HOJA MBADALA “Waraka wa wazi kwa viongozi wa CHADEMA” | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOJA MBADALA “Waraka wa wazi kwa viongozi wa CHADEMA”

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Sep 13, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naomba nianze kwa kuazima maneno ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Ndugu, Alexander B. Makulilo kwenye moja ya makala yake kwenye gazeti la Mwananchi julai 23 2011, Taasisi yote ile kama ilivyo kwa chama cha siasa "huzaliwa, hukua, huzeeka na kufa kulingana na mazingira na mahitaji ya nyakati". Hoja kuu ya Makulilo imelenga katika kuona vyama vya siasa kujitathmini kimfumo kuanzia itikadi, ambayo hutoa sura nzima ya muundo wa chama , malengo yake, maadili ya wanachama na viongozi wake na njia mwafaka za upatikanaji wa rasilimali kuendesha chama. Nimeanza kwa maneno haya kutoa tafakari yangu dhidi ya hoja za Mwanajamii mwenzangu anayejitambilisha kwa jina la Mkandara katika uzi wake "Waraka wa wazi kwa viongozi wa CHADEMA"

  Awali ya yote napenda kumpongeza kwa kazi nzuri ya uchambuzi ambao umejaa mantiki ya hoja katika kutafakari na kujadili juu ya mustakabali wa nchi na kutazama kwa kina mwenendo wa siasa katika nchi yetu. Mwandishi ameazima maneno mawili, "do the right things" na "do things right" kuwasilisha kwa mapana mantiki wa hoja yake, nami naomba nielekeze fikra na mtazamo mbadala ambayo itatuwezesha kupanua zaidi wigo wa uelewa juu ya changamoto mbalimbali ambazo zitatusaidia kupima uhai na uhalali wa siasa zetu. Binafsi natazama CHADEMA kama chama ambacho kinakua hivyo bado kina nafasi ya kujitathmini na kuona ni kwa jinsi gani kinaweza kukabliana na changamoto mbalimbali katika kipindi hiki cha maandalizi ya kupewa mamlaka ya kuongoza nchi yetu na watu wake. Ukuaji wa CHADEMA unapitia katika vikwazo mbalimbali ambavyo bila umakini na ujasiri wa viongozi wake na uvumilivu wa wafuasi na wanachama wake chama hiki kinaweza kabisa kupoteza mwelekeo. Tofauti na binadamu mmoja mmoja ambapo vizingiti vya ukuaji wake husababisha kudumaa kimwili na kifikra, vizingiti hivi vina maana kubwa sana kwenye chama cha kisiasa ambacho kinakwenda kupewa mamlaka makubwa ya kuongoza nchi na watu wake.

  Hoja ya Mabadiliko yapi ambayo CHADEMA inayaongoza ni jambo ambalo viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuyapa kipaumbele ili hatimaye yaweze kuingia kwenye bongo za watanzania. Dr. Slaa aliwahi kutamka kwamba angependa kuongoza taifa kwa kufuata vipaumbele wakati wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, na moja ya kipaumbele ambacho CHADEMA inapaswa kuyatekeleza sasa kwa ufanisi mkubwa ni kuwaeleza watanzania ni kwa vipi na kwa namna gani chama kinaenda kuyasimamia yale ambayo wanayoita mabadiliko na hatimaye kuleta matokeo chanya kwa Watanzania na huu ndio utakuwa kianzio (turn point) kutimiza ndoto za mabadiliko ya kiuongozi na kimfumo katika nchi yetu.Watanzania wanapaswa kuelezwa na kuelewa kwamba kinachopingwa si viongozi tu wa CCM bali ni sera zao ambazo hazina tija kwa taifa letu. Na wanaopingwa lazima watambue kwamba wanaopingwa sio wao tu bali ni hoja na sera zao. Lazima Watanzania tuanze kujifunza umuhimu wa kuwekeza katika siasa za akili kufuatana na ujuzi halisi na hali ya mazingira yetu. Hapa naungana kabisa na hoja ya Mkandara.

  Zoezi la kutafuta wanachama kupitia operesheni za chama ni jambo la muhimu katika kujenga misingi madhubuti ya chama kama taasisi imara inayoongozwa na watu wenye weledi wa kutosha kuongoza nchi. Chama chochote makini cha siasa lazima kiwe mkakati na mtaji wa wanachama ambao watakuwa mstari wa mbele kuongoza mabadiliko na kutafsiri kwa lugha fasaha matarajio ya mabadiliko hayo. Siku zote ukienda vitani lazima uandae silaha ili kusambaratisha ngome ya mpinzani, vivyo hivyo ukiwa na kikosi imara katika mchezo wa soka lazima ufanye maandalizi ya kikosi mbadala. Kukuza mtaji wa wanachama ni moja ya silaha muhimu ya kuongoza harakati za mabadiliko. Umaridadi wa kutandaza soka na kufunga magoli ndio chimbuko la kuongezeka kwa mashabiki hivyo ndivyo ilivyo kwa chama cha siasa katika kuongeza mtaji wa wanachama.

