Hoja ya kupita bila kupingwa imepoteza mvuto CCM

Bwana Kheri

Member
Oct 31, 2018
26
49
Wakati huo siasa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimeshika kasi, hususan kuanzia miaka ya vyama vingi kupamba moto wakati wa NCCR Mageuzi, ikaja CUF na sasa Chadema, ukisikia jimboni mbunge wake ameshinda bila kupingwa, kata diwani amepita bila kupingwa asilimia kubwa kwenye eneo hilo mgombea husika ana nguvu kubwa.

Nguvu hiyo imechagizwa pia na chama chake kilichomteua kukubalika, haswa CCM ambacho ndio chama kilichokuwa kinabahatika wanachama wake kupitia bila kupingwa. Ingawa fununu haziishi kwamba mara nyingi watu hupita bila kupingwa kwasababu wagombea wa CCM huwanunua wale wa upinzani, ila hoja hii inakosa mashiko maana hutolewa mchakato wa uchaguzi unapofikia ukingoni.

Pamoja na upitaji bila kupingwa kwa wabunge na madiwani kutokuwa mgeni nchini Tanzania, lakini kwa siasa za leo umepoteza mashiko. Hata asiyefuatilia siasa anaposikia kuna aliyepita bila kupingwa hugundua kwamba ama wapinzani wamenunuliwa au TUME YA UCHAGUZI imemsaidia mgombea wa CCM kupita bila kupingwa. Ingawa mtindo huu unawanufaisha CCM kwenye majimbo na kata husika, lakini chama kinakosolewa na kudhihakiwa na watu wengi, wakiona chama kinakosa mvuto na mashiko.

Ukiacha Tanga Mjini, lakini wilaya nyingi za Mkoa huo CCM ina nguvu, ikiwamo wilayani Korogwe, ambapo kwenye jimbo la Korogwe Vijijini tumeshuhudia kilichotokea juu ya mgombea wake Timotheo Mzava.

Huko Ukerewe nako mambo ni yale yale ambapo Mgombea ubunge jimbo la Ukerewe Joseph Michael Mkundi (CCM) na wagombea Udiwani kata ya Namilembe Innoseth joseph na Kata ya Bukiko Novatus Fikiri Mgonya CCM wote wamepita bila Kupigwa katika chaguzi mdogo katika Jimbo la Ukerewe Mwanza. Hili na mengineyo yangetokea zamani, wana CCM nchini kote wangetembea kifua mbele kujivunia ushindi huo, lakini sio leo kuonekana ni kituko.

Viongozi wa CCM wote na wana CCM kwa pamoja wanapaswa kutafakari mwenendo huu, sio mzuri, unakichafua na kukiangamiza chama hiki kikongwe barani Afrika. Hatukatai ushindi ni ushindi. Ila ushindi unaozua mashaka nje ya sanduku la kura hauna mvuto. Unaibua maswali. Ikiwa Mkurugenzi wa Halmashauri amepewa amri ya kutotangaza washindi nje ya CCM hadharani, ikapelekea wapinzani kujiweka kando, hapo hapo NEC ikatangaza mgombea wa CCM kupita bila kupingwa, inashangaza na kufikirisha kiongozi huyu kweli anajua anachokifanya?

Wana CCM na viongozi wao wanaofurahia ushindi wao wa kupita bila kupingwa kwenye kata zao na majimbo yao vichwa vyao vina ubongo au Mungu alisahau kidogo?

Bado nawaza.
 
2020 uchaguzi wapo waangalizi jumuia za kimataifa, wasiwasi wangu anaroho ngumu anaweza nunua wagombea karibu wote, kwa cash na vitisho kuwauwa.
 
Hivi Tanzania polisi wapo wangapi hadi raia kuwashindwa?Wananchi wanashindwaje kuwakabili watu wawili dhidi ya elfu mbili?Uzembe huo!
 
Hivi Tanzania polisi wapo wangapi hadi raia kuwashindwa?Wananchi wanashindwaje kuwakabili watu wawili dhidi ya elfu mbili?Uzembe huo!
Kwa taarifa yako tarehe 26/4/2018 Yale yalioitwa maandamano ya kuling'oa jabali la pale viunga vya magogoni kulishuhudiwa vikosi vilivyozunguka nchi zima kwaajili ya kutuliza au kuzima hayo maandamo,

Kibaya zaidi vikosi hivyo vilikua na silaha zenye magazine zikiwa na risasi za moto yani "chuma".

Sasa mkuu hoja yako ni nzuri sana ila umewahi fanyia utafiti matokeo ya risasi aina ya 50 CAL ikipata kuzama kwenye mwili wa binadamu.? (Google impact ya 50 Cal shot in human body)

Jibu ni kwamba tuliowapa dhamana ya kutulinda ndio wauwaji/watesi wetu, wanaopokea order kutoka kwa chama kisicho na maarifa na weledi wa uongozi baada ya muasisi na aliyefiti uongozi huo kutuacha.

Ova!.
 
Umejazwa upuuzi kichwani.Misri na nchi zingine za waarabu zilizoshuhudia Arab spring zilikuwa na majeshi(siyo polisi) yenye nguvu ajabu!Hizo nguvu na marisaa/risasi ulizoandika(MAANA hizijui) viliishia wapi?Amka weye!Acha ndoto na uoga kama mla miguu ya kuku.
 
Back
Top Bottom