Hoja wanaotetea awamu ya tano na wanaoipinga kwa hoja

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
MISTARI IMESHACHORWA - THANKS RADIO DW - NI KATI YA UZALENDO NA MASLAHI BINAFSI

UTANGULIZI
Midahalo ya DW radio imeonyesha mwelekeo wa uchaguzi wa mwaka 2020. Kuna pande mbili zinazopingana. Upande mmoja ni wa Tanzania wengi wanaiona hali ya maisha ilivyobadilika kuwa ngumu kuanzia mwaka 2016. Hilo ni kundi lenye wafuasi na wanachama wa vyama vya upinzani (UKAWA), wanaharakati, viongozi wengi wa kidini, wafanyakazi, wakulima na wafanyiashara.

Upande mwingine kuna kundi la viongozi wa CCM na serikali yao. Kundi hili lina watendaji wa serikali, wabunge wa CCM na baadhi ya wananchi. Hawa wanasema maisha yao wao yamekuwa bora kuliko katika kipindi chote cha historia ya Tanzania baada ya Uhuru. Wanasema hakuna rais aliyewahi kuboresha maisha yao wao kama huyu wa sasa.

KUNDI LA KWANZA LINATETEA HOJA ZAKE KWA MIFANO
1. Ripoti ya National Board of Statistics ya June l, 2019 inaonyesha ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018. Hii ni sawa na kupungua kwa asilimia 42.6%

Inaonyesha pia kwamba Ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.

Pamoja na serikali kudai imejenga viwanda Zaidi ya 3000 lakini hali ya ajira ni mbaya kuliko wakati mwingjne wo wote katika historia ya Tanzania. Wahitimu wengi wa vyuo vikuu hawajaajiriwa na wengine wao wana zaidi ya miaka 3 wako mitaani.

2. Kupungua kwa shughuli za kibiashara katika kipindi cha serikali ya awami ya 5 ni kwasababu ya mazingira yasiyoridhisha kwa wawekezaji ikiwemo urasimu katika upatikanaji wa vibali na utitiri wa kodi, tozo pamoja na maofisa wa TRA wasiyo na utu kwa wafanyibiashara.

3. Hali za wakulima ni mbaya na mfano ni wakulima wa korosho. Wakulima wa mazao mengine nao pia wako taabani. Serikali imeharibu mifumo ya uzalishaji na biashara ya mazao ya kilimo iliyokuwepo hapo awali.

4. Wafanyakazi hali zao ni mbaya sababu hawajapewa haki zao za kupandishiwa mishahara yao kila mwaka. Sasa ni miaka 4 mishahara haijapanda. Wengine wamestahafu na hawajalipwa pension zao huu mwaka wa 4 sasa. Posho walizokuwa wanalipwa wafanyakazi wakati wa serikali ya awamu ya 4 zimeondolewa.

5. Vyama vya upinzani havina haki ya kukutana na kufanya mikutano yao hadhara na ya ndani lakini wanazuiwa kufanya hivyo. Haki hizo wanazo wao ccm tu.

6. Vyama vya upinzani havina haki ya kukosoa serikali. Wanalipwa ruzuku ili wafanye siasa lakini wanazuiwa kufanya kazi yao hiyo ya kikatiba/kisheria.

7. Wanaharakati, viongozi wa upinzani, wanahabari na wakosoaji wengine wa serikali wanapotezwa au kuteswa na watu wanaoitwa wasiojulikana kila wanapotumia haki yao ya kikatiba kutoa maoni yao juu ya maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi yao.

8. Vyombo huru vya habari vinazuiwa kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu, kutowajibika, ubadhirifu na ufisadi ndani ya serikali.

