Hoja ni mafanikio ya CHADEMA au tishio la kisiasa la anguko la CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ni mafanikio ya CHADEMA au tishio la kisiasa la anguko la CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Sep 6, 2012.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu watanzania na wote mnaopenda amani nawasalimu kwa jina la Amani ya Bwana, lakini pia niwape pole kwa vifo vya Watanzania wasio na hatia kwa sababu tu neno amani na utii bila shuruti vimeanza kutumika kwa madhumuni ya kulinda masilahi ya kisiasa ya kundi fulani. Kwanza nianze kwa kuwakumbusha migogoro ya kisiasa duniani ambayo watawala waliopo madarakani huyatambulisha makundi yanayowapinga kama wahuni (Ghadafi), waasi (aphatheid system in RSA), wavunjifu wa amani na maneno mengine utayachagua mwenyewe ukianzia na na jinsi CUF, NCCR na sasa CHADEMA walivyokumbana na mkono wa dola kila walipotaka kufurukuta kisiasa.

  Kwa chama ambacho kilisimamia umuhimu wa utawala wa sheria na kulazimika kupata maadui wengi duniani kama TANU na sasa CCM wasemaji wake wangekuwa makini sana na mabingwa wa kuchaguwa maneo ya kutumia hasa wanapotaka kutoa hukumu juu ya hali ya sasa ya kisiasa katika nchi yetu. Chama ambacho kililazimika kumwaga damu ya watanzania ili kusaidia wananchi wa kusini mwaafrika wajikomboe katika minyororo ya tafsiri mbovu ya utawala wa sheria leo wanachama na viongozi wake ati wanashangilia na kutetea tafsiri ya kikaburu ya neno utawala wa sheria, amani na makatazo yanayonyanyasa kisiasa? Hiki ni nini ebu watanzania wenzangu nisaidieni ni kweli yale ninayoyasikia na kuyasoma ni matamko ya CCM? Chama nilichokipenda na kuwa tayari kukifia?

  Mimi nilidhani chama changu kingekaa kimya na kuacha dola ipambane na hali hii ambayo hata hivyo hairidhishi zaidi ya kuomba msamaha kwa yaliyotokea. Suala kuwa kwa nini yalitokea mauaji ya mwandishi wa channel ten ni gumu kwa kiasi kuwa akili ya kawaida inanikataza kusema kitu ingawa macho yangu yameamua kunielekeza kuamini nilichoona kwenye picha na wanaoonekana kwenye picha hiyo. Kwa dhana ya tafsiri ya picha swali ambalo watawala wakiongozwa na Mheshimiwa Nchimbi wangetakiwa kuliuliza ni je tukio la kuuliwa kwa mwandishi huyu akiwa katikati ya walinzi wa amani ilikuwa ni juu ya bahati mbaya au makusudi? Tunawezaji kupata taarifa za bunduki zilizotoka siku ile na mabomu ya machozi yaliyolipuliwa? kulikuwa na haja gani marehemu kuelekezewa silaha tumboni wakati tayari alikuwa mikononi mwa ulinzi wa polisi. Kwa kuwa polisi wameshindwa kuyaeleza haya mapema itawawia vigumu kuja kuyaeleza baadaye, kiungwana inawezekana kabisha katika purukushani ya kusukuma bunduki ikafyatuka na kusababisha maafa.

  Nataka niwataarifu wana CCM juu ya maoni ya watu wa kawaida huku field tuliko na wapiga kura, wanasema nguvu za Polisi juu ya CHADEMA ni kulinda na kujaribu kudhoofisha nguvu za moto wa mabadiliko ambao unahatarisha uhai wa CCM. Wengi wanasema sasa CCM si saizi ya CHADEMA katika nguvu na hoja za kisiasa bila kumtumia C.LIUNDI na Polisi, hatuna chetu.Tusifanye mzaa na hoja hizi tuzichunguze halafu tuchukue hatua sahihi za kisiasa na si vinginevyo. Tanalojukumu la kusoma nyakati kwa nini haya yanatokea? Tunazo sehemu nyingi sana zinazothibitisha kuwa hakuna nguvu ya dola duniani iliyowahi kuzuia matakwa ya jamii, hata Waamerika taifa kubwa duniani na lenye silaha kushinda mataifa yote lakini lilishindwa na vifaru vyake kuzuia matakwa ya akina Martini Luther, IGP soma kurasa za mabadiliko duniani kama watu wenye silaha za aina yako au zaidi waliwahi kuzuia, nakuonea huruma kwani mabadiliko haya yakitokea utasumbuka peke yako na damu inayotokea mikononi mwako.

  Mimi napenda amani lakini amani amabayo ni zao la haki iliyotendeka kwa usawa na napenda vita juu ya haki iliyonyimwa na ndiyo philosophy ya nchi yetu na tulitumia kusaidia wapigania uhuru kutekeleza matakwa yao ya kijamii na kisiasa.

  Lile kundi dogo ambalo halikubaliani na maamuzi ya polisi linayosababu lisikilizwe na lisaidiwe kufanya mambo yake kwa amani.

  Haki si mali ya kikundi ni mali ya mtu mmoja mmoja na kwa hiyo pale unapoona wameunganika wanaunganishwa na vitendo vya udhalimu ambavyo wanahisi wakiwa mmoja mmoja hawawezi kupambana.


  Aluta continua, mission not yet accomplished, comrade in justice is a comrade in combatants and we are the icon of change
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  nakupa MIA mkuu.


  Tuendeleeni kuwaelimisha watanzania, waelimike ili waliondoe madarakani hili li serikali la ccm MAONGO/MAFISADI/MAJAMBAZI/WAUAJI.
   
 3. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mafanikio yepi chadema wamepata zaidi ya kutuandalia wananchi tuwe wakimbizi katika nchi yetu
   
 4. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siasa ni ufuasi na kama ningepata nafasi kufanya tathmini ni chama gani kimepata mafanikio makubwa ya ukuaji wa kisiasa katika muda wa miaka mitano iliyopita bila kupepesapesapesa nitasema CDM kwani chama cha siasa hai ni kuwafikia wananchi na kufanya mikutano, kufungua matawi na kueneza sera zake.kwa takwimu nilizonazo hakuna chama hata kimoja kimewafikia wananchi kwa kiwango ambacho M4C imefanya.
   
Loading...