Hoja ya Brigedia generali leonard mndeme ina mantiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya Brigedia generali leonard mndeme ina mantiki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Polisi, Feb 21, 2011.

 1. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wakuu mimi ni mmoja wa watanganyika wengi ambao hatukuona mkutano wa jwtz na wahariri wa vyombo vya habari kutokana na side effect ya dowans. Leo bahati nzuri nimebahatika kuangalia marudio kupitia itv. Nimewasikiliza kwa makini sasa wasemaji wote wawili na nimekuja na summary ifuatayo;
  1.je ni JESHI ndilo linalopaswa kuwa mbali na wananchi au WANANCHI ndo
  wanaopaswa kukaa mbali na jeshi
  2.siku chache kabla ya milipuko UKAGUZI
  ulikuwa umefanyika na mkaguzi
  alikuwa bado hata hajakamlisha repoti
  na kutoa recommendations zake
  3 Baada ya milipuko ya mbagala,
  tahadhari zote zilishachukuliwa
  kuhakikisha kuwa milipuko haitokei
  tena MBAGALA.
  4. Jeshi lina watalaam na hivi karibuni
  kuna vijana wamerudi toka CHINA
  5. Jeshi LILIFURAHI SANA wananchi wa
  mbagala kulipwa fidia
  MY CONCERN KWA KILA HOIA 1-5
  1.Wananchi ndo wanapaswa wakae mbali
  na kambi za jeshi
  2.Wakaguzi wa jeshi hawako huru
  3.Emphasis ingekuwa ni kuhakikisha
  milipuko haitokei popote tz badala ya
  mbagala tu
  4. Whether China ni nchi sahihi katika
  masuala ya kijeshi au la
  5. Fidia si mbadala wa roho za watu na
  hivyo si kitu cha kufurahia

  naomba kuwasilisha wakuu
   
 2. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Tatizo JWTZ wangepaswa kutoa elimu kuhusu madhara ya kujenga karibu na kambi za jeshi,lakini tatizo utaambiwa hakuna pesa za kuandaa programu kama hyo,na wakati mwingine w2 wanatafuta huduma muhimu km maji,umeme,tiba n.k ndo mana wananchi huwa tunajenga huko karibu na makambi ya jwtz. Mi nafikiri kuwepo utaratibu wa kuwaelimisha wananchi kwa muda mrefu waelewe madhara yake endapo milipuko itatokea. Hivi waungwana nauliza mbona kwenye hifadhi ya barax2 tunajua vipimo vya umbali wa m2 kujenga nyumba? Ila natoa angalizo labda fedha zinatolewa kwa ajili ya kuhamisha kambi hizo au maghala ya silaha za milipuko ila zinachakachuliwa aidha na wakuu jwtz au sirikalini. Naunga hoja.
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Hii haingii akilini kabisa. 'Karibu na kambi' ni umbali gani kwani? Maana Shimbo siku ile mabomu yanalipuka nakumbuka aliwatahadharisha watu wakimbia umbali wa kilomita 10! Inamaana watu waahame miji wawaachie wanajeshi?
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Kuhusu makazi ya Jeshi, siyo kweli kuwa wananchi wndio wahame kuliacha jeshi. Kwa vile mji unapanuka haiwezekenai kungetengeza kisiwa cha kambi ya jeshi ndani ya jiji; jeshi ndilo linalotakiwa kuhamishwa kadri mji unavyopanuka. Kambi za jeshi zinatakiwe ziwe umbali wa takriban kilometa 25 kutoka makazi ya raia ili kusudi ikitokea milipoko ya namna hiyo, basi isifike kwenye makazi ya raia. Kwa wenzetu hata duka la baruti halitakiwi liwe karibu na makazi ya raia, kwa mfano, huko Tennesee ambako kunasifiwa kwa maduka ya baruti utayakuta yamejitenge sehemu ambazo hakuna nyumba nyingine zaidi ya duka hilo peke yake. Na hayawez kuwepo maduka mawili sehemu moja.

  Ni jambo la kushangaza kuwa mabomu hayo yanatuznzwa karibu na uwanja wa ndege za kiraia wenye hadi ya kimataifa, aibu gani hiyo.
   
 5. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Labda wenzetu mliowahi kutembelea nchi za jirani na kukata mitaa mtujuze jinsi wenzetu wanavyokabiliana na changamoto hiyo
   
 6. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  stil in dillema,hv ni kambi ndo ilianza kuwepo au wakazi wa eneo husika ndo walianza?halafu hv mabomu huwa yana uwezo wa kusafiri kwa umbali gani?mana nimeskia hadi mengne yamepaa hadi mitaa ya kisarawe ,inakuaje hapo?halafu hv ktk milipuko kama hyo huwa wanajesh hawafi mana sijaskia idadi yani.
   
 7. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,629
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 160
  Issue hapa siyo wananchi kukaa mbali na kambi za jeshi. Je kukaa mbali ndio kutazuia milipuko? I hope they are not trying to say that it is ok for them military personnel kufa in such incidents.

  Kuongelea proximity ya raia na kambi za jeshi ni diversion ya hoja ya msingi kwanini mabomu yalipukea. Niseme tu kwa wale wasiojua maswala ya siraha za kijeshi kuwa uwa hazichagua target kama hazielekezwa vinginevyo (hapa itakuwa vigumu kwa swala la Gombolamboto maana ktk kesi hii yalichagua raia tu). Ninachojaribu kusema ni kuwa makombola ya kijeshi usafiri umbali tofauti sasa wanaoongelea makazi ya raia wanaweza kutuambia safe distance? Ndio maana nasema kuwa kuongelea makazi ya raia na kambi ni diversion. Vp ammunitions zilizo ktk vituo vya polisi zikilipuka? Waamishie vituo vya polisi maporini?

  Labda niulize je ktk kambi za jeshi hakuna raia au wote uwa ni wanajeshi? Vipi famili za wanajeshi wanaoshi kambini? Au wao ni collateral? Swala la kulipuka makombola ni uzembe tu period. Kwa msiofahamu mpaka leo hii kuna mabomu ya vita ya kwanza/pili ya dunia yanaokotwa lakini mpaka yawe disturbed ndio ulipuka.
   
 8. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  na kwa kigezo hicho basi Dar yote si salama kwa makazi ya raia.lakini pia ikumbukwe kuwa wakazi wa maeneo kama Majohe hawakuvamia eneo hilo,ila walipelekwa pale na serikali baada ya kutokea mafuriko ya maeneo waliyokuwa wakikaa.inaposemwa wananchi wasiishi maeneo ya karibu na jeshi ili hali ni makazi hali waliyopatiwa na jeshi hainiingii kichwani!
  kwa wale walio nje au mbali na maeneo ya jeshi nao wamethibitisha mabomu kuanguka katika maeneo yao,mfano kuna mabomu yameanguka chanika, kimara, na hata mbande!nini maana yake kwamba maeneo yote hayo yawe wazi kwa vile kuna kambi ya jeshi gongolamboto!!!
  serikali imekuwa ikijinadi kulibadilisha jeshi letu kuwa la kisasa,huo ndo usasa wa mabomu kulipuka?wakati wa mwalimu jeshi lilisheheni askari wengi waliokuwa wameishia darasa la saba,na wengine hata kusoma walikuwa hawajui!lkn hatukuwahi kusikia mabomu kulipuka isipokuwa sasa ambapo jeshi ni la wasomi!!!!!inanifikirisha sana!!
   
 9. m

  mzee wa inshu Member

  #9
  Feb 22, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ah! sisi hao tumeisha choka nao.

  Hakuna cha wataalamu waJWTZ wala Wachina, most of our army generals are mbumbumbus!.

  Hata wao hawakujua kama yanaweza kulipuka endapo yanaifadhiwa hovyo.!

   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  we polisi

  hivi waliotoa vibali vya ujenzi, wakapeleka umeme na maji na wakatengeneza barabara ni raia??

  we have a big problem and we want to solve the problem using very light statements and analysis
   
 11. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #11
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  jibu liko wazi. Corruption
   
 12. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  mkuu wewe ni mmoja wa wanajf ambao huwa nawaheshimu heshimu. Kuna issues mbili. Moja ni mabomu kulipuka. Pili watu kufa na kujeruhiwa. Mimi concern yangu, kinachoniuma zaidi ni watz kufa na wengine kuachwa na vilema. Mabomu kulipuka pekee siyo issue
   
 13. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Aibu kwa mtu asiyejua maana ya ulinzi. Lakini wanaojua hata hawazungumzii hoja za kipuuzi namna hiyo. Ongelea kuhusu cause ya explosion na nini kinafanywa na jeshi kuzuia hali hiyo isijitokeze. Jeshi ndio ma-expert, hivyo hatuwezi kuwashinikiza wafuate matakwa yetu kwa vile tu tuko carried away na emotions zetu. Hatuwezi hata kupanga ulinzi wa nyumba zetu wenyewe. Ndo maana twataka kila baada ya mita kumi pawepo kituo cha polisi. So, waheshimu walau katika suala la ulinzi kwani hata kama wewe una PHD ya kiraia, bado you can,t compare to a mere private soldier. We mwana una pesa ya kuhamisha kambi kila mji unapotanuka? Je, wajua miji mingi ina makambi makubwa ya kijeshi? Kwa nini usiongelee mipango miji ambao walipaswa kuona mbali zaidi? Unfortunately jeshi ni necessary evil.
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Feb 22, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa ni kutokuwa na uwajibikaji Tanzania.
   
 15. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hapana bana. Mtanzania wa kawaida say waliothirika na milipuko ya mabomu kule gongo la mboto na mbagala utamuonea ukisema ajadili cause ya explosion. jeshi ndo wanaweza kujua cause then wananchi tuambiwe jinsi ya kufanya
   
 16. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Then let us listen to the experts
   
Loading...