KUNDI LA PILI NA HOJA ZAKE
Kundi la pili linatetea msimamo wake kwa kurejea hatua hizi zilozochukuliwa na serikali, pengine kwa lengo la kuboresha hali ya kiuchumi:

Imefungia Bureau de change
Imefunga mabenki
Imegungia Bunge Live
Imefungia Safari za nje
Imeondoa wafanyakazi wenye vyeti feki
Imeondoa mishahara hewa
Na baada ya hatua hizi serikalii iliweza kufanya haya:
Kumaliza miradi michache ya miuondombinu ikiwemo baadhi ya barabara na daraja la Tazara.
Imenunua Ndege
Imeondoa karo za shule za msingi na secondary
Imeanza ujenzi wa reli ya kati (SGR)
Imeanza ujenzi wa mradi wa Umeme wa Stigler's Gorge
Imenunua meli ya ziwa Victoria nk

YATOKANAYO NA HOJA ZA UPANDE WA SERIKALI
Orodha ya upande wa serikali ni ushahidi kwamba awamu ya 5, kama serikali zote zilizokuwepo baada ya Uhuru, inajenga miundombinu na kufanya ununuzi. Mradi ambao ungeweza kubadili hali za kiuchumi za waTanzania wengi ni reli ya kati lakini kwa vile ni mradi mkubwa, haijulikani utaisha lini maana vyanzo vya ufadhili wenyewe havina uhakika. Uwezekano wa reli ya kati kujengwa na kumalizwa na serikali ya awamu ya 5 haupo.

Mradi wa Stiegler's Gorge unapigiwa kelele nchini na nje ya nchi kuwa unaharibu mazingira. Hoja nyingine ya wapinzani kupinga mradi huo ni uwezekano wa kuwa uendelevu kwa uzalishaji wa Umeme.

Miradi ya Umeme wa maji ya Mtera na Kidatu ilijaa mchanga kabla ya kutumiza miaka 20 ya uzalishaji wa umeme. Matatizo ya silting (kujaa tope) yaliyoipata Mtera na Kidatu yataipata pia Stiegler's Gorge maana hakuna tahadhari yo yote iliyochukuliwa dhidi ya silting. Kwa maana hiyo mradi ukiisha itachukua miaka 15 halafu matatizo ya tope yataanza na kuathiri uzalishaji wa Umeme. Baada ya muda huo nchi itarudi tena kwenye mgao wa Umeme.

Orodha haionyeshi serikali imefanya jambo la tofauti kulinganisha na serikali zingine zilizopita. Tokea Tanganyika ipate Uhuru hakuna awamu ya serikali ambayo haikujenga miuondombinu na kufanya manunuzi. Vitu vinavyojitokeza sasa, tofauti na huko nyuma ni hali ya ufukara kuongezeka miongoni mwa wananchi walio wengi. Lingine ni haki za kibinafamu kuvunjwa sasa zaidi kuliko wakati mwingine wo wote.
.
Wanaoisifu serikali kwamba ni bora kuliko zote bila shaka wanaangalia maslahi yao wao binafsi na hasa maslahi ya viongozi. Tatizo lililopo ni kwamba serikali haiundwi ili iwahudumie viongozi au ihudumie kundi moja dogo la wananchi peke yao. Serikali ya wananchi inatakiwa igawe raslimali za taifa kwa ulinganifu.

Bajeti kiasi gani ipelekwe.Wilaya ipi kilichokuwa kinazingatiwa huko nyuma ni wapi itapatikana manufaa ya kitaifa makubwa Zaidi. Manufaa ya kiuchumi na kijamii. Hizo indizo zilikuwa kazi za tume ya taifa ya mipango. Serikali ya awanu ya 5 imevunja tume ya mipango na sababu ya uamuzi huo ni ili ielekeze nguvu kubwa ya raslimali za taifa kwenda Geita, Simiyu na baadhi ya mikoa mingine ya kanda ya ziwa.

Mfano mbunge Msukuma, kwenye mahojiano na DW radio, anaposema anaipenda serikali ya sasa kwa sababu hakuna serikali iliyowahi kupeleka Geita miradi yenye thamani ya shillings billion 20, hakusema kama mikoa mingine nayo pia ina miradi yenye thamani hiyo. Kama mikoa yenye miradi ya thamani kubwa yote iko kanda ya ziwa, kumbe ndiyo maana baadhi ya wananchi wa kanda ya Ziwa wanaona serikali ya sasa kwao wao ni nzuri kuliko serikali zote zilizopita.

