HOJA YA KATIBA: Waislamu kushinikiza Mahakama ya Kadhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOJA YA KATIBA: Waislamu kushinikiza Mahakama ya Kadhi

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Jan 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,254
  Trophy Points: 280
  na Asha Bani

  IKIWA mapambano ya kudai katiba mpya yanaendelea, jumuiya na taasisi za Kiislamu Tanzania zimesema katika madai yao kutakuwepo na mapendekezo ya kuishinikiza serikali kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema watapita katika kila taasisi ya Kiislamu nchini kwa lengo la kukusanya maoni kama ilivyoahidi lakini ni muhimu kuwepo na hoja ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo ya Waislamu.

  "Suala la Mahakama ya Kadhi kwa ujumla ndilo muhimu lakini pia ni muhimu kukusanya mambo mengi ambayo naamini yatakuwa na misingi mizuri, kikatiba suala hilo haliwezi kukwepeka lazima liwepo pia," alisema Ponda.

  Aidha, alisema wao kama Waislamu wa jumuia tofauti tofauti wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kusema ataunda tume ambayo itakuwa na uwakilishi wa watu wote.

  Sheikh huyo alisema hata hivyo kutakuwa na mkutano wa jumuia mbalimbali za Kiislamu utakaofanyika Januari 8 katika ukumbi wa Tanzania Muslim Solidarity Trust Fund ukiwa na lengo la kufanya mchakato wa kupata watu ambao wao wanaamini watafaa katika kuwawakilisha pindi mchakato utakapoanza.

  Alisema baada ya kuyapata majina yatakayowawakilisha watawasilisha majina hayo serikalini kama yatakuwa yanahitajika na kwamba Waislamu hao ndio watawafaa katika kuwawakilisha.

  Alisema katika mkutano huo pia BAKWATA wamealikwa kuudhuria na wameamua kufanya hivyo ili kuwatoa unyonge Watanzania ambao wanafikiri BAKWATA peke yao ndio wanaostahili kufanya kazi za jamii nzima ya Waislamu.

  "Utaratibu huu tunaamini kwamba utamsaidia rais kwa kuwa sisi ndio watu ambao tuna mtandao wa namna ya kuifikia jamii ya Kiislamu ambapo pia itarahisisha kazi za tume na miongoni mwa kazi zetu ni kwenye misikiti kwenye jumuia na kwingineko, tutafika kote," alisema Ponda.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,254
  Trophy Points: 280
  Ni vyema Sheikh Ponda akawa na upana wa mawazo kuwa Mahakama za kidini ni lazima zijitegemee kifedha.....zisitegemee serikali kupitia hazina itafanya kazi ya kuzibeba shughuli za kidini kwa sababu siyo kazi yake.....

  Vilevile atetee Mahakama za Dini zote siyo kujikita kwa dini yake tu kwa kufanya hivyo atajikuta anatetea ubaguzi na upendeleo wa dini yake tu.....

  Sheikh Ponda be smart now, the era of a demgogue is truly over.....
   
 3. y

  yogamo New Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa na wakristu wataanzisha mahakama ya kikristo, naserikali iunde tume tuoe! Hawa jamaa wana muono hatua chache sana. Hii nchi si ya kidinieti..
   
 4. F

  Francis Jr Senior Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acheni kuwa na Mioyo ya kutu! Mbona Uganda na Kenya kuna mahakama ya Kadhi lakini hakuna tatizo wala madhara yaliyotokea! Uganda na Msumbiji waislamu ni 10% kwa 12% wamejiunga hakuna madhara yeyote sisi wakristu wa Tanzania tuwaache nao waislamu waishi vizuri katika nchi yao na si kuwasakama na wenyewe nchi yao hii!
   
 5. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa waache ujinga Mahakama ya Kadhi kwani hii ni nchi ya kidini?
   
 6. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli wakati waandika katiba wakifikiria kuanzisha mahakama ya kadhi ambayo waislamu wanataka ilipiwe kwa Pesa za serikali, wasisahau kuweka vipengele vya kullipia mahitaji ya kiimani ya wakristo kwa Mfano kulipia gharama za kuhubiri injiili kwa wakristo, hiki kitakuwa ni kipengele muhimu kwa ajili yetu wakristo kutimiza agizo la bwana wetu yesu kristo kuihubiri injili yake duniani kote.
   
 7. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  mbona hiyo ni haki yenu na nyie mdai tu. Ila pia waislam watahitaji mabilioni yote ambayo kanisa lilitengeneza mkata feki kuibia watanzania yale mabilioni yote ambayo kanisa lilisha chota na waislam wapewe. Halafu kaka suala la nyie kutaka kufanya mahubili hata siku moja hutosikia waislam wanakuzuwieni.
   
 8. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  unajua mnapokosea ni kuwa chuki binafsi mnaiweka mbele, ivi mahakama ya kadhi kenya haipo? mmesikia tatizo gani kuhuiana na hiyo mahakama ya kadhi? chuki haijengi.
   
 9. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Halafu na wakristo watadai mabilioni ya pango ya kutumia mashule yaliyojengwa na wakristo kwa unyang'anyi, mabilioni hayo yarudishwe na mashule yarejeshwe kwa wakristo.
   
 10. J

  Joshua Bukuru Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Japo rais amekiri kuandikwa kwa katiba mpya inayokidhi na kuendana na mahitaji ya watanzania, mimi nadhani hili la mahakama ya kadhi halitakiwi kuwepo kwa mwamvuli wa serikali. Tulikiri tangu uhuru kuwa Tanzania ni nchi isiyofungamana na dini yoyote japokuwa watanzania wana dini zao, ikaandikwa kwenye katiba na itaendelea kuwepo. Kama kweli mahakama hiyo wanaihitaji, kwanini wasianzishe wao kama waislamu kutatua matatizo yaliyopo ndani ya dini ya kiislamu na waislamu wao. Mbona dini nyingine zina mfumo wa kutatua matitizo yao pasipokuwa na mahakama za kadhi? Tusihatarishe umoja na amani yetu kwa mambo yasiyolinufaisha taifa na watanzania. Nisingependa kuona tunagombana na kukashifiana kwa misimamo ya dini zetu. Tanzania is a secular state and it (will and shall and must) remain as a secular state. This is not subject to discussion or debate!
   
 11. M

  MUSTAPHA Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 18, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala la mahakama ya kadhi wasio waislamu haliwahusu.Inasikitisha kuona kuwa hao ndio wenye vimbelembele katika kuipinga mahakama ya kadhi.Hivi nyinyi inawahusu nini?Haya ni masuala ya waislamu mutuachie wenyewe tunaojua umuhimu wa kuwepo kwa mahakama hiyo.
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kuwa Muislam WaTZ NI KUJIVUMILIa. NATAKA KUBADILI DINI
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Sio lazima kuiga hata uovu unaofanywa na mwenzako........iga mambo ambayo yana maslahi kwa wote.........maslahi ya watz sio ukristo wala uislamu kwa hiyo ni mjinga anayetuletea maslahi ya kidini katika mapendekezo ya katiba ya taifa............mbona kwa mfano wakatoliki wana sheria zao za ndoa ambazo hawajawahi kuiomba serikali iweke kwenye katiba.............uislamu ni uchafu ambao hauwezi kuweka kwenye katiba hata siku moja.............ponda ajue matatizo ya maisha ya watz ambao 85% ni masikini hayajaletwa na dini kwa hiyo ni upumbavu kuzungumzia madini haya wkt serikali haina dini.............ni vizuri kila dini kuzingatia sheria za nchi na kuto kutuletea mchezo mchafu wa dini................mbona ponda hajawahi kutumia dini yake kusaidia wat km yafanyavyo madhehebu ya kikristo?......haya maslahi ya dini sio maslahi ya watz....maslahi ya watz ni maisha yao yawe bora ili wawe na uwezo wa kumudu gharama za maisha ikiwemo kumchangia ponda kwa njia ya sadaka ya waumini wake............

  "tuache upuuzi ktk katiba ya nchi.........uislam ni adui wa amani popote duniani"

   
 14. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wanataka kuishirikisha serikali ambayo ina wakristo wengi?...........km ni mambo ya waislamu kwa nini ku-blow out na wengine wasikie...........tatizo uislamu unafundisha uvivu kwa hiyo hawana pesa za kuendesha mahakama zao haramu na kutaka kulazimisha hata wakristo wanaolipa kodi kubwa serikalini wachangie uendeshaji wa mahakama haramu kwa wakristo....................mbona wakatoliki wana sheria zao za ndo ambapo hawana haja ya kuishirikishja serikali au mwislamu yeyote ktk kuendesha kesi zake?....................huu ni ulimbukeni wa dini kutoka kwa waislamu..........

   
 15. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Kwani mahakama za kikristo zikianzishwa zitakuwa na madhara gani?


   
 16. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jibu hoja tajwa na wala si kutoa takwimu isiyojibu hoja asilia. Je mahakama husika katika nchi ulizoainisha zinapata upendeleo maalumu wa kuhudumiwa na pesa za walipa kodi ama zajitegemea kwa gharama za kiuendeshaji?
   
Loading...