Hoja: Umri Wa mwisho wa kuajiriwa Serikalini

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
3,317
2,000
Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza, Ajira nyingi zinazotangazwa na Serikali na Taasisi Mbalimbali huwa na Vigezo Vikubwa Viwili

1. Huwa Uzoefu Wa Kazi, Mara nyingi huwa wanataka mtu alie na uzoefu usiopungua Miaka 5 ya Kazi Au 3.

2. Lakini Kigezo cha Pili Huwa ni Umri Huwa wanataka Mtu asie Zidi Umri Wa Miaka 45. Kanakwamba Ukiwa na Umri Wa Miaka 46 Huwezi Kuajiriwa.

Kigezo cha Pili Kinanipa Maswali Mengi Sana. Kwanini Walio Na Umri Wa Zaidi Ya Miaka 45 Hawawezi Kuajiriwa ikiwa Umri wa Kustaafu Kwa Upande Wa Serikali Ni Miaka 55-60? Kwanini hadi ikifika umri wa miaka 58 mtu asiajiriwe kama Ana Uwezo? Lakini Pia Hii inasababisha Watu wenye Uzoefu mkubwa na kazi Fulani Kushindwa kuonesha/ Kutumia Uzoefu wao Kuisaidia Serikali kuleta maendeleo.

Lakini Swali Jingine kama Wenye umri wa Zaidi Ya Miaka 45 Hawatakiwi Kwanini Nafasi mbalimbali Za Serikalini Huteuliwa Watu wenye Umri Wa Zaidi Ya Miaka 45? Je Huwa hawazingatii kigezo hiki?

Nina Maswali Mengi Nakosa Majibu
 
Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
13,105
2,000
Mkuchika na Mahiga wameajiriwa wapi?.Kuna nafasi ili upewe lazima uwe mwanasiasa, umewahi kusikia tangazo la kuomba nafasi ya kuwa waziri likiambatana na masharti aliyoeleza mleta mada?.
mkuu kwa nilivoelewa mleta mada anauliza kikomo cha umri wa kuajiliwa serikalini hicho ndicho anataka kujua,kuhusu mkuchika si ameajiriwa serikalini ? naomba unieleweshe kama unafahamu zaidi
 
daudthefarmer

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,466
2,000
mkuu kwa nilivoelewa mleta mada anauliza kikomo cha umri wa kuajiliwa serikalini hicho ndicho anataka kujua,kuhusu mkuchika si ameajiriwa serikalini ? naomba unieleweshe kama unafahamu zaidi
Kaajiriwa kwa nafasi ipi? matangazo ya kazi yake ulishayaona wapi?

Unaweza kutifautisha kuajiriwa na kuteuliwa?
 
kikokotoo kipya

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
389
500
mkuu kwa nilivoelewa mleta mada anauliza kikomo cha umri wa kuajiliwa serikalini hicho ndicho anataka kujua,kuhusu mkuchika si ameajiriwa serikalini ? naomba unieleweshe kama unafahamu zaidi
Mkuu wewe ndio umekataa kuwa hakuna umri wa mwisho wa kuajiriwa serikalini, ukatoa mfano wa akina Mkuchika, na mimi nika kuuliza kwani mkuchika kaajiriwa wapi?.Nilichoeleza ni nafasi zao kama mawaziri, kama ndio ulikuwa unamaanisha kuwa wameajiriwa.Lakini vigezo vya kuajiriwa serikali ni kama mhusika alivyoeleza, kwa nafasi zinazotangazwa,ukiacha nafasi za kisiasa.
 
Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
13,105
2,000
Mkuu wewe ndio umekataa kuwa hakuna umri wa mwisho wa kuajiriwa serikalini, ukatoa mfano wa akina Mkuchika, na mimi nika kuuliza kwani mkuchika kaajiriwa wapi?.Nilichoeleza ni nafasi zao kama mawaziri, kama ndio ulikuwa unamaanisha kuwa wameajiriwa.Lakini vigezo vya kuajiriwa serikali ni kama mhusika alivyoeleza, kwa nafasi zinazotangazwa,ukiacha nafasi za kisiasa.
sawa mkuu,nilidhani wameajiriwa
 
kikokotoo kipya

JF-Expert Member
Dec 18, 2018
389
500
mkuu mtu kuajiriwa ni lazima yatoke matangazo ya kazi ?, ahsante kwa ufafanuzi lakini maana nilidhani kila mtumishi serikalini ameajiriwa akiwemo na rais
Mkuu serikalini kuna ajira za kudumu,na zisizo za kudumu,kuna kazi za kuteuliwa kama hizo za wakuu wa wilaya,mkoa,wakurugenzi,mawaziri nk.Kwa hizi za kuteuliwa vigezo huwa juu ya mteuaji mwenyewe atakavyoona inampendeza.Hizo hazina masharti kama alivyoorodhesha mleta uzi.
 
Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
13,105
2,000
Mkuu serikalini kuna ajira za kudumu,na zisizo za kudumu,kuna kazi za kuteuliwa kama hizo za wakuu wa wilaya,mkoa,wakurugenzi,mawaziri nk.Kwa hizi za kuteuliwa vigezo huwa juu ya mteuaji mwenyewe atakavyoona inampendeza.Hizo hazina masharti kama alivyoorodhesha mleta uzi.
pamoja sana mkuu,sasa nimeelewa
 
sawima

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
2,034
2,000
Sababu kubwa huwa ni kwamba mtumishi wa umma anatakiwa kuchangia miaka 15 Kwenye mifuko ya hifadhi za jamii kama pspf kwa hiyo ukiajiriwa na miaka 45 jumlisha na 15 inakuwa 60. Kiwango cha chini kuchangia ni hyo miaka 15

Sent using Jamii Forums mobile app

Wewe ndio umejibu swali la mleta mada labda kama watarekebisha sheria ya miaka ambayo mtumishi anatakiwa kudeposit hela ya pension ipungue basi umri wa kuajiriwa nao utapanda zaidi ya hiyo 45.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom