Nimesikiliza baadhi ya michango ya wabunge wetu juu ya Corona nikabaki na maswali mengi najiuliza hawa wanaongea bungeni kama watu gani?
Anasimama mbunge bungeni anachangia mjadala kwa kuelezea Corona ni nini? Inasambaa vipi? na kibaya zaidi anahitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi ni kitu gani wafanye.
Hizi kweli mbunge ndivyo anavyotakiwa kufanya? Yawezekana hujaona tatizo lakini ngoja nikuelezee mtizamo wangu.
Yaani ukimsikiliza mtaalamu wa wizara ya afya anavyofafanua Corona na kushauri nini cha kufanya, ndivyo mbunge naye unavyomsikia akijadili korona bungeni, ndivyo unavyomsikia layman akijadili Corona mtaani.
Hii inaonyesha tatizo maana wataalamu, wawakilishi wa wananchi na wananchi ni lazima aongee kwa nafasi yake.
Tukiwa mtaani kuna mengi yanasemwa juu ya Corona, wananchi tumesikia mengi hasa kupitia mitandao ya kijamii:
1. wapo wanaosema ugonjwa huu umetengezwa na watu kwa ajili ya biashara kwa madai kwamba wametengeneza wadudu wakaletwa na kutengeneza panic alafu wakaenda kuleta suluhisho la tatizo walilolitengeneza wao wenyewe kutuuzia.
2. wapo wanaosema Corona imetokana na wachina kula popo.
3. wapo wanaosema ugonjwa huu hutokea kila baada ya miaka 100 kwani huko nyuma yalishatokea kama "spanish flue".
4. Yapo mengi yametokea mfano kuna wengine wametengeneza dawa zao huko nje na wanataka kila mtu atumie hizo hizo hizo
5. Yapo mengi yameibuliwa juu ya dawa hizo kwa wengine kusema hiyo siyo dawa na kuhoji uhallali wake kwani technolojia ilitumika haijawahi kuruhusiwa kutumika kwa binadamu.
6. wapo wanaosema mda wa kuzalisha chanjo haikufuatwa na kuhoji iweje tufanyie majaribio kwa binadamu na kuhoji ikiwa kunaweza kutokea madhara makubwa.
7. kwa upande mwingine serikali yetu imetoa taarifa juu ya utafiti unaoendelea nchini kwa kutumia miti shamba na kufanikiwa kuzalisha baadhi ya tiba ambazo imesema zimeonyesha mafanikio mazuri.
8. serikali imeenda mbali zaidi na kutoa msimamo wake kwamba itaendelea kutumia tiba zilizozalishwa nyumbani na haina mpango wa kugiza chanjo nje.
9. taarifa hii imeonekana kupelekewa tofauti na mataifa ya nje kwani shirika la afya Dunia lilianza kwa kusema tanzania ijiandae kupokea tiba, mara ukitazama vyombo vya habari vya kimataifa mfano bbc imeandika makala yenye kichwa Conona Tanzania na kuishambulia kwa kukataa chanjo.
Mwananchi anasikia mengi na waswahili walisema miluzi mingi humpoteza mbwa, na huyu mwananchi ndiye amemtuma mbunge wake kwenda kumuwakilisha katika kuongea na serikali yake.
Wananchi tulitegemea kusikia wawakilishi wetu wakieleza changamoto iliyopo kwa mwananchi kutokana na taarifa nyingi zilizoko mtaani na kwa kutoa mfano yanayoelezwa na kuiomba kuiuliza serikali mfano yafuatayo:
1. Yapo mengi yanahusishwa na chimbuko la virusi vya Corona ikiwemo uhalifu juu ya binadamu, je serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inajiridhisha na chimbuko la ugonjwa huu kabla ya kuingia kwenye mfumo wa biashara ili kama kweli ni uhalifu kuhakikisha haisapoti uhalifu kwa namna yoyote ile.
2. Yapo mengi yanazunguzwa juu ya techolojia iliyotumika kutengeneza chanjo na kudai haifai kwa matumizi ya binadamu kwa sasa, je serikali imefanya juhudi gani za kufuatilia kinachofanyika ili kubaini manufaa na madhara kwa binadamu. tukumbuke serikali ilitunga sheria ya kuzuia matumizi ya GMO katika kilimo na technolojia iliyotumika inahusishwa kwa ukaribu na technolojia hii, je kama serikali ilipiga marufuku kwenye kilimo ni nini msimamo wa serikali juu ya matumizi ya technojia kama hizi kwa wananchi wetu
3. ni jitihada gani serikali inazozifanya kujenga uwezo wa ndani katika kutafiti na kuzalisha kinga, tiba na vifaa, pamoja na wataalamu wa kukabiliana na changamoto kama hizi na nyingine za kiafya.
Na sio mbunge kusoma makala fulani anaikalili hiyo na akipewa mda wa kuchangia basi yeye ndiye anayekuwa kama mtaalamu akiwaelekeza watanzania kilichopo ni kitu gani na nini cha kufanya. Waeleze waliyoyasikia kwa mantiki ya kujenga hoja ya kushauri na kuielekeza serikali katika nini cha kufanya.
Huo ni mtizamo wangu karibu kwa maoni