunge ambalo halipo?

Very good point. Lakini je, kwenye nchi nyingine ambazo tume inawajibika kwa bunge inakuwaje pale bunge linapovunjwa kabla ya uchaguzi? Tume inakuwa responsible kwa nani?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom