ndugu yako
Senior Member
- Mar 30, 2013
- 193
- 96
Habari wakuu!!
Jana tumeshuhudia bunge letu ambalo wao wenyewe wanadai eti ni mojawapo ya chombo ambacho wananchi tuna imani nacho wakijaribu kutetea wezi wa pesa zetu!
Toka siku ya kwanza watu tuliona dalili za baadhi ya wabunge kujaribu kutuaminisha kuwa nyeusi sio nyeusi bali ni nyeupe na nyeupe sio nyeupe bali ni nyekundu!
Kwa macho ya kawaida namuona waziri mkuu akisalimika katika hili, ilo sina tatizo nalo sana ila Waziri Muhongo, katibu Maswi na AG Werema hawa wakisalimika bunge litakuwa halijatutendea haki hata kidogo!!
Pamoja na vielelezo vyote vilivyotolewa najiuliza mbunge anapata wapi ujasiri wa kuwatetea hawa watu?!
Dawa ya kuwaondoa hawa watu ni moja tu,, baadhi ya wabunge waanze mchakato leo wa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu!
Saini 75 naamin ztapatikana, hoja ipelekwe kwa spika na ndani ya siku tisini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ipigwe,, naamin serikal haitakubal hilo litokee hasa ikizingatiwa na makundi yao ya urais n vigumu kuwa na uhakika kuwa waziri mkuu atasalimika kwenye kura!
Ni hayo tu wadau!!!