HOJA: Serikali ipo sahihi kwa hili la watoto wa kike wanaopata mimba mashuleni?

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Huu ni mjadala mpana na mrefu sana kwa sababu unaibua maoni na hisia za watu tofauti tofauti. Wapo wanaoilaumu serikali. Na wapo wanaomlaumu mtoto wa kike anayepata mimba akiwa kwenye masomo. Lakini ili kupata jawabu la kitendawili chetu, kwa mtazamo wangu, ni lazima tuzingatie pande zote tatu na sio mbili tena - Yaani tuitazame serikali, Mtoto wa kike anayebeba mimba na zaidi kiumbe kinachozaliwa.

Binafsi, Naomba niwe wakili wa shetani kwenye hili. Ninaapa nitamtetea hata kama wengi wetu tumeaminishwa kuwa hayupo sahihi.

Ilivyo ni kwamba, Sifahamu kwanini serikali ilichukua uamuzi na kukata shauri watoto wa kike wanaopata mimba kati kati ya masomo yao wasiendelee na masomo baada ya kujifungua, lakini ninafahamu serikali inayo nia njema kabisa kwa watoto wetu hao.

Na bahati nzuri nia njema hiyo ya serikali ipo wazi kabisa. Serikali pamoja na kutoa uamuzi wake huo, ambao unatafsiriwa kuwa ni kumnyima mtoto wa kike haki, lakini pia imeweka mbadala. Kwanini tunasema inamtenga mtoto wa kike? Huo ni uongo uliokubuhu. Na kama ukiniuliza mimi, Nitakuambia kinachofanywa na serikali ni HARD LOVE! Labda siku ambayo tutaacha kuendeshwa kwa hisia na mikumbo ndiyo siku ambayo tutaelewa vizuri zaidi nia njema hiyo ya serikali.

Tatizo ni kwamba binadamu tunachagua kusikia kile tunachotaka kusikia. Tunaona hapa. Hatuoni kule. Hebu tulitazame hili suala lote kwa mapana na ukaribu - Tafiti zinaonesha wasichana wengi wa shule wanapata mimba wakiwa na umri kati ya miaka 16 hadi 19. Tukichukua mfano wa binti aliyepata mimba akiwa na umri wa miaka 18, Hiyo itamlazimu akae nje ya darasa kwa muda usiopungua miaka mitatu.

Hakuna ubishi juu ya hilo. Miezi tisa (9) yaa kulea mimba ongeza miaka miwili ya kumlea mtoto kama inavyoshauriwa kitaalamu na hao hao watetea haki za binadamu. Vinginevyo, Kukatisha malezi na uangalizi wa mtoto ili Mama arejee shule, kwa mtazamo wangu, ni unyama kama ilivyo kutoa mimba. Naamini madaktari watakubaliana na mimi kwenye hili.

Pili, Utayari wa kuendelea na masomo baada ya kuwa nje ya darasa kwa muda usiopungua miaka mitatu unakuwa mdogo sana - Kisaikolojia na hata ki afya ya mwili pia. Umri unakuwa umeenda na nafasi zake za kufaulu hata mtihani wa mwisho zinakuwa ndogo sana.

Hebu waza Mama mwenye mtoto nyumbani anaamrishwa apige magoti na kiranja mkuu wa shule ambaye ni mdogo kwake? Hiyo italeta shida sana, sio kwa walimu tu, bali hata kwa wanafunzi wenzake...

Tukiachana na hayo, swali langu kubwa linakuja - Yule mtoto anayezaliwa akiwa na udumavu na hayuko sawa kiakili kwa sababu alikosa malezi na uangaliza wa mama akiwa mtoto tutakuwa na taifa la watu wa aina ipi miaka 20 au 25 inayokuja? Hebu tufikirie matokeo ya muda mrefu na siyo ya muda mfupi. Hakuna ubishi tukitazama matokeo ya muda mfupi tutaona tunafanikiwa, lakini matokeo ya muda mrefu tunalitafuna na kulinyima haki ya kuishi vizuri taifa la kizazi kijacho - Ambao ni kati ya watoto wanaozaliwa na hao watoto wa kike walio kati kati ya masomo yao.

Mimi nadhani hawa wanaotumia msemo wa "Mfumo rasmi wa elimu" wanakuwa wanakosea. Serikali itakapoanzisha Vocational Training Centres itatengeneza watu ambao wana ujuzi na wasio tegemezi. Hiyo ni moja, Lakini pia hizo centre si zitaingia kwenye mfumo rasmi wa elimu wanaosema... Si lazima zitakuwa na mitaala pamoja na walimu?? Au mimi ndiyo sielewi.....

Faida kubwa nyingine ni kwamba serikali imemtazama mtoto aliyezaliwa, Mtoto wa kike aliyepata mimba kati kati ya masomo na serikali yenyewe. Kusema imekataza mtoto wa kike kupata elimu ni uongo? Ni kuishusha hadhi elimu ya stadi za kazi ambayo, nadhani, ni bora kuliko hata hii ya kufanya mtihani wa taifa! Lakini pia, wakati mwingine kutumia adhabu kali kutaiepushia serikali gharama zisizokuwa za lazima. Naamini ukali wa sheria yenyewe unawadiscourage watoto kujihusisha na NGONO, achilia mbali NGONO BILA KINGA.

Zamani sheria ilikuwa inamkaba anyepachika mimba. Sasa hivi imebana kote. Hiyo inafanya utii uwe wa kiwango cha juu! Tulipe muda hili zoezi, Takwimu zikija kutoka, asilimia za watoto wanaoacha shule kwa sababu ya mimba itakuwa imepungua kwa kiasi kikubwa.

Nihitimishe tu kuwa, Kwenye jambo lolote huwa kuna kafara ambazo lazima zitolewe - Huwa ni suala la uzito tu. Najua wanajeshi wapanga mikakati wanaelewa nasema nini hapa! Sasa kutoa kafara watoto wanaozaliwa kwaajili ya matokeo ya muda mfupi sio jambo sahii mbele za Mungu na kwa jamii nzima, haswa nchi ambayo haiamini kwenye utoaji wa mimba.

Hawa watetezi wa haki, kama wanavyojiita, hoja zao zimeegemea upande mmoja tu - Mtoto wa kike anayebeba mimba akiwa shuleni. Je, hiki kiumbe kinachozaliwa hakina haki? Au wanajaribu kusema utoaji mimba uruhusiwe kwa kundi f'lani la watu? Au iwekwe sheria mtoto wa kike akipata mimba akiwa katikati ya shule iwe ni ruksa kutoa mimba ili aendelee na masomo?

Alamsik.
 
Tunawaita Watoto halafu tunaomba wapate mimba wazae, huu ni muujiza.
 
Imeandikwa kwenye vitabu vya Dini pia madaktari wa afya wameshauri kuwa.

Mtoto anahitaji malezi ya baba na mama Sasa kashazaa huko shulen anaenda kufanya nini?

Mtu alizaa akienda kusoma Tena ataenda kuwamotivate na wengine wawe na familia.

N kosa kimaadili na nidhamu mwanafunzi au mtoto kushiriki ngono na mimba sio kushirik ngono tuu Bali n ngono bila kondomu

Hana sifa za kuwa mwanafunzi Tena huyo.
 
Back
Top Bottom