Hoja ya kilimo cha bangi kuruhusiwa Tanzania

alibaaliyo

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
385
500
Wakuu,
Baada ya kumsikiliza Mh Mbunge akitoa hoja kuwa kilimo cha bangi kiruhusiwe nchini nimekuwa na najiuliza maswali mengi.

Mh Mbunge amesema kilimo kiruhusiwe ila watu wasiruhusiwe kuvuta. Yaani kilimo kiruhusiwe ili bangi uizwe nchi za nje TUPATE fedha. Nina swali lifuatalo:
Je, serikali ina uwezo wa kukabiliana na matokeo ya uhalifu na magonjwa wa akili kwa watumiaji hasa vijana.
Viroba vya pombe virivyokuwa vinauzwa holela vilisababaisha vijana wengi kupata ajali barabarani, kupata vilema, upotevu wa mali n. k.
Je, nchi hiko tayari kukabiliana na wimbi la uhalifu na ajali za barabarani na adhari zake.

Je, uholela huo wa bangi vijana wetu watakuwa taifa la kesho la namna gani?.

China ya zamani walipiga marufuku kilimo cha bangi. Nchi ya China walionja uchungu wa kilimo cha bangi. Vijana wa China wa wakati ule wengi waliharibikiwa serikali ya China ikapiga marufuku kilimo hicho zaidi ya miaka 80 iliyopita.

Kama Mtanzania mwenye ndugu waliohadhirika na uvitaji wa bangi nimesikitika na Mh mbunge kuipigia debe kilimo cha bangi.

Wote ni mashahidi kule Mkoa wa Mara uhalifu ilivyokuwa kule kabla serikali kuweka nguvu za ulinzi na usalama wa raia na kuanzisha kanda maalumu ya Kipolisi. Wananchi wengi mkoa wa Mara wamehamia maeneo mengi kanda ya I want na pengine mikoa mengine wakikimbia uhalifu maeneo yao.

Watanzania wenzangu Kilimo RASMI cha bangi ni hatari nchini mwetu.
 

k123gan

Member
Jul 11, 2015
75
125
Samahani mkuu ushawahi itumia ? Na kama bado hoja zako ni finyu sana. Matatizo ya akili usemayo yaweza tokana na vingi sana ila pombe, bangi nk huamsha tu hayo matatizo ila hayausiani direct. Kuna dhana huwa tunapotoshwa sana lakini mpaka yakupate ndo rahisi kuujua ukweli. Ila haya ya kusimuliwa na kuona kwa watu tunadanganywa sana.
 

nsanzu

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
3,919
2,000
Faza una uhakika kuwa uhalifu uliokuwa ukifanyika mkoa wa Mara ni sababu ya bangi? Nimeishi Tarime Buhemba hapo miaka kadhaa, kitu kama hukijui omba kwa wanaofahamu uelekezwe ufahamu sio kupiga domo tu hapo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom