Hoja ya hoja: Bei ya internet kwa makampuni ya simu

morenja

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
4,343
2,000
Imekuwa ni kawaida kwa makampuni ya simu za Mikononi za Tanzania katika kufanya maamuzi binafsi katika kupanga bei za internet bila ya kumuangalia mtumiaji wa mwisho ambae ni Mtanzania masikini.

Napata ugumu kuamini Tanzania inayotafuta maendeleo kwenye nyanja hii kwanini iweze kukubali na kuwaachia makampuni ya simu kufanya Price Fixing watakavyo huku wakishusha viwango vya internet (MB) na kuongeza thamani ya gharama kwa watumiaji wa Tanzania ambao ni masikini huku wizara husika ipo, Competition Commission, Competition And Consumer Protection Policies zipo na wahusika wapo wanafumbia macho tu.

Tukitaka Tanzania iendane na dunia inavyokwenda na kuongezeka kimaendeleo katika nyanja hii na tukitaka kwenda sambamba na Mtazamo madhubuti na ulio mzuri wa Mheshimiwa Rais wetu Magufuli wa kuiletea Tanzania maendeleo kwenye kila nyanja na kutaka kufanya Tanzania liwe Taifa lenye nguvu duniani na lenye watu walio elimika ni vyema wahusika wakahakikisha haya makampuni ya simu hayafanyi Price Fixing maana ukiangalia kwa undani viwango vyao vya kuuza internet vyote vimepangwa sawa sawa na vyote wamevishusha kwa wakati mmoja bila ya kutoa sababu ya msingi inayo wafanya kuongeza gharama na kushusha viwango vya internet wakati Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umepita Tanzania.

Wahusika kama mkishindwa kuwatetea Watanzania walio wanyonge, Mheshimiwa Rais Magufuli hili ni jipu tunaomba uanze kutumbua kwenye sekta hii ya mawasiliano. Ni matumaini yetu wahusika na wadau wote watakutana na kuweza kulitafutia mchakato madhubuti kwa kuwatetea watumiaji wa simu na internet nchini Tanzania na vile ili kuweza kuleta maendeleo nchi nzima na kuwawezesha ata Mtanzania aliyepo Chato au Sumbawanga aweze kupata fursa ya kuunganishwa na dunia kwa kupata viwango vya bei iliyo nzuri na viwango vikubwa vya internet. Vile vile kuanzia sasa haya makampuni ya simu kamwe yasifumbiwe macho kwa bei wanazozipanga kwenye huduma ya mawasiliano kwa maana yanawanyonya Watanzania ambao ni masikini kwa manufaa yao!
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,260
2,000
Kuna kifurushi cha internet cha airtel cha mb300 kwa sh 500 nilikizoea sana na nilishangaa tarehe 11/8/2016 wamekibadili kuwa mb150 kwa sh 500!
Sijui kwa mitandao mingine ila hili la airtel limenisononesha sana!
 

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,478
2,000
Yan nimenunua mda c mrefu Airtel 150 kwa mia 5 Hal hi I sio saw a hatua zichukuliwe kurekebisha hi I hali
 

pendoharri

JF-Expert Member
Aug 5, 2016
508
500
Tumemchagua wenyew.kipenz chetu wenyew acha waisome number heeee ccm mbele kwa mbele.WALIJUA WATAKAOISOMA NUMBER NI WAPINZANI TUU.kumbe ni wotee
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
16,177
2,000
Yaani ajabu ni kwamba tunategemea mfanyabiashara yeyote akiisha jiimasha katika soko lenye uhakika hupunguza bei ya bidhaa yake ili kuwafavour wateja wake aliotoka nao mbali.hasa kama amerudisha mtaji.

Ajabu hawa jamaa wa mitandao na data sjui wanaendaje!!!!!???, hapa nimejituliza kwa halotel,ila sina amani kabisaa.kama nimelala koridoni.

Muda wowote kinanuka.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom