Hoja tano kwanini Mbowe anaonekana kubambikiwa kesi

Kutuhumiwa ni jambo moja kukutwa na hatia ni jambo lingine ila ikithibitika afungwe kama wengine tusisikie mambo ya fine tena tushamchoka.
 
Eeeeh Bhwanah,

Kumbe Mbowe yupo ndani kwa sababu ya kukaidi amri?

Si basi isemwe hivyo, kwanini kulembalemba na haya ya ugaidi.

Kuna sehemu yoyote ndani ya sheria zetu ambako mtu "kukaidi amri" ni kosa, au ni mazoea ya ujinga ujinga tu?
Huo ujinga ujinga ndio umemfikisha hapa Mbowe.
 
Awe amebambikiwa au hajabambikiwa ila alijua atakamatwa.Yupo kwenye siasa zaidi ya miaka 20 kwahiyo alijua wazi CCM wasingeruhusu kufanyika maandamo na makongamano lakini hakujali kwa kuwa umaarufu wa kisiasa na kutengeneza picha Chadema wanaonewa ni muhimu zaidi.

Mama Samia alipoomba apewe muda zaidi ilikuwa ni amri sio ombi ila yeye na Chadema mlikuwa mnapima upepo kwa makusudi muone atawakamata kweli au atawaacha, akiwaacha mnaendelea kuhamasisha maandamano na mkikamatwa inajengeka picha mnaonewa so kwa vyovyote mtapata public attention.

Mlimjaribu Rais amewapigia.

... kwani Rais SSH aliombwa au alilazimishwa ashiriki ktk makongamano ya CDM ya kujadili katiba mpya?

... Mamlaka kuanza kuwakamata CDM kwasababu ya makongamano yao kunaonyesha kwamba kauli za Rais kwamba atashughulikia suala la katiba zilikuwa za ulaghai.

... Na huo uchumi aliosema anaurekebisha ndio huu wa kutukamua wananchi bila haruma kwa kutuongezea kodi na tozo za miamala?
 
..kwani Rais SSH aliombwa au alilazimishwa ashiriki ktk makongamano ya CDM ya kujadili katiba mpya?

..Mamlaka kuanza kuwakamata CDM kwasababu ya makongamano yao kunaonyesha kwamba kauli za Rais kwamba atashughulikia suala la katiba zilikuwa za ulaghai.

..Na huo uchumi aliosema anaurekebisha ndio huu wa kutukamua wananchi bila haruma kwa kutuongezea kodi na tozo za miamala?
Hakusema atashughulikia muda mnaotaka Chadema, hamna mamlaka ya kumuamrisha.

Kuhusu tozo za miamala, ni kodi rahisi inayolipika na inayokwepeka pia. Unataka wakuongezee kwenye kodi ya mapato ndio ujue hela inahitajika? Tozo za miamala hazikufilisi wala kukutajirisha acha kujitia unyonge usiokuwa nao.
 
..Makongamano ya Chadema hayamzuii Rais kuendelea na ratiba na malengo aliyojipangia.
 
Wao watengeneze sana hayo makesi lakini mwisho tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi ili kuepukana na wabunge dizaini ya Gwajima na kina msukuma
 
Mimi Kwa jicho la tatu naona kama hapa mama anauzwa na wasaidizi wake Kwa sababu amini kabisa suala la katiba si chadema tu hata ccm wanatamani Sana na wanajua sio rahisi kutumia ngozi zao halisi kudai Kwa sababu kumuita mbowe gaidi ni kumpa umaarufu zaidi especially umeenda kumkamata kwenye hotel tena akiwa anajiandaa Kwa ajili ya kongamano yaani unataka kuamini afanye ugaidi mwaka Jana muanze upelelezi halafu mlipoukamilisha ndo mmkamate basi sio gaidi tena
 
Hamumsaidii Mbowe. Mnajazwa upepo na wanaharakati ambao taarifa yoyote hasi ni "mpunga" kwao. Strategy ya matusi na ubabe imefeli. Strategy ya maandamano ilikufa kabla haijazaliwa. Only viable option ni dialogue. Lakini dialogue haiwezekani kwa sababu kuu mbili

1. Dialogue haiwezekani mahala pasipo na ustaarabu. Ni muhimu kuheshimiana kabla ya kufanya maongezi.

2. Radical elements zinazohusiana na chama chenu hazitokubali. Mfano hai, leo wanaharakati wanawashurutisha mumng'oe Pambalu na Moza kisa kukubali/kutoa dhamana polisi. Apparently wanaharakati wanataka wote waliokamatwa wagomee dhamana.

Kuna ombwe la uongozi katika chama chenu ndio maana outsiders wana sauti kuliko viongozi halali. Ila maslahi yao na yenu ni tofauti. Hamuwezi kuwatumia ilhali wao wanawatumia.

Dialogue is only way forward. Inaweza isizae matunda leo lakini it's better than hizo Spaces za kila siku mnajazana upepo.

Mwisho, tuhuma dhidi ya Mbowe ni nzito. Whether ni kweli au la, walioandaa kesi hiyo wamejipanga. Ndio maana hujaona Ubalozi wowote wa kimataifa ulioingilia kati suala hilo. Intelligence zao zimewaambia kutojihuisisha na kesi hiyo (lile tamko la Seneti ya Marekani lilikuwa kabla polisi hawajataja ugaidi)
 
Hamumsaidii Mbowe. Mnajazwa upepo na wanaharakati ambao taarifa yoyote hasi ni "mpunga" kwao. Strategy ya matusi na ubabe imefeli. Strategy ya maandamano ilikufa kabla haijazaliwa. Only viable option ni dialogue. Lakini dialogue haiwezekani kwa sababu kuu mbili
1. Dialogue haiwezekani mahala pasipo na ustaarabu. Ni muhimu kuheshimiana kabla ya kufanya maongezi.
2. Radical elements zinazohusiana na chama chenu hazitokubali. Mfano hai, leo wanaharakati wanawashurutisha mumng'oe Pambalu na Moza kisa kukubali/kutoa dhamana polisi. Apparently wanaharakati wanataka wote waliokamatwa wagomee dhamana.

Kuna ombwe la uongozi katika chama chenu ndio maana outsiders wana sauti kuliko viongozi halali. Ila maslahi yao na yenu ni tofauti. Hamuwezi kuwatumia ilhali wao wanawatumia.

Dialogue is only way forward. Inaweza isizae matunda leo lakini it's better than hizo Spaces za kila siku mnajazana upepo.

Mwisho, tuhuma dhidi ya Mbowe ni nzito. Whether ni kweli au la, walioandaa kesi hiyo wamejipanga. Ndo maana hujaona Ubalozi wowote wa kimataifa ulioingilia kati suala hilo. Intelligence zao zimewaambia kutojihuisisha na kesi hiyo (lile tamko la Seneti ya Marekani lilikuwa kabla polisi hawajataja ugaidi)
Wewe ni unajulikana, jibu hoja hapo juu
 
..hakuna ushindani wowote.

..mnamtisha mama wa watu bila sababu.

..dhuluma na kutesa wapinzani imekuwa ni mradi / ulaji wa baadhi ya watu kwenye system.
Upinzani usio na weledi hauna tija kwa maslahi mapana ya nchi. Alafu tunapozungumzia upinzani sio Chadema tu.
 
Upinzani usio na weledi hauna tija kwa maslahi mapana ya nchi. Alafu tunapozungumzia upinzani sio Chadema tu.

..Na chama tawala kisicho na weledi kama CCM ni mzigo kwa wananchi.

..kwa sasa hivi wananchi tunathirika zaidi na sera na utendaji mbovu wa CCM kuliko mapungufu waliyonayo wapinzani.

..Na CCM inaelekea kudhoofika kifikra na kimaarifa jinsi ktk kila utawala unaoingia nchi hii. Nimekua nikiiona CCM, viongozi wake, makada, na wabunge wake, chama kimekuwa cha hovyo-hovyo.
 
Back
Top Bottom