HITIMISHO
Hakuna kilichofanywa na serikali ya awamu ya 5 cha kuwashawishi wananchi waichague na tena mwaka 2020. Hata hivyo bila tume huru ya uchaguzi maana yake uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ni sawa na kuchezea fedha za wananchi kufanya uchaguzi. Uchaguzi huo hauna maana kwa sababu wananchi hawako huru kumchagua rais, mbunge au diwani wanayemtaka. Ye yote yule atakayesimamishwa na serikali ya ccm atatangazwa ndiye mshindi bila kujali kwamba wananchi hawamtaki.

Mungu ibariki Tanzania ili kipindi hiki kigumu kipite haraka.
 
Kundi ni moja tu ...yaani kundi la maendeleo.Hayo Mengine ni kama saidia fundi tu
 
Jamaa yangu nilikuwa nachati nae jana mkulima wa korosho huyu mkuranga huko

[21/01, 06:15] : Korosho nazo ndio zimeganda tu godown
[21/01, 06:16] : Nyxxxxo wamepata mteja wa 800, kixxxx nasikia wamepata mteja wa 950, nyaxxxx wameuza kwa 1000, sisi kaja mteja ana 650 sijui tuna gundu gani aisee

Hili ni zao ambalo soko lilikuwa uhakika na mkulima alikuwa akiuza kwa shilingi elf 4 kwa kilo moja.
Sasa nadhani hawa wapiga dili tumewafix sasa hali imekuwa shwari na wakulima wote waliokuwa wanaishi kiujanja ujanja kwisha habari yao
 
Tukiacha kuwa mazezeta ndio tunaweza kuelewa vizuri UTOFAUTI mkubwa kati ya kundi la kwanza na la pili. Hata hivyo Rais bora ni yule anayefanya yale ya kundi la kwanza, Yale ya kundi la pili kila ajae anaweza kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kundi ni moja tu ...yaani kundi la maendeleo.Hayo Mengine ni kama saidia fundi tu

Tusiandikie mate, Mimi na ww tulikubaliana toka februari 2016 kuwa ww utatoa taarifa za ujenzi wa viwanda, hasa propaganda ya viwanda 100@mkoa. Nilikuambia hilo haliwezekani, na ww ulisisitiza hilo linawezekana maana tumepata rais na serikali makini. Huu ni mwaka wa mwisho wa huyo rais na serikali makini. Weka list ya viwanda 100@ mkoa kuonyesha kuwa kuna kubwa la kujivunia. Hiyo miradi mikubwa miwili ya SGR & SG haina uhakika wa kumalizika wakati wa Magufuli kulingana na matarajio.
 
MISTARI IMESHACHORWA - THANKS RADIO DW - NI KATI YA UZALENDO NA MASLAHI BINAFSI

UTANGULIZI
Midahalo ya DW radio imeonyesha mwelekeo wa uchaguzi wa mwaka 2020. Kuna pande mbili zinazopingana. Upande mmoja ni wa Tanzania wengi wanaiona hali ya maisha ilivyobadilika kuwa ngumu kuanzia mwaka 2016. Hilo ni kundi lenye wafuasi na wanachama wa vyama vya upinzani (UKAWA), wanaharakati, viongozi wengi wa kidini, wafanyakazi, wakulima na wafanyiashara.

Upande mwingine kuna kundi la viongozi wa CCM na serikali yao. Kundi hili lina watendaji wa serikali, wabunge wa CCM na baadhi ya wananchi. Hawa wanasema maisha yao wao yamekuwa bora kuliko katika kipindi chote cha historia ya Tanzania baada ya Uhuru. Wanasema hakuna rais aliyewahi kuboresha maisha yao wao kama huyu wa sasa.

KUNDI LA KWANZA LINATETEA HOJA ZAKE KWA MIFANO
1. Ripoti ya National Board of Statistics ya June l, 2019 inaonyesha ajira rasmi zilizotengenezwa na sekta binafsi zimepungua kutoka 239,017 mwaka 2016/2017 hadi kufikia ajira 137,054 mwaka 2017/2018. Hii ni sawa na kupungua kwa asilimia 42.6%

Inaonyesha pia kwamba Ajira rasmi zilizotengenezwa na Serikali zilipungua kutoa 82,302 hadi 18,000 ikiwa ni sawa na anguko la asilimia 78.1 katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.

Pamoja na serikali kudai imejenga viwanda Zaidi ya 3000 lakini hali ya ajira ni mbaya kuliko wakati mwingjne wo wote katika historia ya Tanzania. Wahitimu wengi wa vyuo vikuu hawajaajiriwa na wengine wao wana zaidi ya miaka 3 wako mitaani.

2. Kupungua kwa shughuli za kibiashara katika kipindi cha serikali ya awami ya 5 ni kwasababu ya mazingira yasiyoridhisha kwa wawekezaji ikiwemo urasimu katika upatikanaji wa vibali na utitiri wa kodi, tozo pamoja na maofisa wa TRA wasiyo na utu kwa wafanyibiashara.

3. Hali za wakulima ni mbaya na mfano ni wakulima wa korosho. Wakulima wa mazao mengine nao pia wako taabani. Serikali imeharibu mifumo ya uzalishaji na biashara ya mazao ya kilimo iliyokuwepo hapo awali.

4. Wafanyakazi hali zao ni mbaya sababu hawajapewa haki zao za kupandishiwa mishahara yao kila mwaka. Sasa ni miaka 4 mishahara haijapanda. Wengine wamestahafu na hawajalipwa pension zao huu mwaka wa 4 sasa. Posho walizokuwa wanalipwa wafanyakazi wakati wa serikali ya awamu ya 4 zimeondolewa.

5. Vyama vya upinzani havina haki ya kukutana na kufanya mikutano yao hadhara na ya ndani lakini wanazuiwa kufanya hivyo. Haki hizo wanazo wao ccm tu.

6. Vyama vya upinzani havina haki ya kukosoa serikali. Wanalipwa ruzuku ili wafanye siasa lakini wanazuiwa kufanya kazi yao hiyo ya kikatiba/kisheria.

7. Wanaharakati, viongozi wa upinzani, wanahabari na wakosoaji wengine wa serikali wanapotezwa au kuteswa na watu wanaoitwa wasiojulikana kila wanapotumia haki yao ya kikatiba kutoa maoni yao juu ya maswala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi yao.

8. Vyombo huru vya habari vinazuiwa kutoa taarifa juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu, kutowajibika, ubadhirifu na ufisadi ndani ya serikali.

KUNDI LA PILI NA HOJA ZAKE
Kundi la pili linatetea msimamo wake kwa kurejea hatua hizi zilozochukuliwa na serikali, pengine kwa lengo la kuboresha hali ya kiuchumi:

Imefungia Bureau de change
Imefunga mabenki
Imegungia Bunge Live
Imefungia Safari za nje
Imeondoa wafanyakazi wenye vyeti feki
Imeondoa mishahara hewa
Na baada ya hatua hizi serikalii iliweza kufanya haya:
Kumaliza miradi michache ya miuondombinu ikiwemo baadhi ya barabara na daraja la Tazara.
Imenunua Ndege
Imeondoa karo za shule za msingi na secondary
Imeanza ujenzi wa reli ya kati (SGR)
Imeanza ujenzi wa mradi wa Umeme wa Stigler's Gorge
Imenunua meli ya ziwa Victoria nk

YATOKANAYO NA HOJA ZA UPANDE WA SERIKALI
Orodha ya upande wa serikali ni ushahidi kwamba awamu ya 5, kama serikali zote zilizokuwepo baada ya Uhuru, inajenga miundombinu na kufanya ununuzi. Mradi ambao ungeweza kubadili hali za kiuchumi za waTanzania wengi ni reli ya kati lakini kwa vile ni mradi mkubwa, haijulikani utaisha lini maana vyanzo vya ufadhili wenyewe havina uhakika. Uwezekano wa reli ya kati kujengwa na kumalizwa na serikali ya awamu ya 5 haupo.

Mradi wa Stiegler's Gorge unapigiwa kelele nchini na nje ya nchi kuwa unaharibu mazingira. Hoja nyingine ya wapinzani kupinga mradi huo ni uwezekano wa kuwa uendelevu kwa uzalishaji wa Umeme.

Miradi ya Umeme wa maji ya Mtera na Kidatu ilijaa mchanga kabla ya kutumiza miaka 20 ya uzalishaji wa umeme. Matatizo ya silting (kujaa tope) yaliyoipata Mtera na Kidatu yataipata pia Stiegler's Gorge maana hakuna tahadhari yo yote iliyochukuliwa dhidi ya silting. Kwa maana hiyo mradi ukiisha itachukua miaka 15 halafu matatizo ya tope yataanza na kuathiri uzalishaji wa Umeme. Baada ya muda huo nchi itarudi tena kwenye mgao wa Umeme.

Orodha haionyeshi serikali imefanya jambo la tofauti kulinganisha na serikali zingine zilizopita. Tokea Tanganyika ipate Uhuru hakuna awamu ya serikali ambayo haikujenga miuondombinu na kufanya manunuzi. Vitu vinavyojitokeza sasa, tofauti na huko nyuma ni hali ya ufukara kuongezeka miongoni mwa wananchi walio wengi. Lingine ni haki za kibinafamu kuvunjwa sasa zaidi kuliko wakati mwingine wo wote.
.
Wanaoisifu serikali kwamba ni bora kuliko zote bila shaka wanaangalia maslahi yao wao binafsi na hasa maslahi ya viongozi. Tatizo lililopo ni kwamba serikali haiundwi ili iwahudumie viongozi au ihudumie kundi moja dogo la wananchi peke yao. Serikali ya wananchi inatakiwa igawe raslimali za taifa kwa ulinganifu.

Bajeti kiasi gani ipelekwe.Wilaya ipi kilichokuwa kinazingatiwa huko nyuma ni wapi itapatikana manufaa ya kitaifa makubwa Zaidi. Manufaa ya kiuchumi na kijamii. Hizo indizo zilikuwa kazi za tume ya taifa ya mipango. Serikali ya awanu ya 5 imevunja tume ya mipango na sababu ya uamuzi huo ni ili ielekeze nguvu kubwa ya raslimali za taifa kwenda Geita, Simiyu na baadhi ya mikoa mingine ya kanda ya ziwa.

Mfano mbunge Msukuma, kwenye mahojiano na DW radio, anaposema anaipenda serikali ya sasa kwa sababu hakuna serikali iliyowahi kupeleka Geita miradi yenye thamani ya shillings billion 20, hakusema kama mikoa mingine nayo pia ina miradi yenye thamani hiyo. Kama mikoa yenye miradi ya thamani kubwa yote iko kanda ya ziwa, kumbe ndiyo maana baadhi ya wananchi wa kanda ya Ziwa wanaona serikali ya sasa kwao wao ni nzuri kuliko serikali zote zilizopita.

HITIMISHO
Hakuna kilichofanywa na serikali ya awamu ya 5 cha kuwashawishi wananchi waichague na tena mwaka 2020. Hata hivyo bila tume huru ya uchaguzi maana yake uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ni sawa na kuchezea fedha za wananchi kufanya uchaguzi. Uchaguzi huo hauna maana kwa sababu wananchi hawako huru kumchagua rais, mbunge au diwani wanayemtaka. Ye yote yule atakayesimamishwa na serikali ya ccm atatangazwa ndiye mshindi bila kujali kwamba wananchi hawamtaki.

Mungu ibariki Tanzania ili kipindi hiki kigumu kipite haraka.
Hili bandiko limemaliza ubishi kuwa awamu ya tano ni serikali ya hovyo kuliko zote zilizopita
 
Tusiandikie mate, Mimi na ww tulikubaliana toka februari 2016 kuwa ww utatoa taarifa za ujenzi wa viwanda, hasa propaganda ya viwanda 100@mkoa. Nilikuambia hilo haliwezekani, na ww ulisisitiza hilo linawezekana maana tumepata rais na serikali makini. Huu ni mwaka wa mwisho wa huyo rais na serikali makini. Weka list ya viwanda 100@ mkoa kuonyesha kuwa kuna kubwa la kujivunia. Hiyo miradi mikubwa miwili ya SGR & SG haina uhakika wa kumalizika wakati wa Magufuli kulingana na matarajio.
Wengine anatoa hoja kwa data yeye anakalia maneno matupu Jingalao!
 
Nyuzi kuntu kama hizi hauwezi mkuta PASCHAL amechangia kitu. Amakweli police hawezi kuzaa watoto WAZARENDO.
 
Back
Top Bottom