Hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ndio itawafanya wabunge wawe serious katika maamuzi!

ndugu yako

Senior Member
Mar 30, 2013
193
225
Habari wakuu!!

Jana tumeshuhudia bunge letu ambalo wao wenyewe wanadai eti ni mojawapo ya chombo ambacho wananchi tuna imani nacho wakijaribu kutetea wezi wa pesa zetu!

Toka siku ya kwanza watu tuliona dalili za baadhi ya wabunge kujaribu kutuaminisha kuwa nyeusi sio nyeusi bali ni nyeupe na nyeupe sio nyeupe bali ni nyekundu!

Kwa macho ya kawaida namuona waziri mkuu akisalimika katika hili, ilo sina tatizo nalo sana ila Waziri Muhongo, katibu Maswi na AG Werema hawa wakisalimika bunge litakuwa halijatutendea haki hata kidogo!!

Pamoja na vielelezo vyote vilivyotolewa najiuliza mbunge anapata wapi ujasiri wa kuwatetea hawa watu?!

Dawa ya kuwaondoa hawa watu ni moja tu,, baadhi ya wabunge waanze mchakato leo wa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu!

Saini 75 naamin ztapatikana, hoja ipelekwe kwa spika na ndani ya siku tisini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ipigwe,, naamin serikal haitakubal hilo litokee hasa ikizingatiwa na makundi yao ya urais n vigumu kuwa na uhakika kuwa waziri mkuu atasalimika kwenye kura!

Ni hayo tu wadau!!!
 

Daata

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
4,537
2,000
Serikali inapewa nafasi ya kupendekeza namna ya kujihukumu watu wanashangilia......kweli ccm ni janga la kutaifa.
 

Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
3,824
2,000
Serikali inapewa nafasi ya kupendekeza namna ya kujihukumu watu wanashangilia......kweli ccm ni janga la kutaifa.

Tena acha serikali!!! hata watuhumiwa wa ESCROW account, AG na Chenge nao wanaachiwa nafasi ya kuchangia katika maazimio ya kuwahukumu wao wenyewe. Hili hata kama lingekua ktk baraza fulani la kijiji ambalo lina wajumbe ambao hata darasa la pili hawajafika, lisingeweza kuendeshwa kama ilivyofanywa na hawa wawakilishi wetu.

Mimi naamini kiti kitakua kimetambua hilo na kulifanyia kazi na tunaweza kuona umaliziaji mzuri wa maazimio yaliyobaki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom