Hoja Ngeu: Serikali itii kwanza sheria bila shurti... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja Ngeu: Serikali itii kwanza sheria bila shurti...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 12, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mojawapo ya vitu ambavyo tumekuwa tukivisikia kwa muda wa wiki sasa na zaidi ni kuwa wananchi wanatakiwa "watii sheria". Kwamba wananchi wakitii sheria basi hawawezi kukutwa na matatizo mbele ya vyombo vya dola. Wapo ambao wanaamini kauli hii bila kuihoji sana. Na kauli hii inapewa uzito zaidi na ile kampeni ambayo tumeona mara nyingi kwenye luninga na matamasha ya kile kinachoitwa "Utii wa Sheria bila Shurti".

  Kimsingi, hoja ya kutii sheria bila shurti inataka kupendekeza kwa wananchi kuwa watambue matakwa ya sheria na wakisha yatambua wakubali (assent) na kutii (obey). Kwa mfano, mahali ambapo sheria inasema "Usipite hapa" basi mtu asikutwe anapita kwani akiwa anapita atakuwa anavunja sheria na nguvu inaweza kutumika kumzuia asipite (shurti). Kwa kweli kwenye mazingira yenye nchi ambayo utawala wa sheria unatawala wananchi wangekuwa wanajikuta wanatii sheria bila haja ya kulazimishwa.

  Hili ni kweli pia kwenye mambo ya kisiasa ambapo watu wanadaiwa kuwa wawatii polisi bila kushurtishwa. POlisi wakisema rudi nyuma unatakiwa kurudi, wakisema simama unatakiwa usimame na wakisema tawanyika basi unatakiwa kutawanyika. Siyio kusudio langu leo kugusia suala la haki ya mtu/raia kutotii amri halali (inshallah siku nyingine nitagusia hili). Hata hivyo, nataka kupendekeza tu kuwa wale wanaotaka wananchi watii sheria bila shurti wao wenyewe lazima wawe wa kwanza kutii sheria hizo bila kushurtishwa!!

  Kumbe kushurtishwa kuko kwa pande mbili. Wakati polisi na vyombo vya dola vinaweza kuwashurtisha watu kutii sheria wananchi nao wanayo haki na uwezo wa kuwashurtisha watawala kutii sheria! Wananchi wanaweza kufanya hivyo kwa njia nyingi mojawapo ni kutumia Bunge, kuwaandikia watawala na pale inapobidi kuandamana dhidi ya watawala kuwalazimisha kutii sheria.

  Kama watawala wanapata kazi kutii sheria zinazohusiana na manunuzi ya umma, wananchi wanayo haki ya kuwajia ju; kama watawala hawataki kuwakamata wahalifu na kusimamia sheria (fikiria Kagoda) basi wananchi wanayo haki ya kuishrutisha serikali kutii sheria. Ninachosema ni kuwa tunapotaka wananchi watii sheria tujue kuwa nao wanataka kuona serikali yao inatii sheria vile vile bila shurti. Kama serikali inafikiri inaweza kuwashurtisha wananchi kutii basi wananchi nao wana uwezo - na haki - ya kuweza kuwashurtisha watawala nao kutii sheria.

  Hii ni kwa sababu hakuna aliye juu ya sheria. Tunaposema hivi tuna maana hata polisi, usalama wa taifa, JWTZ na hata rais hawako juu ya sheria. Wote wanatakiwa kutii sheria bila shurti. Lakini wasipotii wao basi wajue hawana haki ya kusimama kudai wengine (wananchi) watii sheria. Wanaweza vipi kudai wananchi watii sheria bila shurti wakati wao wenyewe wanaona sheria kwao ni kama "mapendekezo yasiyo na nguvu". Kama sheria inasema polisi wanatakiwa kutoa ulinzi kwa mikutano ya kisiasa bila upendeleo kwanini polisi wasitii takwa hilo la sheria? Kama sheria inasema na kuweka utaratibu wa kumkamata mtu asiye na silaha au asiye tishio kwa polisi au usalama wa wengine kwanini polisi wasitii sheria hiyo lakini wao wanataka wananchi watii sheria ya kutawanyika?

  Utii wa sheria basi unahusu wote, popote na kwa vyovyote. Kama wao wanaonesha jinsi wasivyoweza kutii sheria inakuwaje wanashangaa wananchi wengine wanapoamua nao kutotii sheria? Wao watawala watii kwanza!!

  MMM
   
 2. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nadhani viongozi wa jeshi la polisi wanachanganywa sana. "Sheria" inawataka kutii amri ya mabosi wao hata kama ni kuua huku "sheria" ikikataza kuua! Hapo swala la "utii wa sheria" tena "bila shuruti" ni full confussion!
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Na ukigeugeu wa kutoa kibali halafu kukizuia inachangia maafa.

  Yaliyotokea Arusha na Iringa ni matokeo ya polisi kuongea kwa ndimi mbili. Inaonesha na wao hawajui matakwa ya sheria wanazosimamia
   
 4. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Tumefika hapa kutokana na viongozi wetu kufanya kazi kwa mazoea badala ya kufuata kanuni na miiko ya uongozi.
   
 5. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MMM, hii ni kweli kabisa, viongozi wa Kitanzania wanachotenda ni tofauti na wanachohubiri. Waanze wao kutii sheria bila Shuruti na kufuata kanuni za uongozi na vikiambatana na uwajibikaji. Mathalani, kuna siku nilisikiliza Radio moja hapa mjini DSM ikisema kuwa, wananchi wa maeneo ya Mikoani wanalalamika Vigogo kuwakataza kukata kuni na kutengeneza mkaa, ilihali ukisimama kwenye barabara kuu zote hapa nchini, utakutana na VX aka Kilimo Kwaza yamesheheni Magunia ya mkaa! Hiki ni Kichekesho sana.

  Utii wa sheria utakuwa wa maana sana kwa watu wa ngazi ya chini kama Viongozi wataonyesha mfano katika suala hili mtambuka!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Serikali ya TZhaiwezi kwenda bila shurti..
   
 7. A

  Ame JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Mi sioni confusion yoyote hapo..Kwani hata kama komandi inatolewa bado huyo anayetoa komandi akiwajibishwa na nguvu ya umma kama hataki kuitii bila shuruti wengine wote watatoa komandi zao kufuatana na maelekezo sahihi ya sheria za nchi na hasa ile mama ya katiba.

  Tatizo moja ninaloliona bado umma hauja perceive hii nguvu yao yakulazimisha wale wenye dhamana kutii sheria pale wanapokataa kutii sheria bila shuruti yaani kutoa uongozi kufuatana na sheria. Kwasabau CDM inawaamsha wananchi waelewe huo wajibu wao wakuwasimamia viongozi wakorofi wasiopenda kuongoza kwakufuata sheria wale wale wakorofi wanatumia nguvu bila kufuata sheria kuwanyamazisha wanaotaka kuwalazimisha kuzifuata sheria pale walipokataa kuzifuata bila shuruti.

  Its all about sheria kukata pande zote...Na hapo hakuna confusion yoyote ni ukorofi tu wa viongozi wahalifu kama walivyo raia wahalifu kukataa kuishi kwakufuata sheria. Ila sasa kwavile tumezoea kwa miaka ya karibuni kuona ni raia wadogo wakorofi tu ndiyo ambao sheria inawahusu zaidi basi wengi wanadhani kuna confusion; not at all!
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu hii shuruti ni kwa elite group tu lakini raia wa kawaida yaani commoners na hasa wale rural majority bado social capital yao iko juu sana na hii ndiyo sababu hata wakihongwa bado hawa-default kwakuwanyima mafisadi kura. Hii ni indication kwamba wameingia contract (informaly) na wao huwa hawaivunji hiyo contract kwasababu ya loyalty yao...cultural based.

  Ila angalia elites wote walivyo wasanii na matapeli wamesomeshwa kwa pesa ya umma wanataka ndugu zao wasome kwa jasho lao huku wakiendelea kulipa kodi; wafanyakazi hawafanyi kazi kwa manufaa ya kila mtanzania bali ni mm kwanza wengine baadaye hata kwenye public goods maana wengine watajidai ooh tuko kwenye ubepari; uwongo wao ubepari unatambua public goods na private goods tofauti yake ni ipi....

  Uje kwa wanasiasa is even worse ahadi milioni lakini wakipata kura comitment zero inamaana hapo aliyebaki ni commoner tu ndiyo bado ambao wako loyal lakini si vijana wa leo nao wamesha iga wazazi wao na ndiyo maana taifa very soon litaingia kwenye cheos ambayo Mungu akisaidia msuguano wa matapeli utasababisha tujifunze kuishi kwa sheria ili wote tuwe salama

  Mimi na uliza mpaka tufike huko? We can still decide kujenga nchi yetu katika misingi ya sheria bila mmoja kumlazimisha mwingine; its a choice and fortunately nature has given us a free will to choose!
   
 9. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa kufahamu ukweli huu, nchi haitatawalika. Kila raia akijua haki zake na akatambua namna ya kuzidai, basi watawala watakuwa mashakani
   
 10. d

  dotto JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jinsi ambavyo Polisi hupokea rushwa inakuwa kama sheria nayo. NA inabidi sisi tuitii hii sheria ya kutoa rushwa kwa polisi bila shuruti. Huu msemo wa ovyo na kandamizi!!!
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ...tumefika hapa tulipo kwa sababu ya UDHAIFU wa Rais, uzembe wa Bunge, Upuuzi wa CCM, ....(naongezea ya kwangu), UMBUMBUMBU WA WATAFSIRI SHERIA na UKONDOO WA WATANZANIA.
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,456
  Trophy Points: 280
  Lakini MM, hizo sheria zenye kutakiwa kuwa "assent and obeyed", je wenye kutakiwa kuzitii (hasa kwa upande wa wananchi) walishiriki kiasi gani ktk kuzitunga?Zipo sheria nyingi mbovu na za uonevu ambazo kuzitii ni hatari na uovu zaidi kuliko kinyume chake. Ni vema mchakato wa sheria ukawa mpana na wa wazi. Ukipata hiari ya mtu unaweza kufanya mambo makubwa lakini ni gharama kubwa kumlazimisha punda kunywa maji. Ndio maana CCM kwa kupitia taasisi za serikali na sera nyingi (mfano ya elimu) ikajikita kutengeneza kada fulani kubwa ya wajinga. Ujinga ukawa sehemu na mtaji/mhimili wa mfumo wa watawala. Hawa watu wakizinduliwa usingizini huwezi kuwalaghai tena kwa kauli na matendo za kinafiki kama wanavyofanya kina Nchimbi, Mwema na Tendwa.Nakosoa sana mfumo na sheria nyingi mbovu. Angalia kwa mfano Sheria ya Ardhi Na.4, then jinsi watu wanavyoporwa ardhi zao kila kukicha na kufanywa duni au wakimbizi ktk nchi yao.....kutii sheria mbovu namna hii ni hatari, bali kuzipinga ni afya.
   
 13. Mundungus Fletcher

  Mundungus Fletcher JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 327
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UTII WA SHERIA BILA YA KUSHURUTIHSWA

  Hivi wanamanisha nini "BILA YA KUSHURUTISHWA"

  Hivi tunatakiwa kutii sheria au kuheshimu sheria??
  Msaada wenu kwa wale waloelewa hii kauli
   
Loading...