Hoja ya kurudisha Bungeni sakata la Richmond iende sambamba na kuondoa kinga ya Rais

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,077
2,000
Kuhusu sakata hili yalisemwa mengi na wengi walituhumiwa na ili kutenda haki kama tutaamua kurudisha sakata hili upya Bungeni,basi mimi nashauri hata kile kinachoitwa kinga ya Raisi iondolewe ili kama kuna ulazima wa kuchukua hatua zaidi basi kila atakaetajwa au kutuhumiwa kwa namna au nyinyine basi nae awajibike.

Ikiwezekana hata Tume ya kijaji iundwe kuchunguza upya sakata hili na ripoti yake iwasilishwe serikalini na Bungeni.

Tuliambiwa ile ilikuwa ni ajali ya kisiasa lakini Mwakyembe anaonekana kuwa na mtazamo tofauto hivyo ni bora tu sakata hili lichunguzwe upya ili lifike mwisho.
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,507

Dah, hoja makini sana lakini inahitaji mabailiko makubwa ya katiba na sheria husika. Sijui kama hilo linawezekana kwa bunge hili la waliowengi kujua kusifia tu!

Anyway, hawawezi kurejesha suala hilo bungeni maana hawana ujasiri wa kuondoa kinga ya raisi. Nakuhakikishia kuwa 'Mwa Kiembe' anabipu ukawa lakini ni rahisi sana kwa ukawa kupiga na hiyo ikitokea itaigharimu CCM sana. "Serikali itatikisika" maana aliyesema hatafukua makaburi atashangaa yakiwa wazi. Yakiwa wazi ya richmond ya escrow, epa, meremeta na kadhalika pia yatskuwa wazi. Ahadi ya kuwalinda watsngulizi wake itakuwa null and void au kwa lugha nyingine 'vanquished'!

Wathubutu waone kitakachotokea!
 
Mifupa

JF-Expert Member
May 19, 2014
286
250
Mwakyembe si kawaomba Wabunge wa chadema wakiongozwa na Kubenea na magazeti yake wairudishe bungeni halafu nyie mashabiki wao mnakuja na maswali na majibu wenyewe si waambieni kwenye vikao vyenu wairudishe ili bwana yule na mgombea wenu muone kama hata jinyea tena kama wakati wa kampeni
 
BABU KIDUDE

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
1,588

Mitambo yenyewe ndo hile aliyokuja kuzindua Bwan Baraka Hussein Obama Ujue. Ukiondoa ushabiki kidogo utajua ukweli just kidogo tuuu
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,272
2,000
Kuhusu sakata hili yalisemwa mengi na wengi walituhumiwa na ili kutenda haki kama tutaamua kurudisha sakata hili upya Bungeni,basi mimi nashauri hata kile kinachoitwa kinga ya Raisi iondolewe ili kama kuna ulazima wa kuchukua hatua zaidi basi kila atakaetajwa au kutuhumiwa kwa namna au nyinyine basi nae awajibike.

Ikiwezekana hata Tume ya kijaji iundwe kuchunguza upya sakata hili na ripoti yake iwasilishwe serikalini na Bungeni.

Tuliambiwa ile ilikuwa ni ajali ya kisiasa lakini Mwakyembe anaonekana kuwa na mtazamo tofauto hivyo ni bora tu sakata hili lichunguzwe upya ili lifike mwisho.

Suala la Kinga ya Rais siyo suala la tuhuma au mashtaka ni suala la Katiba. Katiba inaweza kubadilishwa na ikaondolewa lakini kuna sababu kwanini kuna kinga ya Rais; huwezi kuiondoa yote kwani hutakuwa na kiongozi wa kitaifa yeyote. Na Rais hana kinga ya kivile hasa kama kuna wabunge wengi wa upinzani. La maana ni kutaka upinzani ujiimarishe usijivuruge kama ulivyojivuruga 2015. Watu wamekula ng'ombe mzima inafikia mkiani wanaenda kutafuta mataputapu!

Ajali zipo za aina nyingi; nyingine ni ajali za kizembe na nyingine ni za kujitakia. Ukikubali kuwa ni ajali ya kisiasa basi ujue ile ilikuwa ni ya kujitakia.
 
Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344

Chamachamagige watapinga tu. Wakiipitisha hiyo ya kuvua kinga nitaacha utumishi niliyo nao. Hayo ni maneno ya kujifurahisha tu. Mbona mwenyewe kashindwa kufirward report ya Toshiba kwa kusingizia ni one sided? PhD za siku hizi ni shida kama mzee Warioba
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,736
2,000
Mwakyembe si kawaomba Wabunge wa chadema wakiongozwa na Kubenea na magazeti yake wairudishe bungeni halafu nyie mashabiki wao mnakuja na maswali na majibu wenyewe si waambieni kwenye vikao vyenu wairudishe ili bwana yule na mgombea wenu muone kama hata jinyea tena kama wakati wa kampeni
Hawa vijana wa Ufipa ni kama vinyonga ,wabunge wao wameambiwa wairudishe hoja ya Richmond bungeni,sasa badala ya kuwataka wabunge wao wafanye hivyo wao wameanza kuja na ngonjera zingine,hawana lolote Mwakyembe kawageuzia kibao na sasa wanajambajamba tu,wanajitekenya na kujikuna wenyewe.
 
Acha porojo waambie wabunge wa Chadema warejeshe bungeni hoja ya Richmond mambo ya kinga ya raisi wapi na wapi?mnaogopa nini?
 
twahil

JF-Expert Member
May 31, 2011
4,099
2,000
Pia iende sambamba na hapa Jamiiforums watu kutumia majina yao halisi tukianza na wewe...
 
Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Hawa vijana wa Ufipa ni kama vinyonga ,wabunge wao wameambiwa wairudishe hoja ya Richmond bungeni,sasa badala ya kuwataka wabunge wao wafanye hivyo wao wameanza kuja na ngonjera zingine,hawana lolote Mwakyembe kawageuzia kibao na sasa wanajambajamba tu,wanajitekenya na kujikuna wenyewe.
Cdm wakiirudisha mtapinga ili kutetea chama chenu. Pelekeni nyie ili mjazilize na ile nyama mliyobakiza kwa faida ya chama. PhD za leo bwana iko maneno
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
43,077
2,000
Mwakyembe si kawaomba Wabunge wa chadema wakiongozwa na Kubenea na magazeti yake wairudishe bungeni halafu nyie mashabiki wao mnakuja na maswali na majibu wenyewe si waambieni kwenye vikao vyenu wairudishe ili bwana yule na mgombea wenu muone kama hata jinyea tena kama wakati wa kampeni
Acheni unafiki nyie watu!Hili jambo mara ngapi mlikuwa mnalizima Bungeni?
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,591
2,000
Suala la Kinga ya Rais siyo suala la tuhuma au mashtaka ni suala la Katiba. Katiba inaweza kubadilishwa na ikaondolewa lakini kuna sababu kwanini kuna kinga ya Rais; huwezi kuiondoa yote kwani hutakuwa na kiongozi wa kitaifa yeyote. Na Rais hana kinga ya kivile hasa kama kuna wabunge wengi wa upinzani. La maana ni kutaka upinzani ujiimarishe usijivuruge kama ulivyojivuruga 2015. Watu wamekula ng'ombe mzima inafikia mkiani wanaenda kutafuta mataputapu!

Ajali zipo za aina nyingi; nyingine ni ajali za kizembe na nyingine ni za kujitakia. Ukikubali kuwa ni ajali ya kisiasa basi ujue ile ilikuwa ni ya kujitakia.
Mambo mengine tusikumbushane tukachimbua makovu yaliyoshapona yakageuka vidonda tena haswa kwa kuzingatia hoja kama za
Kwenye msafara wa Mamba, na Kenge wapo!- It is Either with US or Against US!

Tena usitukumbushe kabisa kuhusu watu hawa
Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM!
ambapo watu mliokuwa nao mstari mmoja mkipigana bega kwa bega against a common enemy mkijijua you are one and together united you stand, kumbe sii wenzenu!, you are not together hadi wanapowageuka na kumkumbatia adui ndipo mlipajua kumbe mko na wasaliti ndani ya nyumba yenu! .
Tusikumbushane yaliyopita sii ndele, tugange yaliyopo na yajayo!.

Paskali
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,103
2,000
Chadema ndio wamelalamika kuwa Lowassa hakutendewa haki Bungeni 2007

Chadema ndio Walizunguka Nchi nzima kutangaza Ufisadi wa Lowassa

Chadema ndio Jana wamekumbushwa kanuni zinaruhusu Mjadala wa Richmond kurudishwa Bungeni Kama hawakuridhika na Sakata la Richmond

Chadema hao hao baada ya kuambiwa warejeshe Mswaada Bungeni Kama hawaridhiki wanaanza kuleta Masharti
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom