Hoja: Tuteue viongozi kutokana na wingi wa mali zao kwanza, kama ilivyo kigezo cha kuwatumbua wanapoiba mali

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Kama kuna mdau humu atufikishie hili bungeni.

Bunge lione umuhimu wa kuboresha sheria za uongozi wa Umma.

Ili pamoja na mambo mengine kigezo cha Mali kitumike kwanza kumuweka mtu katika uongozi.

Tuache kabisa hii tabia ya kuwapa uongozi watu maskini kwasababu hawana mbinu ya kutufikisha popote zaidi ya kuiba Mali.

Watu maskini wanapopata madaraka mawazo yao yote huwa ni kuiba tu na dezo dezo.

Hivi sasa viongozi wanateuliwa kwa ukada na vyeti halafu wanapokwapua Mali tunawatumbua kwa wizi wa Mali.

Kama Mali ni muhimu wakati wa kutumbua kwanini isiwe muhimu pia wakati wa kuteua?

Ebu fikiria, kama mtu ameweza kutafuta na kusimamia Mali zake binafsi kwa jasho na damu atashindwaje kusimamia Mali za Umma?

Kama bunge litaona Mali siyo ishu mhimu sana.

Basi wakafute na waondoe ile sheria ya makampuni binafsi kutakiwa kuonyesha Taarifa za kibenki kwenye kupata tenda za miradi.

Itawezekanaje mwenye kampuni ya mabilioni ya fedha kwenye mradi akasimamiwe na kiongozi kapuku maskini?

Wataongea nini cha maana zaidi ya kuombana rushwa!?

Kwasababu viongozi maskini hawa ndiyo wanaoleta vikanuni na visheria kandamizi kwasababu hawajawahi kutafta Mali kwa jasho.

Mfano!
  • Kiongozi anaamua kupitisha kanuni ya kudai leseni kwa kinyozi ambae kajiajili kwa shida, kajifunza kunyoa kwa shida, katafta wateja kwa shida, halafu pap! Kiongozi anamuomba leseni.
  • Mkulima anatafta mbegu kwa shida, analima kwa shida, anavuna kwa shida halafu kiongozi anakuja kudai mgao wa STAKABADHI GALANI (wakati selikali haijachanga chochote)
  • Fundi anajifunza ujuzi wake kwa shida au kwa kurithi, anafanya kazi zake kwa tabu ili apate kula Mara pap! Anaombwa leseni! (Maana yake arudi shule akalipe ada) Kama leseni ni mhimu kwanini msiwape semina fupi na Kuwakabidhi hizo leseni zenu kwasababu UJUZI WANAO TAYALI!
Ni kiongozi Maskini tu anaeweza kufanya maamuzi kama hayo.

Mwaka 1849 walipogundua ndege, hakukuwa na leseni za ufundi walifanya hivyo na wakafanikiwa.

Mtu mkubwa sana bwana FORD aliyebuni Ford ranger na magari mengine alikuwa fundi gereji asiye na leseni.

Hapa kwetu mtu anaefungua banda la biashara anatakiwa Afunge biashara ili aende manispaa ofisini kutafta leseni kwanza wakati bidhaa zote anazouza zinakatwa kodi.

Hapa kwetu mfanyabiashara anaelipishwa kodi kibao, mbele ya duka lake anaruhusiwa machinga auze bidhaa ileile bila kodi.

Ni kiongozi maskini tu anaeweza kufanya hayo! Lakini kiongozi mwenye Mali ni kiongozi mzuri zaidi.
 
Yaaah mtu hajawahi hata kisimamia banda la kuku 300 kwake leo unampa taasisi yenye assets aiongoze
 
Tajiri anatamaa ya maendeleo, maskini anatamaa ya kuiba ili awe tajiri kwanza!

tajiri anayetazama maendeleo ni yule aliye tayari kutumia utajiri huo kwa maendeleo,
si mpaka awe kiongozi.
 
Nilitaka nikuambie hujielewi ila nimeona nitakuwa nimekuonea.
Ipo hivi hao matajiri ndo wanaiba vingi
niishie hapo
 
ni hoja yenye mashiko.

lakini lazima tujue kwanza utajiri unaanzia kwa thamani ipi kwanza.maana mwingine utajiri kwake ni milioni 50 na haoni haja ya kuiba tena.
 
ni hoja yenye mashiko.

lakini lazima tujue kwanza utajiri unaanzia kwa thamani ipi kwanza.maana mwingine utajiri kwake ni milioni 50 na haoni haja ya kuiba tena.
Sheria itapendekeza kiwango minimum
 
nilitaka nikuambie hujielewi ila nimeona nitakuwa nimekuonea.
Ipo hivi hao matajiri ndo wanaiba vingi
niishie hapo
Ndiyo maana ukasita! Kwasababu hata Bibilia inasema!
Soma kitabu cha KUTOKA 18:21-22
" 21Lakini kuhusu mambo mengine, chagua miongoni mwa watu wote, watu wanaostahili, watu wanaomcha Mungu, waaminifu na wanaochukia kuhongwa. Wape hao mamlaka, wawe na jukumu la kuwasimamia watu katika makundi ya watu elfu, mia, hamsini na kumikumi. 22Hao ndio watakaokuwa na vikao kila siku kutatua matatizo ya watu. Matatizo magumu watakuletea wewe, lakini yale madogomadogo watayaamua wenyewe. Kwa njia hiyo utaweza kurahisisha kazi yako kwa vile watashirikiana nawe katika jukumu hilo
 
Back
Top Bottom