Hoja rahisi zinaitajika kutumiwa na watu makini kuleta uelewa na kuhamasisha mabadiliko thabiti.

rifwima

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
491
250
Habari JF,

Nianze kwa kuwapongeza wote mlioshiriki na mnaondelea kushiriki katika mijadala mbalimbili kwenye majukwaa tofauti hapa JF na hata nje ya hapa. Mwaka ujao 2014 tuzidi kuendelea na utaratibu huu wa kuibua hoja na mijadala mbalimbali kwa mstakabali wa Taifa hili ambalo sina shaka wote tunalipenda na tunalitakia mema.

Nirudu kwenye hoja ya msingi. Tumekuwa kwenye harakati mbalimbali za kuhamasisha tunachoita mabadiliko, wengi wetu tunafanya hivyo kwa sababu tunaona mambo hayaendi sawa katika maeneo mbalimbali ya uwajibikaji. Kibaya zaidi, tuliowapa mamlaka na raslimali zote kufanikisha matarajio ya wengi wemekuwa butu na Miungu watu kiasi cha kujenga twaswira pana kwa jamii kwambo tumewapa mamlaka ili tuwatumikie, kuwanyenyekea, kuwaogopa na kuruhusu wafanye lolote watakalo kwa maslahi yao.

Hali hii inaondoa dhana nzima ya maana ya Serikali na uwajibikaji kama ilivyo ainishwa kwenye katiba yetu ya mwaka 1977 na marekebisho yake. Matarajio yanayoonekana kwenye katiba ni kupata Serikali na viongozi wanaoheshimiwa na Umma kwa kutimiza wajibu wao. Pia tulitarajia kupa umma ulio na uwezo wa kudhibiti Serikali. Bahati mbaya sana serikali na viongozi wa namna hiyo ina/wanatoweka baada tu ya kushuka kwenye majukaa ya kisiasa pindi uchaguzi unapomalizika. Uchaguzi unapomalizika tunashuhudia Serikali ya Kimwinyi/kisultani pamoja na viongozi miungu watu wasiofuta hata sheria tulizojiwekea. Ni nikipindi hiki ambapo umma unaonekana kutumikia Serikali na Viongozi katika ngazi zote na taasisi zote za Serikali.

Hali hii inatokea kwa sababu mbalimbali zikiwemo mfumo unaozaa viongozi, Uelewa mdogo wa wananchi walio wengi kuhusu wajibu wao kwa taifa, serikali na kwa wao wenyewe. Pia uelewa mdogo wa wananchi kuhusu maana halisi ya Serikali na wajibu wa serikali kwao. Sababu nyingine ambayo inajenga hoja yangu ni wanasiasa, wanaharakati na watu wote wanaoona mambo yanaenda mlama lakini wanashindwa kutumia hoja rahisi kujenga uelewa thabiti miongoni mwa umma wa watanzania kuhusu wajibu wa serikali katika kuleta, kuhamasisha na kutengeneza fulsa za maendeleo.

Sababu hiyo ndo inayosababisha yule anayekusanya machinga na kuwagawia bodaboda achaguliwe kuwa diwani,mbunge, na hata raisi. Ni sababu hii ya kukosa uelewa, umma unaona wajibu wa diwani, mbunge, rais ni kuwapatia fedha wananchi kinyume na utaratibu ambao pia haueleweki miongoni mwa umma. Ni sababu hii ndo inasababisha Serikali inaua raia wake lakini haiwajibishwi na umma na badala yake baada ya mda inachaguliwa tena na umma uleule.

Ni hoja gani? Ni hoja gani rahisi ijengwe miongoni mwa wananchi/umma ili kupata mfumo wa uongozi unaowajibika? Umma/wanachi, wakulima, wafanyakazi, mamalishe na babalise, vijana wa bodaboda, machinga, wavuvi, wachimbaji wadogowadogo wa madini n.k wanawajibika kujua nini?

Umma uelewa maana ya serikali na wajibu wa serikali kwao kwamba:

Mfumo wa kuwa na Serikali ni mbadala wa kila mtu (as an individual) kujitengenezea serikali yake, kwa mfano, mimi Rifwima bila uwepo wa serikali ningejitengenezea serikali kwangu ambayo itajenga shule nitakazotumia mimi na watoto wangu, barabara nitakazotumia mimi na watoto wangu, hospitali nitakayotibiwa mimi na watoto wangu tu, masoko nitakayonunua na kuuza mimi na watoto wangu tu, miundombinu ya umeme kwa ajili yangu na watoto wangu tu, mifumo ya maji kwa ajili yangu na watoto wangu tu. Pia serikali ya nyumabani kwangu itafungua fulsa zinazopatikana kwenye imaya yangu kulingana na maliasili zilizopo i.e madini, mistu, maji, ardhi, wanaya n.k, na fulsa hizo zitatumika kwa ajili yangu mimi na watoto wangu tu.

Hali hiyo ingeleta matatizo makubwa sana kwa jamii. Ni Kwasababu hiyo tumekubaliana, badala ya kila mtu kuwa na Serikali yake, basi tuwe na mfumo kwa sasa wa vyama vingi ulio na watu makini wenye nia thabiti na njema. Watu hao watangaze (campagn) namna watakavyotuletea maendeleao kwenye (Election manifesto).

Wafanye hivyo bila rushwa au mazingira yoyote ya kutilia shaka. Tukilidhika nao, tunawachagua na tunakubali kulipa kodi na kuwapa mamlaka ya kusimamia raslimali zote kwa niaba yetu na badala ya wao kutuletea hela na zawadi, tutataka kodi zetu tunazolipa na raslimali tulizowakabidi zirudi kwetu katika mfumo wa uduma kwa watu na fulsa kwa wote na maisha bora kwa wote.

Kwa maneno mengine rahisi zaidi tulitarajia kodi na rasilimali zetu zikijenga hosptali nzuri, shule bora, masoko kwa wakulima na wafanayabiashara, maji safi na salama ya kunywa, umeme usiokatika, barabara za rami za kiwango cha juu, fulsa za ajira kwa wote n.k. Wakishindwa kufanya hivyo, hawa tuwaite wasalti, wezi, manyang'anyi, majambazi, wauwaji na tuwachukulie hatua za nidhamu. Tuwapoteze kwenye siasa ambayo ni ajira yao.

Hivi ndivyo wananchi wanatakiwa waelewshwe.

Naomba kuwasilisha na niwatakie mwaka mpya mwema 2014.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom