Hoja ya kuhamishia utalii Kanda ya Ziwa ni muhimu kiuchumi. Asante Dkt. Magufuli

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,441
Nimemsikia Mgombea wa CCM akinadi sera zake na kuahidi kuwa serikali inao mpango kabambe ya kubadili ukanda wa ziwa kuwa wa kiutalii ili kuiongezea Serikali mapato nikafurahi sana kama mwananchi. Ni wakati mwafaka sasa kusambaza utalii kanda ya magharibi na kusini ili kutekeleza Master Plan ya utalii Tanzania. Kanda za magharibi na kusini zina vivutio vipya na vya kipekee kuvutia watalii hivyo nashauri yafuatayo:

1. Kuboresha na kupanua miundo mbinu ya viwanja vya ndege maeneo haya kwa vile vilisahaulika muda mrefu
2. Kuhamasisha wawekezaji wa sekta ya utalii ili wajenge mahoteli na kuanzisha makampuni ya usafirishaji utalii
3. Kuboresha miundo mbinu ya mabarabara katika miji na hifadhi zilizoko maeneo hayo
4. Kutangaza utalii wa maeneo hayo

Haya ni machache yanayoweza kuchochea kukua kwa utalii maeneo hayo badala ya kutegemea utalii wa kaskazini pekee.Tumchague Magufuli atuletee maendeleo.
 
Wachaga wakisikia hivi wanatamani kupasuka!

Hawa jamaa wanajionaga nchi hii ni yao pekee
Ingawa Mimi sio mchaga Ila wewe ni mjinga namba 1 hapa jukwaani kwasabb mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ni ecological ya dunia hata magufuli afanye kiasai gani hataweza kubadilisha historia ya mikoa ya kaskazini.
 
Back
Top Bottom