Hoja ya kutovaa majoho ni halali kutekeleza ?

alngwea

Member
Oct 26, 2016
21
4
Nimefanikiwa kuona mahafari ya vyuo vichache tokea tamko la wahitimu wa ngazi chini ya shahada kutovaa majoho ikitekelezwa baada ya hiyo kauli kutolewa na waziri husika.

Napata ukakasi kuhusu uhalali wa utekelezaji wa hii kauli kwasababu mkuu wa nchi peke yake ndo mwenye dhamana ya kusema neno na likawa "sheria" sasa hoja ya waziri kwanini imeanza kutekelezwa wakati haijapitia hatua zote za kuwa sheria na kufuatwa na taasisi husika za kielimu.

Kwanza haijapelekwa bungeni na kupititishwa kama mswada.
Pili huo mswada kupitishwa na mkuu kuwa sheria rasmi na kutumika kama itavyoelekeza.
 
Aisee...eti unaenda kuchukua cheti chako cha Diploma na suruali au gauni!
acha tu..inadhalilisha, hakuna hata kapicha na kajoho kutundika sebule ili watoto wawe wanaona mafanikia ya elimu yako!
 
Aisee...eti unaenda kuchukua cheti chako cha Diploma na suruali au gauni!
acha tu..inadhalilisha, hakuna hata kapicha na kajoho kutundika sebule ili watoto wawe wanaona mafanikia ya elimu yako!
Nchi ishakua ya matamko hii
 
Aisee...eti unaenda kuchukua cheti chako cha Diploma na suruali au gauni!
acha tu..inadhalilisha, hakuna hata kapicha na kajoho kutundika sebule ili watoto wawe wanaona mafanikia ya elimu yako!
Cheti unataka joho? Hahahah dree avae nn sasa kanzu au
 
Back
Top Bottom