  Huwezi kutenganisha siasa za ukanda, ukabila na udini bila kutaja Chama Cha Mapinduzi kama moja ya chanzo kikuu cha kujengeka kwa hisia hizi nchini kwetu. Na hili ni zao la kuwekeza siasa dhaifu ambazo zimejengeka katika kucheza na hisia za ndani za watu. Toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi CCM imeshindwa kujitathmini kisera, kimuundo na kiutendaji, kukubaliana na mabadiliko makubwa na kujikuta ikingia katika siasa za ushindani kwa kutumia njia za haramu (udini, ukabila na ukanda) kupasua ngome ya mpinzani. Na hivyo kupotosha dhana halisi ya demokrasia katika kuwekeza katika siasa za akili zilizojaa busara, ujuzi na maarifa. Hisia hizi ndizo ambazo zinachipuka kwa kasi ndani ya taifa letu. CHADEMA ni chama kinachokuwa hivyo lazima kipitie katika kipindi cha mpito, kuasisiwa na mchaga si hoja ya kusema kwamba chama hiki ni chama cha wachaga la hasha, CHADEMA kama chama ya kisiasa lazima itakumbana na mabadiliko ya kiuongozi ndani ya chama ambayo yatajenga taswira ya kitaifa, ikipingana na mabadiliko ni dhahiri migogoro ndani ya chama itajengeka na hivyo kupoteza mwelekeo.

  Naomba nihitimishe tafakari yangu kwa kuandika maneno yafuatayo; nchi yetu inapita katika kipindi cha mpito kuelekea mabadiliko makubwa ya kisiasa ambacho tusipokuwa makini AMANI yetu itapotea. Suala la msingi tujiulize ni nani tavunja amani ndani ya tifa letu? Ni serikali ya CCM, CHADEMA au CUF? Je tumeridhia mfumo wa vyama vingi kama mtindo (model) kuwafurahisha wajomba na mashangazi wetu wa mataifa ya nje au kuimarisha demokrasia ndani ya taifa letu? Je vyombo vinavyosimamia haki na usalama wa nchi viko tayari kulinda demokrasia tuliyoridhia kwa utu, usawa na haki kamili? Ni dhahiri kwamba nguvu, ubabe na vitisho utapeleka taifa letu mahali kwenye machafuko.
   
 2. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ntarudi kwa ufasaha zaidi....
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  KInachofurahisha wananchi sasa wamekuwa walinzi wa Chadema kila mmoja kwa uwezo wake anatoa ushauri wa aina mbalimbali ,na hii inaonyesha wananchi wengi wanakubali mabadiriko lakini wanashauri njia pana zaidi za kuwafanya wananchi waelewe chadema inasimamia nini
  mimi nadhani wananchi wengi wametangulia kwenye mabadiriko kabla ya chadema
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Good work to considered.
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni ushauri mzuri...nadhani viongozi wamekusikia.
   
 6. m

  mbogamtosi Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 3, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Dedan kimath ni mpigania uhuru wa kenya ni mwanaharakati kwa hiyo WANACHADEMA msikate tamaa, juhudi zenu za kupigania haki ni matunda bora kwa kizazi kijacho.Muangalie Dr SLAA na MBOWE Pamoja na wengine unafikiri wanapigania kwa masilahi yao? "MUNGU HUWATEGEMEZA YATIMA NA WAJANE"This is my own philosophy on what you are doing now and then within the so called M4C pull up your sox, you are going to yield a thousand of CHADEMA convenants (mhehe kijiji IGUNDA IRINGA.
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  you poor thinker, isifikiri wote tuna narrow minded kama zako. who knows akina slaa, mbowe et al wanapigania nini? hiyo ni siri yao na always jenga habit ya kutokuusemea moyo wa mtu mwengine.
   
 8. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #8
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Ushaurim mzuri plus ule wa mkandara. Hope viongozi wanapita humu watajitahidi kadili ya uwezo wao kuangalia the better.
   
 9. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #9
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,395
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280

  Wewe hujamuelewa mtoa mada, na ukisoma vizuri kaweka kama swali. kwanini unamvamia kwa jazba namna hiyo
   
 10. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hapo mwanzo, mwanzo kabisa
  Tasisi zingine huzaliwa na kufa,
  wala hazikui wala kuzeeka!
   
 11. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Well, nadhani suala la msingi ni kutokubali kuwa wasindikizaji wa wanasiasa kwasababu siasa haiwahusu wanasiasa pekee, jukumu letu (wananchi wa Tanzania) lazima tusifunze kuwekeza kwenye siasa za kuhusisha akili zilizojaa maarifa na ubunifu. Tukiwa mbele ya wanasiasa tunaweza kutambua mahitaji halisi kulingana na mazingira yetu ya sasa na matarajio ya baadae. Wanasiasa lazima wawajibike kwa matakwa ya wananchi na sio wananchi kwa viongozi wa kisiasa.
   
Loading...